Rais Samia Apokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe, Ikulu Dar es Salaam

Rais Samia Apokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe, Ikulu Dar es Salaam

nikionaGa picha za huyu bibi huwa naihurumia nchi yangu!
akina bashiru wangesikilizwa kuelekea march 17 hakika tusingekua hapa!
Jamaa wa magwanda wanasema alikomaa. Huwa vijana wa kampuni yake wanadai hakuwa na uwezo wa kimkakati katika maeneo mengi
 
Unao ugonjwa wa kipekee kabisa wewe mtu.
Michango yako yote ndani ya JF tokea ujiunge humu Aug 02, 2016 ni ya aina hii hii, haijabadilika hata siku moja!
Usichojua ni kwamba nimekuwepo humu tangu nilipotoka Darhotwire na enzi za Jambo Forums kabla ya kugeuzwa kuwa Jamii Forums zamani sana kabla yako. Usikariri kwa kuangalia siku nilipojiunga🤣🤣
 
Ndugu zangu watanzania,

Mitaani kumenoga, kumependeza ni furaha ,ni Tabasamu. Ni vicheko ,Ni raha, shangwe Na nderemo baada ya kipenzi cha watanzania, mama wa shoka, mwamba wa Afrika, Jasiri muongoza njia,komandoo hodari, Shujaa wa Afrika, Nembo ya Taifa, Hadhina ya Taifa na Nuru ya wanyonge mh mama samia suluhu Hasssan kuonekana mbele ya macho ya watanzania.

Mitaani,vilingeni na vijiwe vyote mijadala mikubwa imetawaliwa na bashasha na furaha ya watanzania kumuona mama yao hadharani akiwa mwenye furaha,Tabasamu na matumaini makubwa. Watanzania wengine wameonekana wakimuombea hadharani heri ya maisha marefu yenye baraka na amani.Hii ndio maana ya kiongozi wa watu ,Rais samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi wa watu ,mama wa watanzania,mlezi wa Taifa na Tumaini la nchi.

Hakika Rais samia anaishi mioyoni mwa watanzania,nimebeba ndoto na matumaini ya mamilioni ya watanzaniam,. matarajio ya watanzania kwa Rais samia ni makubwa sana.

Ndiyo maana Watanzania wanakosa amani , furaha na amani mioyoni mwao wasipomuona Rais samia hadharani, watanzania wanakuwa wapweke sana wakiikosa sauti ya Rais samia,wanakuwa wenye kukata Tamaa na kuishiwa nguvu wasipomuona Rais wao.

Wanakosa morali ya kazi wasipomuona mama yao maana wanafahamu mama ndiye ajuaye matatizo yao,mwenye uchungu na maisha yao, mwenye kujuwa shida, kero na changamoto za wananchi kwa kuwa wanafahamu huyo ndiye aliyekabidhiwa kila kitu cha nchi hii na kulibeba Taifa katika mikono yake.

Ndio maana wakati na muda wote Rais Samia amelibeba Taifa katika mikono yake kwa umakini m, upendo na uzalendo mkubwa sana katika kuhakikisha kuwa Taifa ni salama na watanzania ni salama,. Huyu ndiye mama samia chaguo la watanzania na Mboni ya Taifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Usichojua ni kwamba nimekuwepo humu tangu nilipotoka Darhotwire na enzi za Jambo Forums kabla ya kugeuzwa kuwa Jamii Forums zamani sana kabla yako. Usikariri kwa kuangalia siku nilipojiunga🤣🤣
Sawa; ina maana hata huko kote ulikoanzia hali ilikuwa hivi hivi kamainavyoonekana hadi leo!
Hili halikustaajabishi wewe?
 
Subiri teuzi.
Sasa hivi mapato hakuna tena yanayokidhi hitaji la serikali.
Wananchi mjiandae kwa kodi au tozo mpya ili kufidia bandari
 
Ndugu zangu watanzania,
...
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Lucas, nimekuwa nikipitia bandiko zako, lakini sikuona umuhimu wa kuzijadili, kwa kuwa hazitofautiani na matamko ya wale ambao amewaita CHAWA wake. Isotoshe, maudhui ya bandiko zako hayatofautiani na ya Bw. Musiba, wakati wa Magufuli.

Ushauri wangu, ungetumia uchambuzi wako wa kumsifia, kujibu hoja pinzani humu JF, km:
1) Tozo za wafanyakazi ambazo mishahara hupitia benki au wanapotuma kwa ndugu zao wakati tayari mishahara imekatwa PAYE

2) Nia ya Serikali kukodisha uendeshaji wa Bandari kwa kutumia IGA badala ya Kituo cha Uwekezaji (Tanzania Investment Centre).

3) Kuchelewa kukamilika kwa miradi ya kimkakati (Bwawa la ufuaji umeme, SGR, nk.), iliyoanza utekelezaji wake wakati wa Awamu iliyopita ikitekelezwa kwa ufanisi na wakati.

4) Kuendelea kukopa huku Serikali ikidai makusanyo ya kodi yameongezeka maradufu, ikiwa ni pamoja na kuwepo tozo za miamala ya fedha

5) Kudolola kwa uchumi, hasa wakati huu ambapo hakuna masharti ya COVID-19 duniani km kuadimika kwa mafuta ya nishati ambako kumesababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na gharama za usafirishaji, au uhaba wa dolari za kimarekani

YAKO MENGI, yenye kero kijamii, kisiasa na kijamii, kuhitaji majibu au ufafanuzi wenye ushahidi wa takwimu za kweli na sahihi.
 
Ndugu zangu watanzania,

Mitaani kumenoga, kumependeza,ni furaha ,ni Tabasamu ,Ni vicheko ,Ni raha ,shangwe Na nderemo baada ya kipenzi cha watanzania,mama wa shoka,mwamba wa Afrika,Jasiri muongoza njia,komandoo hodari,Shujaa wa Afrika ,Nembo ya Taifa,Hadhina ya Taifa na Nuru ya wanyonge mh mama samia suluhu Hasssan kuonekana mbele ya macho ya watanzania.

Mitaani,vilingeni na vijiwe vyote mijadala mikubwa imetawaliwa na bashasha na furaha ya watanzania kumuona mama yao hadharani akiwa mwenye furaha,Tabasamu na matumaini makubwa.watanzania wengine wameonekana wakimuombea hadharani heri ya maisha marefu yenye baraka na amani.Hii ndio maana ya kiongozi wa watu ,Rais samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi wa watu ,mama wa watanzania,mlezi wa Taifa na Tumaini la nchi.

Hakika Rais samia anaishi mioyoni mwa watanzania,Amebeba ndoto na matumaini ya mamilioni ya watanzania,. matarajio ya watanzania kwa Rais samia ni makubwa sana.ndio maana watanzania wanakosa amani , furaha na amani mioyoni mwao wasipomuona Rais samia hadharani, watanzania wanakuwa wapweke sana wakiikosa sauti ya Rais samia,wanakuwa wenye kukata Tamaa na kuishiwa nguvu wasipomuona Rais wao,wanakosa morali ya kazi wasipomuona mama yao maana wanafahamu mama ndiye ajuaye matatizo yao,mwenye uchungu na maisha yao ,mwenye kujuwa shida ,kero na changamoto za wananchi kwa kuwa wanafahamu huyo ndiye aliyekabidhiwa kila kitu cha nchi hii na kulibeba Taifa katika mikono yake.

Ndio maana wakati na muda wote Rais Samia amelibeba Taifa katika mikono yake kwa umakini ,upendo na uzalendo mkubwa sana katika kuhakikisha kuwa Taifa ni salama na watanzania ni salama,. Huyu ndiye mama samia chaguo la watanzania na Mboni ya Taifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Wewe kama sio Mwijaku utakuwa Steve Nyerere.
 
Back
Top Bottom