Rais Samia Aufunga Mkoa Wa Tanga Kwa Muda .Watu Wafurika Mkutanoni hata sisiminzi hawezi kupata mahali pa kupitisha Mguu Wake..

Rais Samia Aufunga Mkoa Wa Tanga Kwa Muda .Watu Wafurika Mkutanoni hata sisiminzi hawezi kupata mahali pa kupitisha Mguu Wake..

Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni zaidi ya upendo ndugu zangu watanzania ,haya ni mahabaa ambayo watanzania wanampatia Rais Samia. Huu ni upendo wa kukabidhi moyo kwa Mtu. Kwa hakika watanzania wametoa mioyo yao ya upendo na kumpatia Rais Samia.

Huyu Rais Samia siyo binadamu wa kawaida hata kidogo. Ni mtu na nusu, Ni mtu wa watu ,ni kipenzi cha watu, ni tumaini la watu, ni furaha ya watu, ni tiba kwa wenye huzuni na Ni Chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mungu Mwenyewe.

Haijawahi kutokea mkoa ukafungwa na kusimama kwa shughuli zote na watu wote kuisha majumbani na kukimbilia uwanjani kwa ajili ya kwenda kumsikiliza Rais na Mkuu wa Nchi.

Lakini Leo watanzania wameshuhudia watu wakifurika na kumiminika uwanjani hata sisiminzi hawezi kupata nafasi ya kusogeze mguu wake kupata kupita na kusonga mbele. Watu wamejaa utafikiri walivutwa kwa Sumaku. Huwezi ukainua mguu wako na kusogeza pembeni.maana ni mguu kwa mguu na hakuna nafasi ya kujisogeza mwili wako.

Hii yote ni kwa kuwa Rais Samia amegusa Maisha ya watanzania,ameleta matumaini, amewezesha Watanzania kutimiza ndoto zao ,ameleta nuru na tabasamu katika nyuso za watu,ameponya mioyo ya wengi na kuwafuta machozi wengi. Amekuwa mfariji wa watu na mkono wake umemfikia kila mtu na jicho lake ni kama La Tai lenye uwezo wa kuona kila mahali na kumfikia kila mmoja mwenye mahitaji ya kupata Msaada wa Rais.

Amekuwa ni Rais Mwenye usikivu na masikio yake yamesikiliza sauti za kila mtanzania na kila kundi. Kinywa chake kinazungumza yawahusuyo na kuwagusa watu. Amekuwa ni mwenye uchungu na maisha ya watu. Ndio sababu watu wanafurika na kumiminika kumlaki na kumpokea kama Sehemu ya kumuunga mkono na kusema asante mama kwa utumishi wako uliotukuka na tupo tayari kwa utumishi wako kwa muhula wa pili.

Kwa hakika wanadamu tuna mambo na vitu vingi sana vya kumuomba Mungu. Lakini kikubwa ni kuwa kama una hekima na busara za kutosha Basi wewe Omba Mungu akupe kibali na kukustahilisha kwa watu. Rais Samia kwa hakika amepewa kibali cha uongozi na Mungu Mwenyewe. Ameinuliwa kwa ajili ya kuongoza Taifa hili.View attachment 3253029View attachment 3253121View attachment 3253122View attachment 3253123View attachment 3253125

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Simizi hao watakuwa na ukubwa kama wa tembo!!
 
Wengi hapo ni walimu na wanafunzi wa sekondari na vyuo. Kuna mtoto wa ndg yangu amenipa taarifa kwamba wamesombwa kutoka chuoni.
Acha kuweweseka wewe. Kwani hao siyo watanzania? Siyo wananchi? Siyo wapiga kura?
 
Leo ijumaa siku ya kazi unakusanya watu na kuzuia shughuli za uzarishaji mali ili iweje?

Nini maana ya mkutano wa hadhara kwa Rais wa nchi? dhumuni hasa ni nini?
 
Alaa hao tuu ndio wanaweza kujaza uwanja 😂😂
Zamani huko nchi za ulaya mashariki madictator wao nao walikuwa wanakusanya watu wengi kwenye mikutano yao ili kuhadaa umma na dunia kuwa wanakubalika sana na wananchi wao. Lakini wingi ule ulikuwa unafanyika kwa vitisho, hongo na ghiliba nyingine za aina hiyo. Na kwa sasa ccm wamecopy tabia zilezile katika kupata mafuriko fake.
 
Leo ijumaa siku ya kazi unakusanya watu na kuzuia shughuli za uzarishaji mali ili iweje?

Nini maana ya mkutano wa hadhara kwa Rais wa nchi? dhumuni hasa ni nini?
Wananchi wamefunga shughuli zao kwa hiyari yao wenyewe ili wakamlaki na kumpokea na kisha kumsikiliza Rais wao kipenzi
 
Back
Top Bottom