Rais Samia atoa Milioni 2 kwa anayekumbatia Watoto hospitali ya Amana

Rais Samia atoa Milioni 2 kwa anayekumbatia Watoto hospitali ya Amana

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25) anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huu umetumwa siku moja tangu mitandao ya Mwananchi Julai 18, 2023 iliporipoti habari kuhusu Mariam na namna alivyosaidia watoto watatu waliotelekezwa na mama zao.

Samia ametuma ujumbe huo leo Jumatano, Julai 19, 2023 uliwasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Brayson Kiwelu ambaye amemkabidhi Mariam kiasi cha Sh2 milioni.

Dk Kiwelu amesema ujumbe huo umetumwa na Rais Samia ambaye amekuwa mstari wa mbele katika huduma za mama na mtoto.

"Rais ametoa Sh2 milioni fedha taslim kumpatia mama huyu kwa kujitoa kwake na amewapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Amana kwa ubunifu huu na uthubutu mama huyu kuwa sehemu yetu.

"Rais ameshukuru sana msaada ambao mama huyu ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji," amesema Dk Kiwelu.

Soma pia
- Mwanamke Anayejitolea Kukumbatia Watoto Njiti Waliotelekezwa Hospitali ya Amana
- Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25) anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana jijini Dar es Salaam.
Jambo alifanyalo mama huyu ni kubwa sana na lenye upendo uliopita kiasi, kwa wasiojua ni kwamba kila siku watotonjiti hupoteza maisha kwa kukosa fukuto toka kwa mama zao ambao wamepata matatizo wakati wa kuzaa, hivyo hulazimika watoto wawekwe kwenye mashinejoto kama ipo na iwapo hakuna inabidi mama yeyote ajitolee kumkumbatia mpaka atakapo timiza uzito muafaka wa kuweza kujitegemea mwenyewe.

Kumkumbatia mtoto ni kulala naye chali kitandani, inachosha ila mama huyu huvumilia kwa sababu anawapenda watoto.

Ndaga mama owombile.
 
Una audit-iwa na nani huo mfuko na una shiing ngapi na hela inatoka kwa vigezo gani, anaewahi kutusha matatizo yake Youtube ?

Walisema huyu mwenzetu kafanya kazi sijui FAO, ana exposure, mbona anafanya mambo kienyeji enyeji ?
Hapo kwenye auditing sijajua. Hivi ofisi ya raisi au ikulu huwa zinafanyiwa auditing?
 
Mbona YY hajitoi na kuhudumia wenye uhitaji mpk anauza BANDARI?
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka Bandari yetu.
Asante
hivi ninyi mbona akili hamna? pesa kapewa mdada wa watu nyie mwapanua midomo. bandari bandari afu ukute kwenyu huko uswekeni hata bandari umekuja kuzionea ukubwani. sasa bandari ushapewa mwarabu fanya unalotaka. mnatushosha sasa
 
Wewe kinachokuuma ni nini?.kwani hii nchi ya baba yako?
 
Back
Top Bottom