Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Mnasemaga tuu hekma na busara, ukali unasaidia unapokuwa na watu wahuni na taasisi corrupt,angalia China,Japan,UAE ma Dubai ninani aliyanyanyua uone kalba zao ilikuwa busara tuu ama ukali ulinyoosha mambo!!
Hakuna nchi duniani iliyonyanyuliwa kiuchumi kwakasi na mwanamke!!

Ni ukweli ukali unasidia lakini sio jazba.
 
Mkuu kuishi na watu inahitaji nidhamu usimdharau MTU huwezi jua atakuja kua nani kwako, labda hawa walikua wanavimba sana enzi hizo yeye hana mamlaka ya kuwatengua kwahyo akawa amewania
ila usemacho nacho chaweza kuwa kweli,maana na sisi wabongo tuko vizuri kwenye dharau

Mimi napendekeza katiba irekebishwe Makamu wa Rais nae awe na nguvu,asiishie kuwa mtu wa kuzindua miradi
 
Tatizo kubwa la serikali ya Tanzania ni ushamba wakufanya siri mambo ambayo wakati mwingine ayahitaji kufichwa hasa investment ambazo bunge inabidi izifanyie appraisal kupitia mijadala.

Unaweza kupata habari kamili ya capital structure ya investment za serikali kupitia news article za nje kuliko kusikia mambo hayo kutoka kwenye mdomo wa kiongozi wa serikali au mijadala ya bungeni.

Matokeo yake wananchi wanaweza sifia investment leo baada ya muda unakuta masharti ya mkopo yanataka mjerumani aliekopesha kujenga kinyerezi I and II malipo yake ni 70% ya faida za mradi kwa miaka 20-30, mchina aliekopesha kujenga bomba la gas malipo yake ni 40-50% za thamani ya cubic feet zinazopita kila siku as a result badala ya TANESCO kupata Gas kwa bei nafuu inabidi wauziwe kwa bei ambayo ita cover deni la mchina kwenye bomba na TPDC kupata hela za kujiendesha; mwisho wa siku hakuna unafuu wa vile kwa mlaji kwenye bei ya umeme.

Kwa hivyo anapokuja raisi mwingine akakuta nini kiko nyuma ya plan zilizoachwa na mwenzake anaona isiwe shida amalizie iliyoanza. Ambazo bado ana abandon bora aende kivingine ambapo anadhani capital structure yake ina return kubwa zaidi kwa serikali baada ya mradi kuisha kuliko investment alizozikuta mezani.

However admin ya serikali ni ‘going concern’ na watu awajaajiriwa kwa sababu ya kusimamia miradi tu kuna kutumikia watu pia huko nako kunahitaji strategies na system za usimamizi ambazo zinachukua muda kuzoeleka. Makatibu wakuu na mawaziri ndio architects wa hizo projects.

Kwa ivyo kila mtu anapoingia na kubadili watu kwa asilimia kubwa unaondoa continuation, predictability ya ufanisi serikalini na inakuwa ngumu kwa wananchi kuelewa utendaji wa serikali na kubadili tabia zao pale inapobidi.

In other words hana sababu ya kubadili kila mtu isipokuwa maeneo ambayo kweli wasimamizi ni shida vinginevyo anaondoa ufanisi inakuwa shughuli ya kupiga hatua kumi mbele ukibadili unarudi hatua sita nyuma na kuanza kuitafuta kumi tena na kuipita ili usonge mbele.
 
Wengine ili waonekane tu wamekosoa, ngoja mama akasirike awe ka jiwe ili watie akili vzuri
This is what I have been saying all over.

Leo anawasikiliza eti tunaanza kumnanga, ngoja sasa awe hatuskilizi ndio tutatia akili
 
Umetaja wanawake wangapi katika population gani? Hata katika huo udhaifu wao si ajabu kupata 1 katika ke 800 na kwa hivyo huyo 1 hawezi kufuta udhaifu wao. La msingi tuombe sana Mungu ili huyu Mama awe wa tofauti na ke wengine walioko katika jamii yetu.
Wanawake wako wengi sana Tanzania na duniani kote. Lakini male chauvinists and rosemarie types will always be there.
 
Kwa maelezo haya marefu, ni ushahidi kuwa hakuna haja yoyote ya huyu mama kufuata hiyo road map ya Magufuli, maana hata yeye mambo yake yalikuwa ni siri. ifahamike kuwa Magufuli alikuwa anasema tunajenga miradi kwa fedha zetu za ndani, wakati huo huo deni la taifa limefikia 20t ndani ya 5yrs.
 
This is what I have been saying all over.

Leo anawasikiliza eti tunaanza kumnanga, ngoja sasa awe hatuskilizi ndio tutatia akili

Mkuu tutatiana akili. Jiwe si alikuwa kiburi, mbona huku mitandaoni kwenye bunge halisi la wananchi alitia akili, na kila akipanda jukwaani frustration za mitandaoni alikuwa haachi kuzianika?
 
TLS walitoa hoja wanayoiona ya kikatiba, kwanini umeona haya ni majibu stahiki kwa hoja yenye uzito huo. Sio lazima wote tuwe na opinion kwenye kila kitu, mara nyingine it's ok kukaa kimya ujifunze.
Mkuu ielewe comment yangu kwanza au "ielewe mitaa"

Hoja zangu ni mama anakuwa msikivu na tunamshkuru kwa hilo, ajabu ni mnapoanza kukosoa mambo ambayo wengine wala hamna weledi nayo.

Ndio tukasema sasa, akiwacha kuskiliza tusije tukaskia fyokofyoko na malalamiko.

Mama aachwe apige kazi.
 
Mkuu tutatiana akili. Jiwe si alikuwa kiburi, mbona huku mitandaoni kwenye bunge halisi la wananchi alitia akili, na kila akipanda jukwaani frustration za mitandaoni alikuwa haachi kuzianika?
Haya mkuu. Ila tukimaliza kutiana akili muda umekwenda, mtu kashastaafu na nyumba ya kifahari kashakabidhiwa.

Kwetu Sisi ya kukwama yashakwama!
 
This is what I have been saying all over.

Leo anawasikiliza eti tunaanza kumnanga, ngoja sasa awe hatuskilizi ndio tutatia akili
Mtu anafanyia maoni yetu na Yuko ku act quickly watu wabwabwaja hawana Jena ngoja aache kusikiliza Sasa watu watokwe mapovu had mate yawakauke yeye hachukui hatua ili wachoke kuchonga ka enzi za Jiwe. Dawa ya Moto ni Moto tu
 
Kuna wapemba wamemuweka wakiwa pamoja na yule mkwe wa mama samia. Yule anayesimamia TISS
Nia yao ni kupiga vitalu vya mafuta.

Yule jamaa wa sasa ni nyoko amewashika mapu** hawawezi kupiga.

Hata meko aliingizwa chaka ila akashtuka mapema na kumtudisha jamaa.
Exactly
 
Haya mkuu. Ila tukimaliza kutiana akili muda umekwenda, mtu kashastaafu na nyumba ya kifahari kashakabidhiwa.

Kwetu Sisi ya kukwama yashakwama!

Mkuu hiyo tofauti ya maisha ipo tu hata kwenye hizo nchi zilizoendelea. Hivyo hizo kelele zipo na zitakuwepo siku zote maana nature ndio ilivyo. Kwahiyo hayo mambo ya nyumba ya kifahari yasikupe tabu maana hatulali nje, japo hatuishi kwenye nyumba za kifahari.
 
Sawa mkuu.
 
Umri sio tatizo Jombaa. Je, ana uzoefu wa masuala ya mafuta na gesi mahala popote? Kama anao hebu tulete huo wasifu wa huyu mtu hapa.

Kumbuka moja ya sifa kuu ya uteuzi wa ukurugenzi mkuu wa mashirika ya umma ni uzoefu wa kiongozi ktk idara za utaalamu husika. Ukuu wa mashirika ya umma ni nafasi makini sana inahitaji mtu anayejua kazi husika kwa uweledi usio tia mashaka.

Nehemiah Mchechu aliteuliwa CEO wa CBA akiwa na miaka 36 kabla ya hapo alikuwa alternate director & head of global and wholesale banking wa standard chartered bank Tanzania technically alikuwa ana-manage 70% ya portifolio ya benki nzima. Uzoefu wake ulikuwa hauna mashaka.

Ian Ferrao aliteuliwa kuwa MD Vodacom Tanzania akiwa na miaka 30 kabla ya hapo alikuwa MD Vodacom Lesotho nyuma kidogo alikuwa mkurugenzi wa masoko Vodacom South Africa.

Unaona uzoefu wa hao watu uliowataja? Walipewa hizo kazi kwa sifa stahiki. Hata ukiwa na miaka 30 kama una uzoefu utapewa nafasi ila sio kiujanja ujanja kama huyo "mstaafu wa TPDC".
 
Umetema point mkuu...huyo mwesiga hana uzoefu wowote wa mafuta na gesi...
Mafuta taa tu sijui kama anauzoefu nayoo

Jamaa angetoboa humo kungetokea vituko
Hapo TPDC

Ova
 
Hapo uliposema hatukuwa na ujirani mwema na Kenya ndio umegusa. Ina maana kwa kauli ile ya raisi Kenyatta huo ugomvi unaosemwa ni nadharia tu za mitandaoni.

Pamoja na trade wars zetu za kila siku. Kenya wakiwa heavily dependants wa raw material za Tanzania mpaka kesho Raisi alielewa road map ya Magufuli kwa wakulima wa Tanzania na agenda zake za kulinda resources.

Mama should stick to the plan. Sio lazima atumie mbinu za mtangulizi wake kufikia malengo. Nonetheless she should follow what worked (don’t mend it, if it’s not broken) and that includes sticking by people who can deliver results and their performance is measurable.
Tatizo la biashara ya TZ na Kenya ni kuwa hii biashara haina maslahi kwa wakubwa kule Kenya. Kwa mfano, wnataka kuagiza mahindi toka nje. Hii kazi inafanywa na kampuni za vigogo. Wanaingiza mali mbovu na bila kulipa kodi. Mara utasikia mchele au mahindi toka nje yasiyokidhi kiwango yamrchomwa. Waagizaji wanalipwa kinyemela. Tatizo ukiagiza TZ au UG kazi wanafanya wafanya biashara wadogo na haina maslahi kwa wakukubwa. Ndiyo maana mara kuna corona kwenye magunia, mara sumu minyoo na vitu mbalimbali. Hivyo cvyote ni visingizio tu, ukweli ni kuwa wakubwa hawapati faida na biashara hii. Punde si puinde utasikia wameagiza mahindi toka India Brazil, au USA.
 
Ndio akili za mafisadi hizo duniani wote wanafanana tabia wao kwanza kwa gharama za wengi.

Kama awajaja na mkakati wa kujigemea visima vya mafuta kama ilivyotokea Russia, basi kwa kushirikiana watauwa mradi wa city trams wenye manufaa kwa wengi ilimradi wauze; magari, city buses and school buses. Yenyewe inataka watu wakajaze mafuta halafu we unataka kuwaletea hadithi za electric city tram; nani anunue magari na mafuta yao.

In short duniani kuna watu walizaliwa kudhulumu wengine and unfortunately most of those end up being filthy rich na baadae kutawala siasa za nchi zao kama sio za dunia.

Anyway nje ya hayo hoja yangu ilikuwa pamoja na tofauti zetu za mara kwa mara na Kenya raisi wao aliona good intentions za marehemu kwa watu wake. Mama hana sababu ya kubadili course of action.
 
Back
Top Bottom