PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Pale Kenya ICC iliwakamata wapinzani labda wamesaau baada ya Vifo 1000 tu

Ruto uyu uyu alifika ICC na Uhuru Kenyata.

Sheria inang,ata pote pote!!

Kuwa mpinzani hakunamana yoyote mbele ya Sheria ikibaini wewe ni sehemu ya vile Vifo !!!!

ujue utakamatwa popote ulipo lazima ulipie ushiliki wako iwe fundisho siku zijazo.✍️

Mm nawakumbusha tu sio kwa ubaya!

Wkt wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Aliwai kutembelea Segerea na Keko baada ya apo kesi ya Epa zikaanza
Nimeona niwakumbushe ilo tu linatosha✍️
 
Jaji Shaban Ally Lila akisaidiana na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.

Ni wepesi sana hawa majaji, hawawezi kwenda popote kimataifa kuwa wasuluhishi, wachunguzi au kuwezesha maridhiano popote duniani hata nchi za jirani tu hawazezi kukubalika

TOKA MAKTABA :
Angalizo kutoka kwa msomi Fatma Karume kuhusu katiba, bado kuna kazi kubwa:

TOKA MAKTABA, MAONO :

FATMA KARUME - KATIBA YA 1977 INAMLINDA MWENYEKITI WA CCM ALIYE RAIS NA WATEULE WAKE

Wakili msomi Fatma Karume apigilia msumari mfumo wa mwenyekiti wa CCM Taifa kuteua watendaji wote kwa kupitia katiba ya 1977 iliyotungwa kwa uchu wa CCM kupokonya madaraka kutoka kwa wananchi ..

Nondo za Fatma Karume Juu ya Utendaji wa Mahakama Dhidi ya Matamko ya Kisiasa​


View: https://m.youtube.com/watch?v=K4kVdwF9vrQ
  • Mwaka 1977 katiba iliyoundwa ina uchu wa madaraka ili chama dola kongwe CCM wabaki madarakani milele
  • Majaji walioteuliwa na Kikwete, Magufuli na Samia wamejaa ambao watabaki kuwa majaji kwa miaka 20 ijayo, athari mbaya za katiba ya 1977
  • Ukweli ni huu:1. 1977 CCM ilijitungia Katiba wenyewe bila ya kuwashirikisha Wananchi.
  • 1993 CCM ilibadilisha Katiba wenyewe bila kushirikisha jamii
  • .Katiba ya Warioba ni ya mwanzo (kwanza) kushirikisha Wananchi na CCM ikaipiga BUTI.
  • Ukweli ni kuwa Katiba ya 1977 si ya WANANCHI ni ya CCM..
  • Kuna tatizo juu ya independent transcripts of the court proceedings... Tanzania hakuna... jaji anajiandikia summary yake... hili ni tatizo .. anafanya summary tu kwani haifikii kiwango cha transcripts of court proceedings..
  • Uhuru wa mahakama hauwezi kubebwa na mtu mmoja au jaji mmoja , ni jambo pana...uwepo wa wanakili wa mwenendo wa kesi yaani stenographer, bajeti ya mahakama, uteuzi wa majaji n.k kwa pamoja ndiyo huleta uhuru wa mahakama
  • Jaji Mkuu anachaguliwa na Rais. In fact Rais kamuongezea muda kinyume na matakwa ya Katiba. *Majaji wote wa Mahakama Kuu ...
  • N.k
NO REFORMS NO ELECTION 2025

1779124876555.jpeg

Wadau wa ICC kuhusu uhuru wa tume za kiJaji au Mahakama ukanda wa Afrika

TOKA MAKTABA:

2013 August 28
KWANINI KESI YA WILLIAM RUTO NA MTUHUMIWA MWENZAKE SANG ILIKATALIWA KUSIKILIZWA KENYA AU TANZANIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=85Q4LYZpbS8

Badala yake ikapelekwa ICC The Hague Uholanzi kusikilizwa.

Msemaji wa Mahakama ya ICC Fadi El Abdallah, aelezea sababu zake kesi hiyo kukataliwa na ICC isisilikizwe Afrika ya Mashariki na kujibu maswali kibao lukuki jinsi mwenendo wa kesi utakavyoenda

In this edition of the "Ask the Court" programme: Fadi El Abdallah, Spokesperson of the International Criminal Court (ICC), answers questions concerning proceedings, hearing schedule and presence of the accused during trial which is scheduled to start on 10 September 2013.
1779124967554.jpeg

Jaji Shaban Lila wa Mahakama ya Rufaa Tanzania
 
kimsingi kauli za uchochezi zilitoka pande zote,Serikali ,CCM na Chadema wakiwemo AZAZI. Hili suala ni complicated kinachotakiwa wachunguzi kutoka nje ingesaidia mno kubaini jinai. vinginevyo tunaingia kwenye mkwamo mwingine mkubwa wa kimaridhiano. wanasiasa hili hawaliwezi wanalenga kwenye madaraka mno.
 
Hakuna kitu kizuri kama mtoto wa kike kutumia lugha za kiungwana!, kwa vile hujaziona hadidu za rejea, tusianze kutoleana maneno makali, ngosha kuambiwa na binti anapotosha ni kama...
Nimeisha kusamehe!.
P
Kupotosha ni lugha ya kiungwana,ningesema umeongopa kwa umri ningekua nimekukosea adabu
Mi kidume,jando nikikatwa govi kwa kisu bila ganzi
 
Majasiri ni wachache sana kama shujaa huyu ambaye jina lake linatajawa

JAJI KIPENKA MSEMEMBO MUSSA APUMZISHWA​

1779125683969.jpeg

  • Jaji Mkuu aongoza mamia ya waombolezaji kumsindikiza
  • Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kati atoa ujumbe mzito
Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Singida

Mamia ya Watanzania leo tarehe 6 Novemba, 2024 wamejitokeza kumsindikiza Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kipenka Msemembo Mussa aliyefariki Dunia tarehe 2 Novemba, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Mlonganzila) jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewaongoza watumishi wa Mahakama na Watanzania kwa ujumla katika safari ya mwisho ya Jaji Kipenka ambaye amezikwa kwenye makaburi ya familia Kinampanda katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida.

Viongozi wa Mahakama waliohudhuria maziko hayo ni Majaji sita wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Majaji wanne wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Naibu Wasajili, Watendaji wa Mahakama na Mahakimu kutoka Mahakama Singida. Alikuwepo pia Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fatuma Masengi.

Kabla ya kulazwa kwenye nyumba yake ya milele ilifanyika ibaada iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati, Baba Askofu Dkt. Syprian Hilinti kumwombea Marehemu Kipenka kabla ya Viongozi wa Mahakama, Bunge na Serikali kutoa salamu za rambirambi.

Katika salamu zake, Jaji Mkuu wa Tanzania amemwelezea Marehemu Kipenka kama mtumishi wa umma aliyetekeleza majukumu yake kwa weledi, uaminifu na bidii ya hali ya juu na kwamba mchango wake kwa Taifa hautasahaulika kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya.

“Ili kuweza kupata historia yake kamili ni vizuri kufanya ulinganifu maeneo gani alikuwa anafanya kazi na sheria gani muhimu zilipitishwa au uamuzi gani muhimu umefanyika,” amesema.

Alitoa mfano wa Marehemu Kipenka alipokuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna sheria nyingi muhimu zilipitishwa, ikiwemo Mkataba wa Afrika Mashariki, Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002.

“Kwa hiyo, ukitaka kuandika historia yake ni lazima urejee matukio muhimu yaliyojitokeza ambayo alishiriki bila kupata sifa. Bahati nzuri, kazi alizozifanya akiwa mahakamani zipo katika maamuzi yake ambayo yapo kwenye mtandao wa TanzLII... Court of Appeal of Tanzania – TanzLII Watoto mkitaka kuandika historia ya baba tayari kunataarifa nyingi sana ambazo zipo,” amesema.

Aliwaomba mama mzazi, mke wa marehemu na familia kwa ujumla kuwa na faraja kuwa Kipenka Msemembo Mussa ameacha historia na mchango mkubwa kwa nchi yake na kuwasihi kumshukuru Mungu kwa maisha yake.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Peter Pinda ameiomba familia ya Marehemu Kipenka kuwa na utulivu katika kipindi hiki kigumu na kuwaomba Watoto wasisahau kuwa mwenza wa Kipenka Msemembo Mussa bado yupo.

“Tafrsi ya mwenza wengi hawaielewi, mwenza ni kitu kimoja ambacho kinakaa pamoja, hakuna aliyechini wala juu. Kwa hiyo, nguvu ya mama bado ipo pale pale. Kwako mama kizaa chema, Mungu akutie nguvu sana na uendelee kusihi na wajukuu wako vizuri ili muweze kulimaliza jambo hili salama,” amesema.

Akiwasilisha salamu kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendegu ameunga na wananchi wa Kinampanda katika maeombolezo hayo na kwa kutambua kazi kubwa aliyoifanya marehemu Kipenka kwa Kanisa la KKKT, Mahakama na Taifa kwa ujumla.

Alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, mke na mama wa marehemu kwa msiba huo mkubwa. “Hakuna jambo kubwa kama kupoteza mtoto wakati wewe ungali hai. Unategemea mtoto akuzike, inauma sana kwa mzazi anapomtanguliza yeye…

“Lakini ni mapenzi ya Mungu na tunaiombea familia ishikamane. Haya mazuri yaliyosemwa hapa mwende mkayaenzi, mwendelee kumheshimisha (marehemu Kipenka),” amesema.

Naye Askofu Hilinti akizungungumza kwenye mahubiri, aliwakumbusha waombolezaji kuwa vitu vyote walivyonavyo, ikiwemo cheo, heshima vitawaacha, ila matendo yao wataambatana nayo watakapoiacha Dunia.

“Ili matendo mabaya yasifuatane na sisi ni muhimu kutubu. Tubuni maana ufalme wa Mungu umekaribia. Wapendwa, kila mmoja, kwa nafasi yake, kwa kazi yake asali, awe na ibaada, amwamini Yesu Kristo mfufuka,” amesema.

Marehemu Jaji Kipenka alijiunga na Mahakama ya Tanzania mwaka 2004 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania hadi mwaka 2012 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania kabla ya kustaafu utumishi wa umma mwaka 2019.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Marehemu Kipenka alikuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2004 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Marehemu Kipenka aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Haki za Binadamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali, Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wanne wa amadini Januari, 2006 na Katibu wa Tume ya Rais ya Kuchunguza mazingira ya mauji ya aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa Tanzania, Luteni Kanali Imran Kombe Julai, 1996.

Source : JAJI KIPENKA MSEMEMBO MUSSA APUMZISHWA
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Tume hiyo inalenga kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ili kuchukua hatua stahiki na kuimarisha usalama wa taifa, huku Jaji Lila akisaidiana na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.

====

TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI WA MATUKIO YA GHASIA YA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

Katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 na kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, Mhe. Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume na wafuatao wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume hiyo:-

(i) Mhe. Gad John Mjemmas - Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
(ii) Mhe. Awadh Mohamed Bawazir Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania; na
(iii) Mhe. Aishieli Nelson Sumari Tanzania. Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hapa naona kama kun kundi la watu wanatafutwa kiujanja na watakamtika tuu
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Tume hiyo inalenga kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ili kuchukua hatua stahiki na kuimarisha usalama wa taifa, huku Jaji Lila akisaidiana na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.

====

TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI WA MATUKIO YA GHASIA YA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

Katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 na kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, Mhe. Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume na wafuatao wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume hiyo:-

(i) Mhe. Gad John Mjemmas - Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
(ii) Mhe. Awadh Mohamed Bawazir Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania; na
(iii) Mhe. Aishieli Nelson Sumari Tanzania. Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Nadhani baada ya hii Tume kukamilisha kazi yake itapendekeza polisi wafanye upelelezi ili wahusika wapelekwe mahakamani.
Kwani wao Tume hawatekelezi,bali wanachunguza.
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
halafu kaka pascall mayalla mambo ya kusema hakuwa waandishi creem wa kuuliza maswali, hali na wewe ulikuwepo kwenye kuuliza sio poa.kumbuka ulipofanya mahojiano na kituo kimoja cha habari cha kimataifa..
 
Una ushahidi wa hilo? Wanachama wa CCM Tu wako million 30
Una ushahidi wa hiyo 30m ?? Huu ni uongo wa wazi.

Wao wenyewe husema mara nyingi kuwa wapo 13m, ingawa hata hii siyo sahihi, ni wachache kuliko hiyo figure.

Kumbuka kuna vijana wengi siyo ccm ila hulazimika kujiunga ili kuepuka kubaguliwa na Wahuni kwenye kupata fursa za ajira, biashara, nk..
 
Tume ya Jaji Chande imeleta kizaazaa! Je, na hii nayo tutegemee nini? Hizo hela zinazotumika hazina matumizi muhimu na ya msingi?
Mwendelezo wa ulaghai; akiwa na matumaini atafika 2030.
Kila hatua anayochukuwa sasa hivi lengo ni hilo hilo la kumfikisha 2030, hana jingine lolote.

Hii tume itachunguza ni kina nani hasa waliotekeleza amri ya kuwaua waTanzania?

Kama mauaji hayakupangwa toka mwanzo kabla ya hiyo siku ya uchaguzi; polisi mbona hawakuonekana mitaani wakitumia njia zinazojulikana kudhibiti maandamano.

Walioonekana mitaani ni watu wenye silaha, bila ya unifomu; hawa walitoka wapi na ni nani aliyewaandaa kufanya mauaji?
 
Mapito ya waheshimiwa majaji

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Awadh Bawazir photo

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Mwenyekiti Rufani ya Zabuni za Umma PPAA: Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma PPAA ni chombo cha kisheria nchini Tanzania chenye jukumu la kusikiliza na kutatua malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya ununuzi wa umma na utupaji wa mali za umma. Inafanya kazi kama mhimili huru wa kisheria unaosimamia haki na usawa kwa wazabuni na taasisi zinazonunua .


Retired Judge Gad John Mjemmas
View attachment 3590734

Pichani ni Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Gad Mjemmas ​

The President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, has appointed Retired Retired Judge Gad John Mjemmas as the Chairperson of the Tax Revenue Appeals Tribunal (TRAT) 2025

Baraza la Rufaa la Mapato ya Ushuru (TRAT) nchini Tanzania ndilo chombo cha pili cha rufaa kwa migogoro ya kodi . Jukumu lake kuu ni kusikiliza na kuamua migogoro ya kodi ya kiraia kati ya walipa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hasa likifanya kazi kama chombo cha rufaa kwa maamuzi yaliyofanywa awali na Bodi ya Rufaa ya Mapato ya Ushuru (TRAB). [1, 2, 3]

19 October 2018
View attachment 3590736
Mhe. Jaji Kiongozi (katikati) akimkabidhi shada la maua, Jaji Mstaafu, Mhe. Jaji Gad Mjemmas ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kustaafu salama, anayeshuhudia (aliyesimama nyuma mwenye miwani) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kitengo cha Usuluhishi ‘Mediation’, Mhe. Rose Teemba na kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Crencensia Makuru.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
​


Jaji Aishiel Nelson Sumari
View attachment 3590717
24 Juni 2014 Jaji Aishiel Nelson Sumari mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi Jaji Sumari majaribuni tena Moshi | JAMHURI MEDIA

MAAMUZI YA KESI MUHIMU KABLA YA MAJAJI KUSTAAFU :
..


​

Panafrican Energy T. Ltd vs Commissioner General Tra (Civil Appeal 121 of 2018) [2019] TZCA 170 (31 May 2019) - [2019] TZCA 170​

​

18 May 2026

JUDGE SHABAN ALLY LILA TO LEAD THE TANZANIAN COMMISSION OF INVESTIGATION INTO THE CRIMES AGAINST HUMANITY FOLLOWING RIOTS OF OCTOBER 29, 2025​

Monday, May 18, 2026



The President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan today, Monday May 18, 2026, in implementing the recommendations of the Presidential Commission to investigate incidents of breach of peace that occurred during and after the October 29, 2025 General Election, has formed a Commission to be headed by Court of Appeal Judge Hon. Shaban Ally Lila to conduct a criminal investigation into the events of October 29, 2025.
1779127992947.jpeg

Photo : Judge Shaban Ally Lila

A statement issued by the Chief Secretary of the cabinet, Ambassador Dr. Moses Kusiluka, said President Samia has also appointed Hon. Gad John Mjemmas, Retired Judge of the High Court of Tanzania, Hon. Awadh Mohamed Bawazir, Retired Judge of the High Court of Tanzania and Hon. Aishiel Nelson Sumari, Retired Judge of the High Court of Tanzania, as Commissioners of the Commission.
1779128175538.jpeg

Photo : Retired judge Gad John Mjemmas

According to Ambassador Kusiluka's statement, the appointment made by President Samia Hassan was made in accordance with the powers she has under the Commission of Inquiry Act, Chapter 32.
1779128386062.jpeg

Photo : Retired judge Aishieli Nelson Sumari

Retired Chief Justice Mohamed Othman Chande proposed the establishment of a Criminal Investigation Commission to investigate in detail specific criminal incidents against humanity, looting and riots that occurred during and after the October 29, 2025 General Elections. The recommendations were made in April 23rd, 2026 when the Presidential Commission to Investigate Incidents of Breach of Peace submitted its report to President Samia Suluhu Hassan.
1779128451678.png

Photo : retired judge Awadh Bawazir

Judge Mohamed Chande explained that, although his commission identified the sources and general trends of violence before and after the October 29 General Election, there are serious criminal matters the likes of random and indiscrimately shooting of thousands of people termed as summary executions that require a special investigative body to facilitate legal accountability.
 
halafu kaka pascall mayalla mambo ya kusema hakuwa waandishi creem wa kuuliza maswali, hali na wewe ulikuwepo kwenye kuuliza sio poa.kumbuka ulipofanya mahojiano na kituo kimoja cha habari cha kimataifa..
Sisi waandishi tunajuana, wako waandishi maripota, kazi yao ni kutumwa na kuripoti, tupo waandishi wa analysis, ambao tumegawanyika makundi mawili
1. kuna waandishi wenzetu ni machawa, ambao wanauliza maswali mepesi mepesi
2. Kuna waandishi ni ma critical, tunauliza maswali magumu, viongozi hawapendi maswali magumu, hivyo kwenye baadhi ya events, sisi ma critical hatualikwi!.
P
 
Ukihesabu hasara uliyopatikana kwa kumkumbatia huyu mwanamke na kumpa urais wa mchongo ni zaidi ya trillion 5, Anza na hasara za kuitisha uchaguzi hewani,hasara za vurugu,hasara za kunyimwa misaada,hasara za Kutuma wapumbavu wenzie nje ya nchi ili kumsafisha ,hasara za kuunda tume feki.


Huyu mwanamke ni Bora angejiendea kwake zanzibar. sidhani kama ataiepuka ICC, probability ni 0.001
 
Back
Top Bottom