PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hii tume itachunguza ni nani na nani waliratibu maandamano ili wapewe mzigo wa vifo na katu haitachunguza waliuwa waandamanaji.
 
Hata tume ya kuchunguza ali kibao mpaka leo haijaleta majibu..
Kama wanataka ukweli wajiuzulu kwanza..
Huwezi kuona msitu ukiwa msituni utaona miti tu
 
Subiri tume ilete majibu acha kuwalisha maneno.
Tume ipi, ile aliyounda kuhusu mauaji ya Ali Kibao na kutaka ripoti haraka una majibu yake? Ni hivi, tarehe 9 tunarudi barabarani, hiyo tume ya ccm ikampelekee majibu anayoyataka yeye, hatuna muda na hayo maigizo yake. Yeye ni rais aliyetangazwa kwa mtutu wa bunduki, na hana uhalali wa umma.
 
Hasira hasara. Kama umehusika mkono wa sheria utakupitia.
 
Hii midhaha na utani wake kwetu mpk tufanye jambo litakalo mgusa moja kwa moja km kwa kina jux ,nenga na shishi lbd utaelewa
 
Huyu bibi ana dharau kupita dharau yenyewe
 
Ukifatilia matendo yake,kauli zake,mauaji,hotuba ya juzi,Uteuzi wa mawaziri,.na Leo Tume
Utagundua huyu bibi ana provoke watanganyika makusudi,anataka kujua kitu gani kita tu trigger the most hadi tuchukue hatua,

challenge accepted Samuya
 
Tume huru unataka iundwe na Maaskofu wa TEC. Walio kwenye Tume ni majaji wakuu wastafu wanaoheshimika duniani kote. Wewe unataka wawekwe akina nani?
Kuwa serious kwenye mambo yanayohusu maisha ya watu mkuu ,watu wameuawa wewe unaleta upuuzi wako wa UDINI.

Unataka kusema haujui maana ya tume huru? Yaani wewe kwa akili yako ya STD II unahisi kwamba kina Mwema ,Tax ,Chande wataleta ripoti ya uchunguzi sahihi? Tume zote alizounda SAMUYA ngapi zimeshaleta matokeo yake? Mbona tume alizounda kikwete wakati akiwa na akili zake mbona zilitoka? na mojawapo ni ile iliyomtia hatiani Zombe(OC-CID) na Afande bageni kwa mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge.
 
Mtuhumiwa namba moja ndio aliyeunda tume. Mtu mjinga tu ndii anaweza kuamini hao wahuni waitwao tume huru.
Subiri uone kitakachotokea. Unadhani kupindua serikali ni jambo dogo. Baada ya wiki mbili hii message utakuja kuirudia. Serikali haifanyi mambo kwa mihemko. Kila kitu kinawekwa kwenye utaratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…