Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa, Korea, Juni 3, 2024

Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa, Korea, Juni 3, 2024

Acha ujinga. Wameona mama ameboresha kila kitu kilichoharibiwa na lile joka jpm. Nakuhakikishia jpm angekuwa rais mpaka leo nchi imeshapinduliwa siku nyingi au vikundi vya kigaidi vingekuwa vingi. Mama kaleta furaha. Sasa hivi vyombo vya habari vinaandika chochote na wameajiri watu kibao ambao walikuwa mtaani mfano tanzania daima imeajiri wati zaidi ya elfu 50 ambao bila samia wangekuwa wameshakufa nk
Japo mimi sio mwanasiasa wala sipendi kujulihusisha nayo ila jpm ndio kiongozi alifanya mambo ya maendeleo yaliyoonekana kwa mda mfupi tu tangu tumepata uhuru , yule bwana alikua anania ya kufikisha taifa mahali pazuri .

Kipindi chake nilikaa kenya 🇰🇪 kama miezi 6 iv niliona kasi ya huyo bwana ya maendeleo mpaka majirani walikua wanaihofia .
 
Hizi PhD za mfululilizo zinanipa alarm juu ya rasilimali za Tanzania.
India wametoa PhD majuzi tu wamepewa gati nambari 2.
Sasa sijui JMT au DP ndio waliowapa tenda.
Korea nao wameona mpenyo.
umesikia wapi PhD za heshima zikanunuliwa? Mradi unapewa kwa merit yako km kampuni. Omba hata wewe km una uwezo, au ulitaka hilo gati namba 2 aendeshe nani? Mmejaa maujinga tu na husda
 
Hili nalo nendeni mkalitizame
 

Attachments

  • IMG-20240601-WA0037.jpg
    IMG-20240601-WA0037.jpg
    32.8 KB · Views: 2
Japo mimi sio mwanasiasa wala sipendi kujulihusisha nayo ila jpm ndio kiongozi alifanya mambo ya maendeleo yaliyoonekana kwa mda mfupi tu tangu tumepata uhuru , yule bwana alikua anania ya kufikisha taifa mahali pazuri .

Kipindi chake nilikaa kenya 🇰🇪 kama miezi 6 iv niliona kasi ya huyo bwana ya maendeleo mpaka majirani walikua wanaihofia .
Alifirisi nchi. Hakuwa na kipaumbele kulingana na bajeti ya nchi. Huwezi kuendesha nchi as if bajeti ya nchi ni sawa na bajeti ya marekani ndo mana vyuma vilikuwa vimekaza kila sehemu na watu wamekufa wengi kwa stress ndo kuvunjika kwa sababu yake
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Anga cha Korea (KAU) leo tarehe 03 Juni, 2024.


View: https://www.youtube.com/watch?v=3MuZRVjIipc
===
View attachment 3007278
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.


View attachment 3007279
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr wa kwanza kulia, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea

Nyerere,Mugabe nk walitunukiwa nyinsi Sana Sasa sijui kama Ni Upendo wa Mabeberu au? 🤣🤣
 
Tulieni hivyo hivyo nyie si hamjui mnataka nini ? Subirini sasa unaambiwa hata Sultan Mangungo wa msovero alipewa chupa la k vant tu na mashine ya kunyolea ndevu akagawa nchi ,akitokea mtu akikaza wote mnapaza mishipa ya shingo humu ,diktekta,muuaji,mtekaji haya kula Phd hizo na bado phd kutoka Gambia,Togo, Comoro, na burundi nao washaweka oda wanataka watoe phd
 
Back
Top Bottom