Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Mawakili wapambanie haki ya huyo kijana alipwe stahiki zake za kudhalilishwa na akishindwa kulipia tutachangia apate haki yake
Inauma sana watu kama hawa kuwa na ukatili huu tena kiongozi upande wa sheria
Afunguliwe mashtaka na apate hukumu yake
 
Kwamba huyo Pauline aliamuru kijana awekewe chupa matakoni? Kwamba huyo Gekul nae ni muumini wa ufiraji na ukatili, yaani katika adhabu zote akaona hiyo ndio inafaa kijana kupewa? Iwe tuhuma au kweli, hatakiwi kuwa waziri na hapa ndipo katiba inatakiwa kuangaliwa tena, hafai hata huo ubunge. Nasema iwe tuhuma au iwe imethibitika.
Mkuu ndio michezo yao. Hata Sabaya alikuwa akiwafanyia hivyo hivyo.
 
Mawakili wapandanie haki ya huyo kijana alipwe stahiki zake za kudhalilishwa na akishindwa kulipia tutachangia apate haki yake
Inauma sana watu kama hawa kuwa na ukatili huu tena kiongozi upande wa sheria
Afunguliwe mashtaka na apate hukumu yake
Nadhani hapa ndipo majukumu ya Waziri wetu Mh Dkt. Gwajima D yanaingia, atusaidie ni jinsi gani wizara yake wanashughulika na case kama hii inayomuhusu kiongozi wa Umma na haswa mwenye ngazi ya Juu kama Waziri, na hapo ndipo tutafahamu kama kuna double standards katika kushughulikia masuala ya ukatili au sheria zinahusu watu wote bila kujali status ya mtu, matukio kama haya hayakuanza leo lakini mara nyingi sheria zimeonekana kuwalinda wakubwa haswa wenye vyeo au pesa.
 
Nadhani hapa ndipo majukumu ya Waziri wetu Mh Dkt. Gwajima D yanaingia, atusaidie ni jinsi gani wizara yake wanashughulika na case kama hii inayomuhusu kiongozi wa Umma na haswa mwenye ngazi ya Juu kama Waziri,
Mimi naona RPC angejiongeza kabla ya kupewa ki memo
La sivyo na yeye ataliwa kichwa kwa kusubiri Rais afanye yake tu
Gwajima anaweza kukaa kimya kwa sababu tayari Rais katimua ila tusubiri watasemaje kwa hili

Ila ni aibu kubwa kuwa na watu wakatili namna hii kwenye uongozi ingawa nao ni binadamu lakini kuna nafasi huwezi hata kuwaza mambo kama hayo
Aliwaza nini kutoa adhabu ya chupa au ni mmoja wa watesaji wa zamani?
 
Mimi naomba niwe tofauti kidogo.

Kwanza sijafurahishwa na kilichotokea natoa pole kwa kijana.

Pili sina imani na mahakama, kutenguliwa imetumika kupoza upepo tu at the end of the day kama atapelekwa mahakamani " it will be a walk in the park"

Sina imani na mahakama za Tanzania hata kidogo achilia mbali polisi maana hapo ingekuwa mpinzani hapo nyumba ingekuwa ishazingirwa na kulazwa mahabusu, ila huyu katolewa kofia tu ya unaibu waziri.

Kwa matendo waliyofanya Makonda na Sabaya ni zaidi ya hili je hampo nao huko mtaani?

Wakongo wanasema Ngai Te!( mimi hapana! )
 
Kweli JamiiForums inasomwa hadi Ikulu.

Hii taarifa ya Gekul kufanya Ukatili ililetwa humu Jana tu

Kudos founder wa huu Mtandao 🫡
JF na Twitter ziko acknowledged sana tu.

Samia yumo humu na alisema.

Twitter alisema anapita sana hadi analijua lile jina la kule "Jamhuri ya Twitter"

Twitter ndio imefanya hadi kina Nape na wenzie wamejulikana walivyo weupe kichwani hadi kufunga comment section.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.

Zaidi soma,

Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili Mtoto

Kuna yule waziri alimsababishia mauti Binti wa udom Bado hajatumbuliwa
 
Naibu Waziri mpumbavu kuwahi kutokea hivi hizi nafasi zinatolewa kwa vigezo gani huyu mama ni wa hovyo since way back nilikuwa najiuliza amekuwaje Naibu Waziri sikuelewa nikasema mambo ya connection yanaleta viongozi wa hovyo.

Hatimaye maji yamejitenga na mafuta mambo yake ya gizani yamedhihirika.

Usicheze na Mungu.
 
Safi sana huwez kuwa wazir wa katiba na sheria alafu ukafanya upuuzi kama huo, nguvu ya social media inaonekana wazi sasa
 
Back
Top Bottom