Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Mwanaume hawez kubakwa Juzi judge mmoja wa Mahakama ya Rufaa katoa tafsiri hiyo
Ndiyo niliona habari. Jopo la majaji watatu. Hii nadhani ni sheria ya kiingereza na nadhani ina upungufu mkubwa wa kupambana na makosa ya ubakaji kwa dunia ya leo. USA siyo hivyo. Wao rape inajumuisha pamoja na mtu kuingiza ''object'' yoyote kwenye uke au sehemu ya haja kubwa. Sheria yao inasema “The penetration, no matter how slight, of the vagina or anus with any body part or object, or oral penetration by a sex organ of another person, without the consent of the victim.”
 
Mimi naomba niwe tofauti kidogo.

Kwanza sijafurahishwa na kilichotokea natoa pole kwa kijana.

Pili sina imani na mahakama, kutenguliwa imetumika kupoza upepo tu at the end of the day kama atapelekwa mahakamani " it will be a walk in the park"

Sina imani na mahakama za Tanzania hata kidogo achilia mbali polisi maana hapo ingekuwa mpinzani hapo nyumba ingekuwa ishazingirwa na kulazwa mahabusu, ila huyu katolewa kofia tu ya unaibu waziri.

Kwa matendo waliyofanya Makonda na Sabaya ni zaidi ya hili je hampo nao huko mtaani?

Wakongo wanasema Ngai Te!( mimi hapana! )
Kwa hio ushauri wako ni upi ? Mana unaonekana hutaki apelekwe mahakamani
 
Kweli JamiiForums inasomwa hadi Ikulu.

Hii taarifa ya Gekul kufanya Ukatili ililetwa humu Jana tu

Kudos founder wa huu Mtandao 🫡
JF na Twitter ziko acknowledged

Samia yumo humu na alisema.

Twitter alisema anapita sana hadi analijua lile jina la kule "Jamhuri ya Twitter"

Twitter ndio imefanya hadi kina Nape na wenzie wamejulikana walivyo weupe kichwani hadi kufunga comment section.

Very interactive and informative.
Kwa hio ushauri wako ni upi ? Mana unaonekana hutaki apelekwe mahakamani
Soma tena vizuri nilichoandika utapata jibu.
 
Pauline hasimuliwi vizuri hata na watumishi wa Wizara aliyokuwepo na hata kule Wizara ya Uvuvi na Mifugo

Ni mtu wa mihemuko na ushamba wa madaraka
Ameshashangazwa. Hadi Rais mwelewa kama Mama Samia anakutumbua ina maana wewe umeshindikana. Na Rais akishakukataa kuna watu lazima wakuoshee kuonyesha kuwa wako kazini. Hapo DPP, Polisi na mahakama lazima wampe kitu inauma.
 
Wewe mpuuzi tu! Unadhani Rais anapaswa kupangiwa cha kufanya? Sasa maamuzi ya Samia unataka kulinganisha na wengine!
Kweli hatakiwi kupangiwa, anaweza hata kuteua majambazi kwenye serikali yake na ukimpangia umekwisha...Ila Mungu fundi
 
Kwamba huyo Pauline aliamuru kijana awekewe chupa matakoni? Kwamba huyo Gekul nae ni muumini wa ufiraji na ukatili, yaani katika adhabu zote akaona hiyo ndio inafaa kijana kupewa? Iwe tuhuma au kweli, hatakiwi kuwa waziri na hapa ndipo katiba inatakiwa kuangaliwa tena, hafai hata huo ubunge. Nasema iwe tuhuma au iwe imethibitika.

..asiishie kwa Gekul tu.

..Makonda naye ashughulikiwe.


..Na Kingai na genge lake waliompoteza komando aliyekuwa mlinzi wa Mbowe.
 
Mama ana legitimize character assassination za kisiasa kwenye mwamvuli wa accountability. Haya mambo huwa hayaishii hapo, yana tabia ya kukurudia hadi wewe uliefanya legitimization ikigundulika vinginevyo. Kinachoonekana hapo ni watu wanatengeneza faida za kisiasa na kukusanya mitaji ya kisiasa wakiwaza 2025. Hili sio geni maana hata mama alishawahi kuliongelea. Critical thinking lakini inatukumbusha kwamba kama Gekul katenguliwa ili awajibike basi kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya husika pia zisiachwe. Ukiamua kucheza na nguruwe kwenye tope basi usiogope tena kuchafuka.
 
amesoma hadi masters bado

Mtu kujivua utamaduni wake ngumu, inatakiwa kufanyiwa social engineering kabla hajatimiza umri wa miaka 4, lakini utegemee msomi aanze kutupa tunguli, 'mikoba' na imani zake zote akiwa na umri wa miaka 21 mwanafunzi mwaka wa kwanza chuo kikuu ni ngumu sana.

Sawa na umuambie mwanaCCM wakulelewa katika chipukizi, UVCCM hadi CCM ya wakubwa ajivue gamba wakati tayari ameshajitoa kifikra na akili yeye ni CCM daima dumu .
 
Raisi wetu hakuwahi kua na ndoto za kua raisi ndo maana hadi Sasa anafanya Mambo kwa kubahatisha bahatisha, Mungu atusaidie tu
 
Back
Top Bottom