Rais Samia atangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
Watu wengi wameshapuuza box la kura. Sioni tena watu wakijitokeza kupiga kura kama awali.
Sahau kuhusu box la kura. Hii nchi haipo shwari kabisa watu wanasubiri catalyst tu wa react.
 
Si angemteua na Salma tujue moja kwa moja kwamba hii Ni awamu ya 4 (b)
 
Muda mfupi ujao Mabadiliko ya Baraza la mawaziri yanatarajiwa kutangazwa kutoka Ikulu Jijini Dar es salaam.

======

Rais Samia amebadilisha muundo wa Wizara Tatu, Ameunganisha Wizara ya Uwekezaji iliyokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa Wizara Moja ambayo itaitwa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya mwisho aliyoifanyia mabadiliko ni Wizara ya Afya

Uteuzi (Mawaziri Wapya):

Nape Moses Nnauye - Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hamad Masauni - Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi

Dkt. Pindi Chana - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Dkt. Angelina Mabula - Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hussein Bashe - Waziri wa Kilimo

Manaibu:
Anthony Mavunde - Kilimo

Jumanne Abdallah Sagini - Mambo ya Ndani

Dr. Lemomo Ole Kiruswa - Madini

Ridhiwani Kikwete - Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Atupele Mwakibete - Ujenzi na Uchukuzi (Upande wa Uchukuzi)


Mabadiliko ya Mawaziri:

Jenista Mhagama - Utawala Bora

Ummy Mwalimu - Afya

George Simbachawene - Katiba na Sheria

Profesa Joyce Ndalichako - Waziri wa Kazi

Innocent Lugha Bashungwa - TAMISEMI

Profesa Adolf Mkenda - Wizara ya Elimu

Dkt. Dorothy Gwajima - Wanawake, Jinsia na Makundi Maalum

Mohammed Mchengerwa - Utamaduni na Michezo

Dkt. Ashatu Kijaji - Uwekezaji


Mawaziri Walioachwa

Palamagamba Kabudi - Alikuwa Wizara ya Katiba na Sheria

William Lukuvi - Alikuwa wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi

Kitila Mkumbo - Alikuwa Wizara ya Viwanda na Biashara

Geoffrey Mwambe - Alikuwa Wizara ya Uwekezaji

=====

Kwa Ufupi;

Ikulu

Mkuchika

Utumishi
Mhagama
Ndejembi

Tamaisemi
Bashungwa
Silinde
Festo

Makamu wa Rais
Jafo
Hamis Hamis


Sera Bunge
Pindi Chana
Nderiananga

Ajira na kazi
Ndalichako
Katambi

Fedha
Mwigulu
Chande

Ulinzi
Tax

Ndani
Masauni
Sagini

Katiba
Simbachawene
Pinda

Mambo ya Nje
Mulamula
Mbaruku

Kilimo
Bashe
Mavunde


Mifugo
Mashimba
Ulega

Ardhi
Mabula
Kikwete

Maliasili
Ndumbaro
Masanja

Nishati
Makamba
Byabato

Madini
Biteko
Kiluswa

Ujenzi
Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya

Viwanda
Kijaji
Kigahe

Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel


Elimu
Mkenda
Kipanga

Maendeleo ya kamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis

Maji
Jumaa aweso
Mahundi

Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

Habari Mawasiliano
Nape Nnauye
Kundo Mathew
Mbona waitara simuoni popote? Waloachwa hayumo, kwenye mpangilio wa wizara hayupo pia
 
Lukuvi vipi tena, mbona jembe sana yule mzee!

Nape amekuja kuharibu mpira wetu

Ohoo kumbe ni habari mawasiliano!!!

Kila lakheri mawaziri, msimwangushe mteuzi tafadhari!!!

Hongera sana Riz, tunaofahamu uwezo wako hatuna wasiwasi na wewe.
 
Juzi juzi hapa eti kalienda Arusha kwa kuunguza kodi za wananchi kukagua nauli stendi akidhan katamfurahisha mama. Kamepigwa chini Sasa. Hakuna tena drama za kisoro.

Bwahaha hahaha hahaha.

Kammmmonnn
Mwenzio anakula milion 11 per monthly alafu unamcheka huku unapiga miayo?
[emoji23][emoji23]
 
Magufuli ameshapanda mbegu ya kuingia madarakani bila kuheshimu box la kura. Mlikuwa mnafurahia ule uhuni, sasa ngoja watu wapeane vyeo kwa kujuana maana hawategemei box la kura.
Kwani mama nae ni dhalimu?
 
Me Sina timu , ila naongozwa na sheria ya right and wrong. Huwezi Nikita nasifia ujinga kama sukuma gang. Mnaona mtu analipeleka taifa shimoni mnasifia tu, kwa kusema mitano Tena, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa hiyo sasa hivi kuna sheria ipi inayofuatwa mpaka unabaki unasifiasifia hovyo, ewe chawa wa mama?
 
Muda wowote baraza jipya....... stay tuned

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua @Nnauye_Nape kuwa Waziri wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua @HusseinBashe kuwa Waziri wa Kilimo na @AnthonyMavunde kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amembadilisha @ummymwalimu kuwa Waziri wa Afya akitoka @OR_TAMISEMI

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Mhandisi Hamad Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi na @ridhiwankikwete kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemhamisha George Simbachawene kwenda Wizara ya Katiba na Sheria

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Mhandisi Hamad Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

#UTEUZI Rais @SuluhuSamia amemteua Profesa Adolf Mkenda kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akichukua nafasi ya Profesa Joyce Ndalichako.

Rais Samia Suluhu amemteua Prof Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu

#MabadilikoBarazaLaMawaziri

View attachment 2073756View attachment 2073757
Ikulu Zanzibar?? Hebu download hizo attachment mbili hapo juu, hasa ile ya pili! Hii imekaaje!
 
Inategemea na mtazamo wa ntu na ntu... kwangu kaongea ukweli... unafikiri kwa nini tanganyika inakomaa na kuoshikitia zenji ilhali hamna daida kubwa inayonufaika nayo kiuchumi?
Ni kwa sababu Waingereza ndivyo walivyokubaliana Na Nyerere Wakati walipomweka madarakani baada ya kupinduliwa Na wanajeshi. Sharti Lao moja ni kuivamia Zanzibar Na kuidhibiti. Waingereza walishiriki katika uvamizi
 
Kuna watu wajinga sana eti mataga tumeumizwa na huu uteuzi kwani ungekuwa wewe ungemwacha mwanao?
Anyway alichokifanya cha maana ni kumtoa hiyo wizara ndalichako, maana dah na kingereza chake kama changu
 
Back
Top Bottom