Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Hii ni dalili ya wazi kabisa kuwa mama ni mwepesi sana wa kudanganywa

Huko tuendapo si pazuri kabisa TPDC ni shirika ambalo 100% linadeal na mabeberu waliokomaa kwenye sector ya mafuta na Gas. Anakwenda kumuweka kada wa UVCCM tena bila hata kuangalia CV yake hii ni hatari sana...

Kuna haja gani ya sasa hv kuanza kuteua na kutengua? amepata wapi muda wa kukaa na kujua huyu ni safi huyu si safi kwa siku hizi chache baada ya msiba? wakati serikalini yeye alikuwa msaidizi number 1 wa JPM ni sawa baba kafa hata matanga hayajaisha unaona mama anaanza kugawa mali na kufanya mabadiliko haraka haraka kwenye nyaraka .

Mama alikuwa msaidizi na mashauri number moja wa mzee kama kiapo chake kinavyosema anatamshauri Rais kwa hekima na hvyo tunapata kujua wote walioteuliwa bhasi kwa namna moja ameshiriki ktk uteuzi wake sasa inakuwaje tena hata siku 21 jazijapita anaanza kutengua na kuweka watu wengine amepata wapi muda wa kucheki vzr CV na amewafanyia vetting watu hao saa ngapi? Wkt msiba tumezika juzi tu ???ina maana wkt sisi tunalia na kujipanga mabarabarani yeye anapanga safu yake ?mmmh
 
Sasa unatarajia yeye atamfahamu kila mteuliwa katika kipindi hichi kifupi? Lazima ategemee wasaidizi wake kumpa taarifa. Hata hao marais waliopita hawakuwafahamu wote kwa mara moja.

Mbona JPM alitengua uteuzi wa yule Naibu Waziri aliposhindwa kuapa?

Naona expectations zenu zimezidi mipaka tena.
anakimbilia wapi?kwa nini asijipe muda?
 
huyu mama ana matatizo,kwanza nilihisi kitu siku ile katibu mkuu kiongozi anaapishwa,huyu mama alisema aliletewa jina na alikuwa hamfahamu??????huyu mama atatupeleka pabaya sana,mwanamke ni kiumbe dhaifu na nchi yetu hatupo tayari kwa sasa hivi kuongozwa na viumbe dhaifu,angemuuliza boss wake magu kwa nini alikaa miezi mitatu bila kuteua alikuwa na maana gani----
Acha kumwita dhaifu kisa teuzi aisee, eti hauko tayari, kweli jamii yetu ina Perception mbaya kwa wanawake mbona hata magufuli aliingia Chaka na kurekebisha. Makosa ni sehemu ya ubinadamu ndio maana yanarekebishika
 
Yes na vile wahuni walichomekeza sioni Cha kumlaumu wanataka raisi ndo awe anapitia majina wakati Wana work as a team
Rais anasaini hivyo licha ya kupitia kama timu yeye pia lazima ajiridhishe, wakiboronga sio mzigo wa hiyo timu bali ni zigo lake.
 
Well said my friend Lord denning 😍😍
Kitengo cha vetting kina watu wanataka kumhadaa na kuhujumu juhudi za Rais SSH

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Rest well our hero President John Pombe Magufuli
Hapo kwa John Pombe Magufuli, he is not our hero, he is your hero!

Embu acha ukorofi mama D tujikite kwenye mada😎
 
JF walikoosea sana kuunganisha ule uzi kwani hili lilikuwa ni jambo sensitive sana la kujadiliwa kwenye uzi wa kujitegemea
Huo ndio ujinga wa mods kwamba kukiwa na madamoto kisha ikaanzishwa madanyingine inayochambua kwakina mada ya awali kazi yao kuunganisha tu
 
Hii kwangu inatosha kusema hatuna Rais hapa,ni mfano wa rais tu. Unawezaje kuteua mtu wa shirika nyeti kama lile bila kufanya vetting ambayo hata mteuzi mwenyewe lazima asome ripoti na cv pembeni.
Wewe hujawahi kuingia Chaka mahali?
 
Kwanini Rais anateua mtu ambaye hamjui vizuri na hana cv zake mezani? washauri wa Rais kwenye mambo ya uteuzi ni akina nani!?
wakati mwingine Rais mpya anapoingia ofisini asipokwa makini hapo ndipo watu huweka watu wao nia kwa kulinda maslahi yao hadi azoee atakuwa kaishaingizwa chaka vingi sana maana kwa sasa chanzo cha taarifa ni wale walio mzunguka tu(persuasion&manipulation at work)
 
👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍💚💚💚💚💛💛💛🔰🔰🔰🔰🔰🔰🙏🙏🙏🙏🙏

Mama Samia shikamooooo, shikamoooooo, Rais wangu, shikamooooo mamaaa..!!!
 
Nashauri uapisho uahirishwe kwanza mpaka ajiridhishe, kwa Kila mtu aliyemteua kwa nafasi zote, je huyo mtu ana sifa za kuwa hapo. Mwingine anaweza kuwa na sifa nzuri sana, lakini kwa nafasi aliyepo hafit vizuri, unampangia upande mwingine anakofit zaidi. Mtazamo tu
 
Back
Top Bottom