Rais Samia, asema kuna mabadiliko makubwa zaidi yanafuata, ameanza na Jeshi la Polisi

Rais Samia, asema kuna mabadiliko makubwa zaidi yanafuata, ameanza na Jeshi la Polisi

Rais Kumekuwa na ulazima wa kufanya mabadiliko katika taasisi za haki jamii ili kuboresha suala la utawala bora.

Rais amesema amelazimika kufanya mabadiliko kwenye taasisi hizo ambapo ameanza na Jeshi la Polisi, wataiangalia TAKUKURU, Magereza
Na pia wataangalia mafunzo maana mtu ili apandishwe cheo ni lazima apitie mafunzo ya kitaaluma na kimadaraka.
Kwa uelewa wangu mdogo Mh. Rais ana azimia kufumua Mfumo wa haki jinai/ Criminal Justice System

Wadau wengi wa haki za binadamu pia wanaharakati bila kusahau wanaJF hapa Jamiiforums walizungumzia suala la hitaji la mabadiliko ili kazi hii nyeti kabisa ya utoaji haki izidi kuboreshwa kwa muendelezo.

Leo mheshimiwa rais amefanya mabadiliko kwa imani kuwa anateau mmojawapo wa wakuu wa mfumo unaohusika na utoaji haki kupitia mfumo wa haki jinai akiamini kuwa kutakuwepo mabadiliko na pia uwepo wa uwezo zaidi wa kusimamia watendaji chini yake kufanya kazi vizuri zaidi :

18 September 2021​

Rais mstaafu TLS - Mfumo wa Haki Jinai Tanzania uundwe upya, haki ipatikane​

 
Kwenye ajira aangalie Jeshi sio sehemu ya kupeleka mtoto kwa vigogo ohh mwanangu kafeli hana maisha aende polisi au Jeshi

Kuna video nyingi zikionyesha baadhi ya vijana wakilia mafunzoni inalilia mama zao Kuwa hawataki mafunzo wanataka kurudi nyumbani

Vita ya Ukraine na Urusi wazee reserve imebidi waitwe wakapigane

Jeshi Urusi liligeuka kuwa sehemu ya ajira kwa watoto wa vigogo na wakapandishwa vyeo chap chap bila kukidhi vigezo vya mafunzo makali ya kufa mtu

Vita ya Ukraine ilipolipuka waliteketezwa kama kuku na majeshi ya Ukraine

Kenya pia walikuwa na hiyo tabia kuajiri ndugu nk na kuacha vikabila fit kwenye kupigana

Alshabab walipoanza mambo yao Jeshi ls Kenya likaenda kupigana walifyekwa hasa.Sasa hivi ajira Jeshi la Kenya hakuna upendeleo. Wamejua nini maana ya kuajiri Askari.

Zanzibar mfano mwanzo ilikuwa ukitoa Askari wameiva hasa mfano ni makomandoo marehemu kanali mahafoudh toka afariki hatujasikia mbabe toka Zanzibar ni yupi

Hata vita ya Kagera hawakusikika wababe toka Zanzibar ila bara walikuwa kibao

Zanzibar pia mchujo uwe mkali.Na wajue hawaendi tu jeshini sababu kuna mgao tu wa nafasi kiasi fulani za bara kiasi fulani za Zanzibar kwa hiyo legelege yeyote ruksa kwenda!! Ni kumpeleka akafie vitani .Jeshi sio sehemu ya yakhe yakhe ni roho ya mtu yaweza Potea vitani.Mtu atakuwa awe yuko fit hasa sababu iko.siku aweza pewa kazi ya kulinda Raisi au kuongoza vita .Mchujo unatakiwa kuwa mkali toka chini
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule wafuatao:
1. Inspekta Jenerali CAMILLUS MWONGOSO WAMBURA, kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
2. Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (GP) SIMON NYAKORO SIRRO, kuwa Balozi Wa Tanzania Nchini Zimbabwe 3. Balozi Luteni Jenerali MATHEW EDWARD MKINGULE, kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zambia
4. Dkt. SULEIMAN HAJI SULEIMAN kuwa Balozi



====​

Aliyoyazungumza Rais Samia katika hafla ya uapisho Ikulu, Dodoma: Asema kuna mabadiliko makubwa yanakuja
Rais amempongeza IGP aliyepita Simon Sirro kwa utumishi wake uliotukuka lakini amesema kama maisha yalivyo amelazimika kufanya uteuzi huo. Na ameahidi kutakuwa na mabadiliko mengine makubwa. pia amempongeza kwa kuteuliwa kuwa balozi.

Rais pia amempongeza IGP Wambura kwa kuteuliwa kuwa IGP na amemtaka awe muadilifu katika nafasi yake hiyo aliyoteuliwa baada ya utendaji wake kwa nafasi zilizotangulia kuonekana.

Pia Rais amewapongeza watu wengine walioapishwa.

Rais Kumekuwa na ulazima wa kufanya mabadiliko katika taasisi za haki jamii ili kuboresha suala la utawala bora.

Rais amesema amelazimika kufanya mabadiliko kwenye taasisi hizo ambapo ameanza na Jeshi la Polisi, wataiangalia TAKUKURU, Magereza na Kamishne ya dawa za kulevya ambapo wataangalia mfumo wa utendaji katika maeneo hayo ili kuboresha utendaji.

Amesema wataangalia mifumo ya upandishaji vyeo kwenye taasisi hizo. Amesema ametazama maeneo mengi watu wanakaribia kustaafu lakini mabega yako wazi kama watu walioanza ajira hivi karibuni. Na pia wataangalia mafunzo maana mtu ili apandishwe cheo ni lazima apitie mafunzo ya kitaaluma na kimadaraka.

Jambo lingine litakaloangaliwa ni mahusiano na raia na taasisi nyingine. Ili kuangalia kanuni zilizpo kwa kuwa wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa wageni.

Mwaka wa fedha 2022/23 ameongeza bajeti ya majeshi ili kuangalia stahiki na haki za maaskari. Suala lingine la kuangaliwa ni namna ya kuwaingiza watu katika ajira. Amesema maaskari wengi ukiwatizama na nidhamu yao haviendani. Na inaonekana hakuna kushindwa katika majeshi. Ambapo amesema kuna viashiria ya vyeti feki.

Amesema kutakuwa na mchujo kwenye majeshi yote ili kuwa na wataalamu mbalimbali ikiwemo wataalamu wa fedha, ICT na wataalamu wengine. Pia kuangalia masuala ya tafiti na ugunduzi ili kuwa na zana za kisasa katika majeshi kwa kuangalia mahitaji yakoje.

Mipango ya mawasiliano itaangaliwa ili kujua teknolojia inatumiakaje. Kwa sasa amenza na jeshi la polisi

Kamati ya watu 12 yaundwa.
Kamati inaongoza na Jaji Msaafu Chande Othmani na makamu wake Sefue. Rais Samia amesema ameunda kamati ili kupewa ushauri wa namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi bora. Ambapo wameanza na polisi na watampelekea taarifa ya taaisis nyingine ili kuboresha taasisi hizo.

Rais amesema kwa sasa serikali inakuja na jicho lingine kwenye masuala ya kijeshi ili kuunda majeshi imara na bora katika utendaji.
PIA, SOMA: Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Mongoso siyo mwo
 
Mnacheza na akili za wadanganyika vizuri tu..
Haya ndio mabadiliko?
Hivi kwa nini watawala mnaziba masikio hamtaki kusikia.
Wachafuzi ndio mnawapa kututawala.
KATIBA MPYA MUHIMU KULIKO TUNAVYODHANI
This is a joke! Mabadiliko eti mabadiliko nyie haya tu
 
20 November 2020

Ijue sheria ya mfumo wa haki jinai nchini Tanzania - mwanasheria msomi anafafanua



Source : ITV Tanzania

 
PCCB,DPP na Ma DED,DC,,RC, kiama chenu kinakuja kama mna kesi za kisiasa katika maeneo yenu hiyo tume 12, inafanyia kazi maelekezo ya kamati kuu iliyoyatoa Kwa serikali kufuta kesi za kisiasa, futeni kesi hizo mnazopewa na katelefoni wenu ,safari hii msipozifuta katelefoni anavalishwa shanga na mama
 
Si umemsikia kasema utendaji mbovu sababu kuna wenye vyeti Feki huko majeshini
Weee tulia. Una taka majambazi yarudi? Hao wana vyeti vya ndg zao wako private sector. Ila aawaache tu. Adhibiti kuingia feki wapya tu.

Ila kwa Ramadhani Khamis Kingai, kachemsha!!!
 
Polisi wetu wajitahidi sana kwenda sambamba na mabadiliko ya Tehama.. wawe fiti zaidi kwenye sekta hio kwa kujipambanua kwenye kuzuia na kulinda mifumo ya tehama maana sasa Dunia inahama kila kitu mtandao na wez wamekimbilia huko
 
Back
Top Bottom