Rais Samia atangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu
Kwa hiyo lukuvi, kabudi na ndugai ndo presidential aspirants waliokuwa wanamnyima mama usingizi........bila shaka ataanza kulala usingizi wa pono, naona mambo ya ndani tumemweka home boy ili tuandae mazingira ya kulinda ushindi kwa virungu.....
 
Tangu timu zianze kuteuliwa zimebadilisha nini kwenye maisha yako binafsi!?

Umasikini wako utabaki pale pale hata akiteuliwa mjomba ako
Najua timu jiwe wazee wankusifu na kuabudu inawauma sana, tulitoka mavumbuni tutarudi mavumbini, muhimu kuishia kwa maslahi ya umma wa Watanzania, sio kikundi Cha watu flani. Leo uyu kesho Yule, Amina.
 
Muda mfupi ujao Mabadiliko ya Baraza la mawaziri yanatarajiwa kutangazwa kutoka Ikulu Jijini Dar es salaam.

======

Rais Samia amebadilisha muundo wa Wizara Tatu, Ameunganisha Wizara ya Uwekezaji iliyokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa Wizara Moja ambayo itaitwa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Ameunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya mwisho aliyoifanyia mabadiliko ni Wizara ya Afya

Uteuzi (Mawaziri Wapya):

Nape Moses Nnauye - Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hamad Masauni - Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi

Dkt. Pindi Chana - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Dkt. Angelina Mabula - Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hussein Bashe - Waziri wa Kilimo

Manaibu:
Anthony Mavunde - Kilimo

Jumanne Abdallah Sagini - Mambo ya Ndani

Dr. Lemomo Ole Kiruswa - Madini

Ridhiwani Kikwete - Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Atupele Mwakibete - Ujenzi na Uchukuzi (Upande wa Uchukuzi)


Mabadiliko ya Mawaziri:

Jenista Mhagama - Utawala Bora

Ummy Mwalimu - Afya

George Simbachawene - Katiba na Sheria

Profesa Joyce Ndalichako - Waziri wa Kazi

Innocent Lugha Bashungwa - TAMISEMI

Profesa Adolf Mkenda - Wizara ya Elimu

Dkt. Dorothy Gwajima - Wanawake, Jinsia na Makundi Maalum

Mohammed Mchengerwa - Utamaduni na Michezo

Dkt. Ashatu Kijaji - Uwekezaji


Mawaziri Walioachwa

Palamagamba Kabudi - Alikuwa Wizara ya Katiba na Sheria

William Lukuvi - Alikuwa wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi

Kitila Mkumbo - Alikuwa Wizara ya Viwanda na Biashara

Geoffrey Mwambe - Alikuwa Wizara ya Uwekezaji

=====

Kwa Ufupi;

Ikulu

Mkuchika

Utumishi
Mhagama
Ndejembi

Tamaisemi
Bashungwa
Silinde
Festo

Makamu wa Rais
Jafo
Hamis Hamis


Sera Bunge
Pindi Chana
Nderiananga

Ajira na kazi
Ndalichako
Katambi

Fedha
Mwigulu
Chande

Ulinzi
Tax

Ndani
Masauni
Sagini

Katiba
Simbachawene
Pinda

Mambo ya Nje
Mulamula
Mbaruku

Kilimo
Bashe
Mavunde


Mifugo
Mashimba
Ulega

Ardhi
Mabula
Kikwete

Maliasili
Ndumbaro
Masanja

Nishati
Makamba
Byabato

Madini
Biteko
Kiluswa

Ujenzi
Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya

Viwanda
Kijaji
Kigahe

Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel


Elimu
Mkenda
Kipanga

Maendeleo ya kamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis

Maji
Jumaa aweso
Mahundi

Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

Habari Mawasiliano
Nape Nnauye
Kundo Mathew
sorry labda mimi nipo nyuma ya wakati, inakuwaje usema Rais atangaza baraza la mawaziri hapo baadae halafu wewe utupatie baraza la mawaziri ambalo hlijatangazwa? ina maana umedukua mkeka wa muheshimiwa?
 
Wewe endelea kuuwaza upinzani wakati hiyo ccm yako ndo bye bye baba jeni.Kama huna akili zakutosha kusoma alama za nyakati huwezi kuona hilo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sisiemu itaendelea kushinda viti vya ubunge na urais bila hata kuiba kura, kitakachotokea ni wananchi wachache watajitokeza kupiga kura... bado hamna chama mbadala hapa tanzania... chadema muache kudanganyanya, faraja yenu itaendelea kuwa kuona sisiemu wanapasuana ila mwisho wa siku wataendelea kutawala hii nchi kwa muda mrefu sana...
 
Huwa najiuliza sijui Kikwete huwa anaifikiria familia yake kwamba ataiachaje siku akienda au anafikiri ataishi milele? Hakuna Familia inayochukiwa Tanzania kama hiyo na kila siku chuki inazidi.

Haya Spika Ndugai yuko wapi ?
Labda wewe na familia yenu ndiyo mnaichukia! Kwanza chuki ya nini?
 
LAZIMA SASA RAIS SSH AUNDE KIKOSI KAZI CHA KUFATILIA UTENDAJI KAZI WA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU NADHANI INAWEZA KUSAIDIA SANA UWAJIBIKAJI WAO SIYO WANAKUWA WANAGOMBANIA MICHONGO YA PESA TU !!!!!!!!!!!
Huu ndiyo upumbavu tusioutaka. Yani mtu umpe wizara na mshahara alafu uunde kikosi kazi Cha kufatilia?. Pole Tanzania yetu.
 
Huyu Mchengerwa kumpeleka Wizara ya Utamaduni amekosea, kwakeli hata kama ana unasaba nae lakini walau kwa maoni yangu niliona kuna kitu utumishi alikuwa anafanya!!
 
Kwani wasukuma si watu? Mbona ukabila ni mwingi sana siku hizi?? Watu ni kusema sukuma gang tu
Mlivyokuwa mnawasema wachaga mlijua itaishia kwa wachaga tu. Imeanza kusambaa hii dhambi.sasa ipo kwa wasukuma ikitoka uko itaenda kwa makabila wengine. Mpaka mtubu hii dhambi
 
Back
Top Bottom