Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Fedha hizo zinatumika katika matengenezo yanayotekelezwa kwa awamu, yakiwemo kuziba mashimo, kurekebisha maeneo korofi yenye uharibifu na kuweka tabaka jipya la lami (resealing), pamoja na ukarabati wa sehemu zilizoathirika (partial rehabilitation), kulingana na kiwango cha uharibifu.
Akizungumza Oktoba 25, 2026, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kazi za ukarabati wa barabara hiyo.
Aidha, Mhandisi Besta ameeleza kuwa Serikali, kupitia Kitengo cha Tafiti na Maendeleo (RDU), imekamilisha utafiti na kushauri kuwa barabara hiyo inahitaji kujengwa upya kwa kuwa imefikia mwisho wa muda wake wa usanifu (End of Design Life).
Ameongeza kuwa sehemu zilizobaki zinaendelea kuandaliwa kwa ajili ya utekelezaji, ambapo makandarasi wamepatikana na wanaendelea na maandalizi ya kupeleka mitambo na vifaa vya ujenzi maeneo ya kazi.
Kwa mujibu wa mpango huo, sehemu ya kwanza na ya pili zenye jumla ya kilomita 35 zinatekelezwa na Mkandarasi M/s Saimoo Co. Ltd. Sehemu ya tatu, yenye urefu wa kilomita 15, ipo kati ya Dareda na Masqaroda na inatekelezwa na Mkandarasi M/s Rocktronic Ltd. Sehemu ya nne, yenye urefu wa kilomita 16.5, ipo kati ya Katesh Mjini na Masqaroda na inatekelezwa na Mkandarasi M/s Saimoo Co. Ltd.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Hanang, Mhe. Asia Halamga, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hiyo hususani maeneo korofi.
Mbunge Halamga amesema kuwa kukamilika kwa sehemu ya kwanza na kuendelea kwa kazi katika sehemu ya pili ni hatua muhimu katika kuboresha hali ya barabara hiyo.
Utekelezaji wa matengenezo hayo unalenga kuboresha hali ya barabara, kuongeza usalama wa watumiaji, kupunguza gharama za uendeshaji wa magari na kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo katika ukanda huo muhimu wa kiuchumi.
Pia soma:
- Barabara ya Babati kwenda Singida kuanzia Dareda mission ni Mungu mwenyewe tu anajua tunayopitia
- Mtendaji Mkuu TANROADS atembelea Mradi wa Uboreshaji wa Barabara ya Babati–Gehandu