Rais Samia apandisha kiwango cha Posho ya Kujikimu ya Safari za Ndani ya Nchi na Malipo ya Kazi Maalum kwa Watumishi wa Umma

Rais Samia apandisha kiwango cha Posho ya Kujikimu ya Safari za Ndani ya Nchi na Malipo ya Kazi Maalum kwa Watumishi wa Umma

Kwanza tujiulize kipi kilianza kupanda..Gharama.za Maisha au hizi posho..amefanya jambo jema toka vita vya Urusi vianze maisha yalikuwa tight sana
 
Wale wa 120,000 wanakuwa 250,000
Wale wa 80,000 wanakuwa 100,000
Haya wale wa 100,000 inakuwa ngap mbona hapa papo silence?
 
Hii ni kufuru atasabisha inflation balaa
yani mambo ya hovyo sana hivi vitu vilitakiwa viwe siri sasa hapa ndugu si wataanza kuzingua wakisikia nimesafiri kikazi da alafu wenyewe wanasisitiza tusiweke document za serikali mtandaoni while wao wanatuweka uchi hivi mbona walipandisha madaraja kimya kimya na mambo yakaenda
 
Sawa, Ila watu wa chini nyongeza Yao inasononesha. Wenzao toka 120,000 Hadi 250,000 zaidi kidogo ya mara mbili ya kiwango cha hapo awali. Wao toka shilingi 80,000 hadi 100,000 yaani wameongezewa robo tu ya kiwango cha hapo awali. Ama kweli aliyenacho...
wale wa laki imekua 150 mkuu mama anaupiga mwingi kama mayele
 
Huyu mama kila ushauri anaopewa anakubali tu,,, .atamaliza muda wake hakuna alichofanya...
atakua ameongeza mishahara mkuu ni achievement pia manake mkimpiga mzinga mshkaji wako wa serikalini atakua anakutoa so na wewe utakua umelamba asali mkuu
 
Hatari sana tusijeachwa kwenye financial crisis za hatari. Manake kama unachopata ie kutoka kwenye makusanya ya kodi na mauzo ya nje ni kidogo kulinganisha na kile unachotumia. Sio afya kwenye uchumi wa nchi
Itafikia muda pesa za kulipa wafanyakazi zitakuwa hamna...Itabidi akakope,,.washauri wake sijui ni wakina nani?
 
atakua ameongeza mishahara mkuu ni achievement pia manake mkimpiga mzinga mshkaji wako wa serikalini atakua anakutoa so na wewe utakua umelamba asali mkuu
Upuuzi mtupu....Tunataka miradi mikubwa ya maendeleo kama kipindi cha Magufuli...
 
Rais Samia ameridhia marekebisho ya posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum kwa, ambapo kiwango cha juu kimepanda kutoka Tsh. 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini toka Tsh. 80,000 hadi 100,000/=.

Rais Samia amebadilisha pia kiwango cha malipo cha kazi maalumu kwa ngazi ya chini kutoka 15,000 hadi Sh30,000 kwa ngazi ya kazi kutoka Sh20,000 hadi Sh40,000 na ngazi ya juu kutoka Sh30,000 hadi Sh60,000

Dk Ndumbaro asema kuwa mabadiliko hayo yataanza rasmi Julai Mosi, 2021 na kwamba bajeti iliyopangwa ndiyo itakayotumika kutekeleza viwango hivyo.


View attachment 2240705
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro
Huu ni unyanga'anyi mwingine.
Posho ya juu kutoka 120,000 - 250,000 ongezeko zaidi ya mara 2 yaani %/mia na zaidi wakati posho ya chini toka 80,000 - 100,000 tu ! hapa ongezeko la asilimia isiyo zidi 25!

Taratibu wanaanza kuimarisha matabaka ya walionacho sana na walio na kidogo sana.

Nimeanza kubadili mawazo.Watanzania wenzangu tuamke
 
Ukiongeza spending unaongeza inflation ndugu.. Production ndio zinachochea uchumi kukua.
Utaproduce kama hakuna walaji 😂😂😂😂😂😂😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬..

Do you know even the incentive to produce?

Tuachie wenye taaluwe wewe jikite upande wako..
 
Back
Top Bottom