Rais Samia ataenda tena kujitambulisha wapi? Sijasikia akizindua hata mradi mmoja

Rais Samia ataenda tena kujitambulisha wapi? Sijasikia akizindua hata mradi mmoja

Akiwa nchini Kenya, Rais Samia alieleza kuwa nia ya kuizuru Kenya mapema sana ilikuwa kujitambulisha kwa majirani kwa kuwa alikuwa "mpangaji mpya"!

Leo akizungumza na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" amekariri tena ya kuwa ataendelea kuzuru nchi mbalimbali akitoa sababu ileile ya "kujitambulisha kwa majirani" akiwa ni "mpangaji mpya"!

Kiongozi mzalendo anawajibika kueleza manufaa ya kila anachonuia kufanya. Inashangaza ni kwa nini Rais anakimbizana kujitambulisha kwa majirani, yaani utii wake upo kwa majirani na siyo kwa mwenye nyumba, watanzania waliompangisha Ikulu yao.

KWA kuwa mwenye nyumba anayo madhara ikiwa ni pamoja na kutompangisha tena, nilitegemea angeweka kipaumbele kuwazuru wananchi kwanza ndipo aanze kupepea iwapo kuna manufaa ya umma katika kupepea.

Nawasalimu kwa jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kazi Iendelee 🇹🇿🇹🇿
Sasa tunaanza kuelewana kuwa tuanzo taratibu na sheria mbovu. Rais anazo nguvu na mamlaka makubwa kuliko kuliko taasisi, analosema ndilo huwa, hata kama halimo kwenye taratibu hata kama halimo kwenye ilani,......mtamdhibiti vipi wakati mmempa kila kitu.
 
UWANJA WA SOKA WA KISASA KUJENGWA CHATO... Serikali itajenga Uwanja wa soka wa kisasa katika eneo la Chato na utajulikana kama Chato Stadium.

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amesema Uwanja huo utakuwa wa pili kwa ukubwa baada ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kalemani amesema Uwanja huo utatumika kwa ajili ya kuvutia watalii na wawekezaji katika masuala ya utalii.

Waziri Kalemani amesema Uwanja huo utaanza kujengwa hivi karibuni.
Baada ya Mkoa wa Chato mkoa upi utafata?
 
Kuzindua miradi siyo kazi ya Rais pekee, Urais ni Taasisi, changamoto tuliyonayo kwa sasa na bahati mbaya hatutaki kubadilika ni kwamba Magufi alifanya "power monopoly". Kila kitu alitaka kufanya yeye, mama anauelewa mkubwa wa maana ya uongozi hususani "Urais".

Kazi kubwa ya kiongozi wa juu (Rais) ni kuunganisha watu, kuonyesha njia iliyo sahihi na kuhamasisha watu wake kujiletea maendeleo kwa kuwatengenezea mazingira wezeshi. Safari ya Kenya inamanufaa makubwa mno kwa nchi yetu, sisi wakulima tunajua.

Waziri mkuu ndo mtendaji wa shughuli za kila siku za serikali, tumuachie huyo kuzindua miradi mpaka pale Rais itakapo bidi. Muda wakujitangaza kila kitu unachokifanya umeisha sasa ni kuacha nature ijitangaze yenyewe.

Uongozi jumuishi ndo uongozi uliofanikiwa sana Duniani, kwanza unapunguza makosa (errors) na unajenga sustainability ya kile unachokijenga. Mama anatakiwa aungwe mkono na kila mtanzania anamaono makubwa (she is visionary leader). Nimalizie kwa kukili tu kwamba sera za mama ni sera nzuri mno na inafaida kwa taifa.

Mwisho, Ujasusi wa Kiuchumi huongozwa na kichwa yaani akili, siyo mabavu. Safari ya mama Kenya tayari ilishafuta na kulisafisha taifa letu juu ya mahindi yetu kuwa na "sumu kuvu" yaani Aflatoxin (big brain ya mama ipo hapa). Hili halikuhitaji kikao maalumu ni kujishusha tu na kulimaliza. Hongera mama, go on your in the right track.
 
Utawala wa sukuma gang umewaacha mkiwa hamuamini kmmk zenu na bado mtashusha nyuzi humu mpaka mtaota sugu. Kibalini tu kuwa nchi hii haitakaa itawaliwe tena na sukuma gang!

Shenzy zao,

Kama wanaumia Sana basi wakamfufue,

Wanatupigia kelele sana
 
Kama kina wauma waka lale nae pale kaburini Chato.
Jamaa tumesha msahau wao bado wanadhani ata amka.

Au kama vip waongee na Gwajima akawasaidie kumfufua,maombolezo yameshaisha na tushamsahau
 
Wanalinda legacy [emoji3][emoji3]
Ez4EgXXX0AADDgd.jpg
 
Akiwa nchini Kenya, Rais Samia alieleza kuwa nia ya kuizuru Kenya mapema sana ilikuwa kujitambulisha kwa majirani kwa kuwa alikuwa "mpangaji mpya"!

Leo akizungumza na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" amekariri tena ya kuwa ataendelea kuzuru nchi mbalimbali akitoa sababu ileile ya "kujitambulisha kwa majirani" akiwa ni "mpangaji mpya"!

Kiongozi mzalendo anawajibika kueleza manufaa ya kila anachonuia kufanya. Inashangaza ni kwa nini Rais anakimbizana kujitambulisha kwa majirani, yaani utii wake upo kwa majirani na siyo kwa mwenye nyumba, watanzania waliompangisha Ikulu yao.

KWA kuwa mwenye nyumba anayo madhara ikiwa ni pamoja na kutompangisha tena, nilitegemea angeweka kipaumbele kuwazuru wananchi kwanza ndipo aanze kupepea iwapo kuna manufaa ya umma katika kupepea.

Nawasalimu kwa jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kazi Iendelee 🇹🇿🇹🇿
Atazindua mingi sanaa kuna daraja la kigongo busisi + tanzanite+ interchange ya kamata+ sgr zinamsubiri azindue ww kaa tu mkao wa kula
 
Back
Top Bottom