Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Mama aachane na mitandao afanye kazi taratibu. Lakini sasa anateua anakimbilia kuchungulia comment za raia. Ina maana alikua haoni kabisa alichokua anafanya mtangulizi wake?
 
Nilitarajia kitu kama hiki kutokea,mara baada tu ya kuwa nimeona CV ya mteule mpya. Kwa hiyo ni Mataragio tena kwa mara ya tatu sasa, na pengine hadi mpaka mwisho wa kipindi chote cha Mama, baada ya miaka kumi ijayo!
 
Yan ana turudisha miaka ishirin nyuma, mbelen hata kosa hela zakulipa mishaara, yeye hajui kama watu wamejipanga kuiba
 
Ni sahihi kutokufanya kila kitu mwenyewe. Hapa sasa kamati iliyoteua majina inaweza wajibishwa na udhaifu umeonekana haraka na kupigiwa kelele.

Angekuwa yeye ndo anafanya kila kitu makosa yake hayarekebishiki mpaka maafa maana maamuzi kayafanya mwenye nchi na ndo final.

Hili tatizo lilionekana sana kwa awamu iliyopita. Once raisi kafanya maamuzi hakuna wa kutengua maana yeye alishaamua na ndo raisi. Watu watanyamaza na wanafiki watasifia mpaka tatizo litokee.
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake. Hongera Rosemarie kwa kuthibitisha hilo.

Mwanamke kiumbe dhaifu peke yako usiejiamini usijumuishe wote.

Nikupe mfano tu: Ellen Johnson Sirleaf, Mwele Malecela, Msuya wa UNEP...
Acha hizo
 
Mama aachane na mitandao afanye kazi taratibu. Lakini sasa anateua anakimbilia kuchungulia comment za raia. Ina maana alikua haoni kabisa alichokua anafanya mtangulizi wake?
Hili nilisema mwanzo kabisa Ogopa sana mtu anayepost kitu mitandaoni kwa kutaka like na postive feedback hakuna kiongozi yeyote anayeshinda mitandaoni akafanikiwa atakuwa anaongoza kwa pressure tu kwani mitandao imejaa watu ambao ni wapingaji wa kila kitu hili kuwaridhisha inabidi uende vile wanavyotaka soon tutaanza kuongozwa na mawazo wa Kigogo na wenzie huko mitandaoni .
 
Mama kabla ya kuwaapisha hao wengine, yampasa sasa apitie upya yeye mwenyewe wasifu wa kila mmoja...
 
To be fair jamaa hana cv ya kumtosha kua pale.
 
Hakuna tatizo hapo so long alikuwa hajaapa, hizo zote ni mbinu za kupata watu sahihi kwa kupata public opinion, ameteua watu zaidi ya 40 lakini mmoja tu ndiyo kalalamikiwa objectively so uteuzi ni 98%correct.Piga kazi mama yetu
Fact
 
Asante mama kwa kutumbua hiyo kada ya ccm, ila Mh. Rais kuwa makini la sivyo wahafidhina wa ccm watakupoteza!Jiridhishe pia na yule mpwa wetu!
 
Mama Samia anajua anachokifanya na wala hakurupuki, mpeni muda muone matunda yake...naamini atakua the best president of africa.
Hiyo imani yako inatusaidiaje kwa mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…