Rais Samia atuombe msamaha Wakristo, Simba wa Yuda kwetu ni Yesu Kristo peke yake

Rais Samia atuombe msamaha Wakristo, Simba wa Yuda kwetu ni Yesu Kristo peke yake

Biblia haiwezi kuwa nyepesi inayotafuna herufi kwa herufi. Kuna vitabu vya kinabii mfano cha Ufunuo wa Yohana ambacho kama huna Roho wa Bwana kukufunulia huwezi kuelewa.

Cha kukusaidia tafuta walimu wa dini na watumishi wa kiroho wakusaidie kukufunulia usiyoyaelewa au omba kwa Roho wa Bwana na si kuuliza swali linalotia shaka ufahamu wako.

Swali llinalotia shaka ufahamu wangu?!!---- ni swali linalowashinda nyinyi wenye roho ya Bwana!!, au tuseme huyo roho wenu anaogopa maswali na ndio maana anashindwa kuwafunulia majibu ya hako kaswali ??!.

Ni wapi ndani ya Biblia ambapo ninaweza kusoma ili nitambue kwamba Yesu ndiye Lion of Judah??, just a simple question.
 
Huyo mfalme Selasie hilo jina LA simba alipewa na wazazi wake? Hujui pia alikuwa anajiita mfalme wa wafalme au Utatu mkuu au Aliyeteremshwa na mungu? Huoni kabisa majina yote aliyokuwa anajiita ni makufuru? Najua hujui lakini omba toba kabla ghadhabu ya Mungu haijakuwakia ndani yako.

Narudia tena Simba wa Yuda ni Yesu pekee yako ndio maana hata Diamond anajiita SSimba lakini hakuna anayehoji lakini kwa simba wa Yuda ni jambo jingine

Ni wapi Yesu aliitwa au alijiita Yeye ni simba wa Yuda??--- Nyinyi inaonekana kuna siku mtafanya hila na mtaandika Biblia (katika agano jipya) na humo mtaingiza maneno yenu ili mthibitishe kwa uongo kwamba Yesu ndiye Simba wa Yuda.

Swali bado hamjajibu, ni wapi katika Biblia Yesu alijiita au aliitwa kwamba yeye ni Simba wa Yuda??
 
Ushaambiwa kikristo Simba wa Yuda humrejelea Yesu unaleta ligi yanini?
Haile Selassie wa Ethiopia alijiita Simba wa Yuda, hata bendera yake ilikuwa na picha ya Simba, waulize ma Jah wanaomfata. Au japo jifundishe kutumia google.
 
Kweli kumwita Hayati Magufuli Simba wa Yuda si sawa kabisa. Ni dharau kubwa sana kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo.

Maana kwetu sisi Yesu Kristo ndiye Simba wa Yuda.

Rais kweli hapa si sawa kabisa.
Yaani hiyo ikupe picha kamili jinsi,waislam wengi hata kama wamesoma,wanavyoziona imani za wengine,
Hili limama siku hizi linalipuka hatari Wala halifichi chuki aliyokuwa nayo dhidi ya boss wake JPM!
 
Jiwe si Kuna watu walimwita Yesu kwa sababu alikuwa anawabatiza watu kwa moto
 
Kweli kumwita Hayati Magufuli Simba wa Yuda si sawa kabisa. Ni dharau kubwa sana kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo.

Maana kwetu sisi Yesu Kristo ndiye Simba wa Yuda.

Rais kweli hapa si sawa kabisa.
Majitu mengine nyie ni kama mna upuuzi tu, kweni alipo tamka hakujua kua huyo Simba wa Yuda ni YESU? Kweni wewe hukuelewa anamaanisha nini,? Au ndo unachotaka ni kuona watu wana comment mada yako finyu, siyo kila kitu ni Cha kuongea ongea tu
 
Nimesoma lakini sioni palipondikwa kwamba Yesu ndiye Lion of Judah, hebu wewe unisaidie.
Wewe umeona pameandikwaje? Ukiona huelewi ujue huna cha kukuelewesha ndani yako. Ndiyo ninyi mliambiwa mkikwama muwaulize watu wa kitabu.
Yohana aliona yule anayetakiwa akifungua kitabu ni simba wa yuda pekee na pale ni mtu anazungumziwa sasa kama si YESU BASI NI NANI MWINGINE AMBAYE NI ALAMA SAHIHI YA KIAMA?
 
Nimesoma lakini sioni palipondikwa kwamba Yesu ndiye Lion of Judah, hebu wewe unisaidie.
SOMA ufunuo 22:16 uone huyo anaitwa simba wa yuda na shina la daudi katika ufunuo 5:5 ni nani maana anajitaja kabisa mimi YESU SHINA LA DAUDI
 
Majitu mengine nyie ni kama mna upuuzi tu, kweni alipo tamka hakujua kua huyo Simba wa Yuda ni YESU? Kweni wewe hukuelewa anamaanisha nini,? Au ndo unachotaka ni kuona watu wana comment mada yako finyu, siyo kila kitu ni Cha kuongea ongea tu
Unamfananishaje mbweha na YESU AMBAYE HATA HUYO MBWEHA AMEUMBWA NAE
 
Hakuna anayekataa kwamba Rais Samia anaponyesha majeraha yaliyoletwa na awamu zilizopita hususani ya tano lakini Simba wa Yuda si jina la kumfananisha na mwanadamu.
Kuna kiongozi wa klabu moja maarufu ya soka nchini nakumbuka aliwahi kujiita Simba wa Yuda
 
Unaweza kutoa ushahidi wa andiko yesu anajiita simba wa Yuda?
 
Ushaambiwa kikristo Simba wa Yuda humrejelea Yesu unaleta ligi yanini?
Kwi kwi kwi kwi teh teh teh teh. Judah ni kabila na ndiyo maana yakw tunapopata neno wa Wayahudi, kama Yesu ni Simba wa Wayahudi, wewe mwenzangu na mie kinakuuma nini? Au nawe ni Myahudi?
 
Kweli kumwita Hayati Magufuli Simba wa Yuda si sawa kabisa. Ni dharau kubwa sana kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo.

Maana kwetu sisi Yesu Kristo ndiye Simba wa Yuda.

Rais kweli hapa si sawa kabisa.
Wanazi wa sukuma gang, nawauliza hivi, kwani hamuamini kwenye "kazi ya Mungu haina makosa"?
 
Wewe umeona pameandikwaje? Ukiona huelewi ujue huna cha kukuelewesha ndani yako. Ndiyo ninyi mliambiwa mkikwama muwaulize watu wa kitabu.
Yohana aliona yule anayetakiwa akifungua kitabu ni simba wa yuda pekee na pale ni mtu anazungumziwa sasa kama si YESU BASI NI NANI MWINGINE AMBAYE NI ALAMA SAHIHI YA KIAMA?

Swali mbona ni rahisi tu; Ni wapi katika Biblia au mahali popote Yesu alijiita Simba wa Yuda??.

Nashangaa Wewe unaanza kuniuliza eti kama katika huo ufunuo wa Yohana simba wa Yuda aliyetajwa hapo sio Yesu basi atakuwa ni nani??--- Mimi najibu kuwa; Simba huyo wa Yuda ni Ras Tafari (Haile Selassie) yeye ndiye aliyejiita na akaitwa na anaendelea kuitwa Simba wa Yuda, hatuoni popote kwamba Yesu alijiita au kuitwa Simba wa Yuda katika Biblia ni nyinyi tu kwa tamaa na mapenzi yenu binafsi kwa Yesu mmejiamulia kumpachika Yesu kuwa Simba wa Yuda.
 
Back
Top Bottom