Rais Samia Aufunga Mkoa Wa Tanga Kwa Muda .Watu Wafurika Mkutanoni hata sisiminzi hawezi kupata mahali pa kupitisha Mguu Wake..

Mbona Shule zote kuanzia Kabuku zimefungwa na wananchi wanasombwa na Fuso?
Tayari umeanza kuweweseka. Na hapo ni utangulizi tu kabla ya picha lenyewe. Uwanja umejaa mpaka nje ya uwanja watu wamekosa pa kuweka miguu yao.
 
Kwani wana Tanga wana ongozwa na Tv? Walichagua tv kuwaongoza? Waliombwa kura kupitia Tv? Miradi itakaguliwa kwa Tv? Majibu na majawabu kwa wananchi yatatolewa kwa Tv?
Walifanya hivyo ili mkoa wao ufungwe ?
 
Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe
1740749085016.png

Chozi la furaha limenibubujika kwa comment yako.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni zaidi ya upendo ndugu zangu watanzania ,haya ni mahabaa ambayo watanzania wanampatia Rais Samia. Huu ni upendo wa kukabidhi moyo kwa Mtu. Kwa hakika watanzania wametoa mioyo yao ya upendo na kumpatia Rais Samia.

Huyu Rais Samia siyo binadamu wa kawaida hata kidogo. Ni mtu na nusu, Ni mtu wa watu ,ni kipenzi cha watu, ni tumaini la watu, ni furaha ya watu, ni tiba kwa wenye huzuni na Ni Chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe.

Haijawahi kutokea mkoa ukafungwa na kusimama kwa shughuli zote na watu wote kuisha majumbani na kukimbilia uwanjani kwa ajili ya kwenda kumsikiliza Rais na Mkuu wa Nchi.

Lakini Leo watanzania wameshuhudia watu wakifurika na kumiminika uwanjani hata sisiminzi hawezi kupata nafasi ya kusogeze mguu wake kupata kupita na kusonga mbele. Watu wamejaa utafikiri walivutwa kwa Sumaku. Huwezi ukainua mguu wako na kusogeza pembeni.maana ni mguu kwa mguu na hakuna nafasi ya kujisogeza mwili wako.

Hii yote ni kwa kuwa Rais Samia amegusa Maisha ya watanzania,ameleta matumaini, amewezesha Watanzania kutimiza ndoto zao ,ameleta nuru na tabasamu katika nyuso za watu,ameponya mioyo ya wengi na kuwafuta machozi wengi. Amekuwa mfariji wa watu na mkono wake umemfikia kila mtu na jicho lake ni kama La Tai lenye uwezo wa kuona kila mahali na kumfikia kila mmoja mwenye mahitaji ya kupata Msaada wa Rais.

Amekuwa ni Rais Mwenye usikivu na masikio yake yamesikiliza sauti za kila mtanzania na kila kundi. Kinywa chake kinazungumza yawahusuyo na kuwagusa watu. Amekuwa ni mwenye uchungu na maisha ya watu. Ndio sababu watu wanafurika na kumiminika kumlaki na kumpokea kama Sehemu ya kumuunga mkono na kusema asante mama kwa utumishi wako uliotukuka na tupo tayari kwa utumishi wako kwa muhula wa pili.

Kwa hakika wanadamu tuna mambo na vitu vingi sana vya kumuomba Mungu. Lakini kikubwa ni kuwa kama una hekima na busara za kutosha Basi wewe Omba Mungu akupe kibali na kukustahilisha kwa watu. Rais Samia kwa hakika amepewa kibali cha uongozi na Mungu Mwenyewe. Ameinuliwa kwa ajili ya kuongoza Taifa hili.View attachment 3253029

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hatari wacha upande ule waendelee na tone la maji tone wapate mtaji wa kufungua genge!
 
Mkutano ukiisha, hakikisheni hao watu mnawarudisha mlikowatoa
 
Kwani wamekwambia ni vipofu mpaka wasahau makwao? Wamekwenda kwa miguu yao na watarejea kwa miguu yao wenyewe wakiwa wenye tabasamu na furaha kubwa sana mioyoni mwao.
 
Mbona wewe hujasafirishwa? Watu wana hudhulia kwa hiyari ya mioyo yao na upendo wao kwa Rais wetu
Mimi ninajitambua nasafirishwaje kwenda kumuona muuza bandari? Nimeambiwa maeneo ya Mkinga mabus ya Ratco yameenda kubeba watu bure kwenda kujaza uwanja.
 
Mimi ninajitambua nasafirishwaje kwenda kumuona muuza bandari. Nimeambiwa maeneo ya Mkinga mabus ya Ratco yameenda kubeba watu bure kwenda kujaza uwanja.
Unaona ulivyo Chizi? Si unaona unasema umeambiwa . Sasa nakwambia ya kuwa watu wamefurika na kumiminika kumlaki Rais Samia kwa hiyari ya mioyo yao
 
Ni chizi kwa kuambiwa na ndugu zangu kwamba leo hata wale ambao hawajaenda mjini, wamepata fursa ya kutembea?
 
Mimi siyo chawa ndugu yangu mtanzania. Mimi nawaleteeni taarifa na habari za kweli zikiwa bado za motomoto
Wewe ni zaidi ya chawa mpumbavu, 2mbli mpaka uliharibu ishu yake. Kafie mbali tu, huyo mama yako unayemfanyia uchawa siku akikujua vyema lazima akupige chini. Bora kiasi Tlaatlaah japo mnafanana
 
Wivu tu ndio unakusumbua unapoona watu maelfu mpaka milioni ya watanzania wakimlaki Rais Samia kila akanyagapo. Na huo ni mwanzo tu. Subiri picha yenyewe kampeni zianze utaona moto wake. Ni lazima utachangayikiwa na kuanza kuokota Makopo jalalani huko
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni zaidi ya upendo ndugu zangu watanzania ,haya ni mahabaa ambayo watanzania wanampatia Rais Samia. Huu ni upendo wa kukabidhi moyo kwa Mtu. Kwa hakika watanzania wametoa mioyo yao ya upendo na kumpatia Rais Samia.

Huyu Rais Samia siyo binadamu wa kawaida hata kidogo. Ni mtu na nusu, Ni mtu wa watu ,ni kipenzi cha watu, ni tumaini la watu, ni furaha ya watu, ni tiba kwa wenye huzuni na Ni Chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe.

Haijawahi kutokea mkoa ukafungwa na kusimama kwa shughuli zote na watu wote kuisha majumbani na kukimbilia uwanjani kwa ajili ya kwenda kumsikiliza Rais na Mkuu wa Nchi.

Lakini Leo watanzania wameshuhudia watu wakifurika na kumiminika uwanjani hata sisiminzi hawezi kupata nafasi ya kusogeze mguu wake kupata kupita na kusonga mbele. Watu wamejaa utafikiri walivutwa kwa Sumaku. Huwezi ukainua mguu wako na kusogeza pembeni.maana ni mguu kwa mguu na hakuna nafasi ya kujisogeza mwili wako.

Hii yote ni kwa kuwa Rais Samia amegusa Maisha ya watanzania,ameleta matumaini, amewezesha Watanzania kutimiza ndoto zao ,ameleta nuru na tabasamu katika nyuso za watu,ameponya mioyo ya wengi na kuwafuta machozi wengi. Amekuwa mfariji wa watu na mkono wake umemfikia kila mtu na jicho lake ni kama La Tai lenye uwezo wa kuona kila mahali na kumfikia kila mmoja mwenye mahitaji ya kupata Msaada wa Rais.

Amekuwa ni Rais Mwenye usikivu na masikio yake yamesikiliza sauti za kila mtanzania na kila kundi. Kinywa chake kinazungumza yawahusuyo na kuwagusa watu. Amekuwa ni mwenye uchungu na maisha ya watu. Ndio sababu watu wanafurika na kumiminika kumlaki na kumpokea kama Sehemu ya kumuunga mkono na kusema asante mama kwa utumishi wako uliotukuka na tupo tayari kwa utumishi wako kwa muhula wa pili.

Kwa hakika wanadamu tuna mambo na vitu vingi sana vya kumuomba Mungu. Lakini kikubwa ni kuwa kama una hekima na busara za kutosha Basi wewe Omba Mungu akupe kibali na kukustahilisha kwa watu. Rais Samia kwa hakika amepewa kibali cha uongozi na Mungu Mwenyewe. Ameinuliwa kwa ajili ya kuongoza Taifa hili.View attachment 3253029View attachment 3253121View attachment 3253122View attachment 3253123View attachment 3253125

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hii inaonyesha nguvu yake hata baada ya kuwapopoa akina ummy na january

Mama komaa hapohapo
 
Back
Top Bottom