Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Mkuu pitia mitandaoni hasa huko Twitter ambako tunadhani inawezekana wengi wao wana ufahamu ,maarifa na utashi wa kiwango kikubwa angalia hoja zao si kujenga nchi au kushauri huko wamejaa watu wenye Roho mbaya ,wivu, ubinafsi ,chuki ,Visasi na wenye kutamani nchii ianguke au ipate matatizo kwao ni furaha sasa kama ww unaweza chukua ushauri wa watu ambao 90% wanaongozwa na mawazo ya Kigogo ,Chalali,Fatma Karume, na yule mjaruo?

Bora hata hapa JF wapo watu ambao unaweza kuchukua hata ushauri kwao kuliko kule ambapo Nchi ikipata matatizo wanashangilia utadhani wao wapo Chicago USA
Twira kuna wajinga Yani kigogo akishasena kwao wanabeba hivo hivo bila kuchekecha mambo
 
Nilishtuka sana mwaka 2015 mwezi wa 12 nilipoona jina la Doto Mgosha James kuwa naibu katibu mkuu wizara ya fedha.

Alipanda kutoka kuwa Transport Economist TANROADS to deputy permanent secretary alipata uzoefu wa miezi sita kupanda kuwa katibu mkuu.

Nafasi ya katibu mkuu hazina ndio injinia mkuu ya uchumi wa nchi.
Nani nchi hi hajui kuwa huyo Ngosha Dotto James ni mtoto wa dadake na marehemu Jiwe....???
 
Akirudi kuwa ka jiwe asisikilize musilalamike tena
Tunalalamika nini wewe umekuja kuomba kazi tumekufanyia interview na umepita bhasi tunakuacha kufanye kazi yeye na JPM waliomba kazi ya kutuongoza miaka 5 mpk 2025 wakiwa na vision na mission yao kichwani kuwa watafanya hiki na kile bhasi wafanyie kazi mawazo yao tatizo kila mtanzania mwenye smartphone na akiwa na account Twitter anajiona mbobevu wa maswala ya kisiasa na kiuchumi
 
unajua kuna vitu vinafikirisha sana.

mtu aliezaliwa 1987 (japo sura yake anaonekana ni 1977,1978, 1979) anaweza kuwa mkurugenzi wa shirika kama tpdc?

modi msifute au kuunganisha.

nataka tuende kwa mifano ya hapa kwetu kama yapo mashirika yenye maDG ya mtu wa 1987 or above.


IMG-20210405-WA0008.jpg
 
TLS walitoa hoja wanayoiona ya kikatiba, kwanini umeona haya ni majibu stahiki kwa hoja yenye uzito huo. Sio lazima wote tuwe na opinion kwenye kila kitu, mara nyingine it's ok kukaa kimya ujifunze.
 
Huyu kadaganya umri ili apate fursa uvccm , ila hata elimu yake ya chuo Cha Mtakatifu Yohana ni ya kuunga unga
 
Hapo uliposema hatukuwa na ujirani mwema na Kenya ndio umegusa. Ina maana kwa kauli ile ya raisi Kenyatta huo ugomvi unaosemwa ni nadharia tu za mitandaoni.

Pamoja na trade wars zetu za kila siku. Kenya wakiwa heavily dependants wa raw material za Tanzania mpaka kesho Raisi alielewa road map ya Magufuli kwa wakulima wa Tanzania na agenda zake za kulinda resources.

Mama should stick to the plan. Sio lazima atumie mbinu za mtangulizi wake kufikia malengo. Nonetheless she should follow what worked (don’t mend it, if it’s not broken) and that includes sticking by people who can deliver results and their performance is measurable.

Ni nadharia za mitandaoni kwa mambo tunayoyaona kwa vitendo? Nimefuatilia hiyo road map yako ya Magufuli sioni ni ipi hasa ya kumtaka huyo Mama afuate.

Hatuna utaratibu wa marais wetu kwa mmoja kufuata mipango ya mwenzake, huwa naona kila mmoja akifuata anayoamini. Mfano mrahisi ni JK na Magufuli,wakati wa JK kulikuwa na mpango wa umeme wa Gas, na tuliimbishwa kama wendawazimu umeme wa gas ni muarobaini wa nishati hapa nchini, na wakati huo Magufuli alikuwa waziri kwenye serikali ya JK. Tuliambiwa umeme wa gas ukikamilika kwa 100% tutapata. 5,000mg+. Tukakopa 2t+ kwa mradi ule, na umeanza uzalishaji hapo kinyerezi. Ameingia Magufuli kaachana na umeme wa gas tulioimbishwa kama wendawazimu wa kuzalisha 5,000mg, kaanza mradi mpya wa umeme wa maji wa 2,115mg wa $3b+! Kwa mfano huo halisi, huyo mama afuate road map ya Magufuli ili iweje kwa mfano?
 
Kuna tatizo linakuja huko mbele. mama hteui mwenyewe, analetewa bila yeye mwenyewe kufabya scrutiny!

Je wanaweza wakampelekea file la kigogo20I4 wakati anayetakiwa ni kigogo2014 ?

Dawa ya hii kitu ni kupanga upya la sivyo watampanda mpaka kichwani
 
Mama ataendelea kuyumbishwa na kulishwa matango pori mpaka akome. Waliomzunguka wengi lengo ni kuprove kwamba hana uwezo ili huko mbele ya safari wamuengue kiaina
 
Huo umri unawezekana sana. Watu wanaongeza makampuni makubwa sana in their 20s kwanini 34 ashindwe?

Mwalimu aliongoza TANU akiwa kwenye age hizo, Mchechu aliongoza CBA Bank kama CEO akiwa na umri huo. Ian Ferrao CEO wa Vodacom aliyepita leo ndio ana 37 kwa hiyo aliongoza Vodacom akiwa na miaka hiyo hiyo. Kuna Dada ni Mkurugenzi wa Biashara hapo Vodacom anaitwa Linda Rows nae ana 33 kwa sasa. Mifano ni endless.

Ukuaji wa kikazi kwenye taasisi za Umma ni kikwazo. Unajali sana umri badala ya uzalishaji. Ndio maana huoni vijana kule juu. Ni mfumo wa kipuuzi.

Tatizo hapo si umri ni vigezo.
 
Back
Top Bottom