Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

na alipo teua akaja na vichekesho
 
Acha kuijfanya mjuwaji miezi mitatu unataka kuteua malaika?
 
Hii ni doa la mapema sana,binafsi sitegemei jipya sana.......nini kilimfanya atengue na nini kimemfanya arudishe......waandishi wa habari kamuulizeni siku ya kuapisha
 
Atakuja saini kitu then too late...
Umenikumbusha bosi mmoja aliagiza baadhi ya watumishi kufukuzwa. Barua zikapelekwa kwani akasaini zote.
Siku moja kaenda kijijini kwao kusalimia wazazi akamkuta mdogo wake yupo huko kama mwezi, bosi kumuona akahamaki kwa nini yupo hapo na kazini hayuko.
Akaletewa barua aliyoisaini ya kumfukuza kazi mdogo wake, bosi hakuwa na la kufanya zaidi wa kupata fadhaa ya familia.
 
Karibuni serikali nyingi duniani hupambana social media utopolo ambazo habari zake hazichujwi kila mwehu ni mwana habari huweka bandiko na likarushwa hewani.

Nahayo unayoyasema viongozi kfanya maamuzi na kukimbilia social media kutizama marejesho hizo ndoto za mchana Maamuzi mangapi mzee wa HAPA KAZI ALIFANYA na watu wakatoa povu lao ktka social media mpaka kuzirahi humo lakini hakuna kilichobadilika.
 
Mama naye ni kama mama zetu na ni binadamu kama sisi, kukosea lazima hasa ukizingatia kipind hiki ndo kwanza anaanza
 
Ila watanzania mna midomo sana wakati mwingine Marehemu alikuwa sahihi kuwajibu mbovu.kitu kidogo mnakishupalia utadhani nini.
 
Kuna muda mwingine zaidi ya huu alionao?
Tatizo letu UmuchKnow mwingi sana Wabongo.

Kila kitu tunajifanya tunajua alafu we c ndo unelalamika ile thread juu ya huyu jamaa mbona tena hauridhiki au ulitaka uchaguliwe wewe[emoji3][emoji3][emoji3]
Mkuu sasa ndio naelewa kwanini Marehemu alikuwa anawatukana watanzania wana mdomo na ujuwaji sana.
 
Mimi nahisi watu walichomekea Hilo jina na CV yake isiyoeleweka ili kumharibia Raisi aisee kwa makusudi kabisa. Mazaa awe makini sana

..nafasi ya DG wa Tpdc inapokuwa wazi huwa tangazo linaweka ktk vyombo vya habari ili walio interested watume maombi.

..baada ya hapo kuna vetting inafanyika na majina machache hupelekwa mbele ya JOPO litakalowafanyia interview waombaji wa nafasi.

..baada ya hapo JOPO huteua 3 FINALISTS ambao majina yao hupelekwa kwa RAIS ambaye atateua mkurugenzi mkuu wa Tpdc.

..Process niliyoieleza hapo juu huchukua muda mrefu at least miezi 6.

..Nilishangaa kusikia uteuzi wa DG wa Tpdc bila kuwa na taarifa kwamba nafasi hiyo iko wazi. Nafasi ya DG huwa wazi ikiwa aliyepo amemaliza mkataba wake na anataka ku-renew, au amemaliza mkataba na sheria haimruhusu ku-renew, au amefutwa kazi na Raisi.

Cc Kichuguu, Nguruvi3, Richard
 
Endelea kukaza hilo fuvu
 
Mkuu sasa ndio naelewa kwanini Marehemu alikuwa anawatukana watanzania wana mdomo na ujuwaji sana.
Tatizo jingine kila mtu anajiona yeye ndio anapaswa kuteuliwa, yaani akiteuliwa CDF wanapinga, akiteuliwa IGP wanapinga, uhamiaji, magereza, DC , RC , DED,

Unakuta mtu mmoja anataka ateuliwe yeye nafasi zote hizo.

Kaazi kweli kweli.
 
SSH, soma na soma na urudie tena kusoma ma file na hizo CV. Slow down kumwaga wino kutia sign. Jipe.muda epuka kuchukua maamuzi ya haraka.

Sikiliza sana. Ila pata muda wa kureflect na kuchambua unayoambiwa.

Believe in vetting and due process.
 
Kweli kabisa mkuu macho_mdiliko

Jana nilishangaa mno na sikuamini kama hilo ndo lilikua Chaguo mbadala la Mataragio pale TPDC hasa kwa nature na Shughuli za lile Shirika.

Aisee kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na strong institutions zilizojengwa na katiba kiliko hii ya kuegemea kwenye personalities za watu.
 
Dhaifu sana tena sana.. sijui 2025 tutafikaje
 
Hahaha huo wasifu wake uko wapi?

Mama anaingizwa mkenge na washauri wake. Inaonekana wana-take advantage ya upole wake.
Na waliingiza Hilo jina kusudi la mtu asiye qualify kwenye nafasi nyeti kusudi. Sasa mtu kasoma chuo Cha Yohana bachelor ya evening program, then kafanya uvccm, kah ilikuwa joke ya hatari
 
Kwenye vyeo vikubwa wawe wanaruhusu watu ku apply then wafanyiwe michakato uliyotaja ikiwezekana wapitishwe na bunge, bila hvo tutaendelea kupata watu wasio wazoefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…