Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Si unaona wakina Nape, Kigwangalla wanapumua sahii kutoa utopolo wao kwenye media! Kipindi cha Jiwe, Thubutu...!
Hahaaa watanzania hatuekeweki mtu akiwa fair ni shida akiwanyoosha wanaanza kulia Lia, jakaya was fair uchumi ulikuwa mzuri, democracia ikakua, aliajiri kila mwaka chakushangaza nyaraka za maaskofu zilikuwa zinatoka daily, kaja magufuli akawanyoosha Hadi maaskofu wakawa dhaifu, Sasa kwa Raisi Samia wameanza Tena, Tena mtu karekebisha wanachonga ngenga
 
mimi sina resources kama za rais usinilinganishe na rais ambaye mpaka mswaki anapigwa. siwezi kuingia chama kifala namna hiyo
Mkuu punguza ukali wamaneno sote twajua kuwa unauchungu sana na nchii na nimzalendo pia.
 
CV ya yule kijana wa uvccm iliniacha hoi
 
Kwenye kibao motomoto cha Reggae strong-Lucky Dube unaambiwa Reggae's everywhere.

Mama anacheza tu reggae kwenye hizi teuzi wala hazina tija yoyote zaidi ya yeye ku-exercise mamlaka yake.

Tuwe tunaambiwa na sababu za mtu huyohuyo mmoja kutolewa point F na kupelekwa J.

Kama KM ka-underperform wizara G,kuna muujiza gani atafanya huko wizara H anayohamishiwa?

Ushauri:Aendelee na wateule wote wa mtangulizi wake kama walivyo tu bila hizi sub za ajabuajabu.

Huku kwa DEDs,RAS,DCs and RCs atatuletea mpaka vichaa kwa staili hii.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa mkuu wa shirika la maendeleo ya petrol( TPDC), Bw Thobia Mwesiga Richard leo tarehe 5, April 2021.

Bw Thobias Mwegisa Richard aliteuliwa jana na ilitarajiwa ale kiapo kesho April 6, saa nne asubuhi.
View attachment 1743924
 
Yaani Tumevurugwa! halafu hamna watu walinistaajabisha kama Maaskofu, JPM alikuwa anajua kuwaweka mtegoni baada ya corona kuingia akaitisha Maombi halafu ghafla akakatisha kutangaza maambukizi halafu akadai Maombi yameponya hamna alimpinga!

Baada ya Makasisi na Masista kuanza kuputika huko waliko wakanza kulia nyau wakati kipindi JPM anasema maombi yameponya walim-support! Na tena wale wabishi waliwanyang'anya passort zao!
 
James mataragio ni mtu wa karibu sana na JK. Hivyo kumrudisha tena mataragio ni yale tuliyoyasema swali kuwa JK= SSH
Kama una kumbu kumbu nzuri huyu Mataragio alifanya pia kazi na JPM; na JPM ndiye aliyeamuru afutiwe kesi aliyokuwa nayo mahakamani baada ya kuona kuwa haikuwa na msingi.

Wewe tatizo unaloona kwa Mataragio ni lipi wakati ana sifa zinazostahili kwa huo wadhifa na hakuna tuhuma zozote zinazomkabili?!
 
hata Kigogo kasema huyu alikuwa DSO , kada wa CCM sasa haya mambo ta TPDC wapi nawapi? Samia analetwa mezani bila yeye kufanya personal scrutiny... kuna hatari mbele iakuja.. tena kubwa
Mchakato wa teuzi za Viongozi wa Mashirika ya Umma zinafanywa na Wizara husika.
Tujiulize, Dr. Medard Kalemani alimpendekeza Mwesiga kwa vigezo vipi?
Nashawika kuamini kuwa Dr. Kalemani alipeleka jina hilo Ikulu kwa shinikizo.
Shinikizo la CCM.
JPM na Bashiru wangekuwa bado wako kwenye viti vya Enzi, Mwesiga asingetumbuliwa.
 
Hajui kuwa wa kwanza kumrudiishia cheo chake mataragio alikuwa mwendazake JPM
Najua Lord denning ndio maana nimeuliza kwani uhusiano au ukaribu wake na JK una uhusiano wowote na majukumu yake kiserikali?
 
Duuu hii habari mpya kabisa haijawahi kutokea miaka yote mitano ya Magufuli.
Mbona imetokea sana fatilia bana kuna watu walitajwa kuteuliwa lakini walitenguliwa kabla ya kuapishwa tena wengine wakiwa wamefika ikulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…