Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Rais ana nafasi nyingi sana za uteuzi.Ambao anaweza kuwafahamu ni wachache sana. Ndio maana iko haja kubwa ya kuwa na mfumo mpya wa kupata viongozi. Rais abaki kuteua mawaziri,mabalozi na wakuu wa vyombo vya usalama.
Kwanini Rais anateua mtu ambaye hamjui vizuri na hana cv zake mezani? washauri wa Rais kwenye mambo ya uteuzi ni akina nani!?
 
Rais anafanya kazi na watu, anaweza kupokea na kudai taarifa muhimu kabla ya kufanya maamuzi ila hapa naona kabisa Kuna watu wanaenda kuwajibishwa na kutenguliwa kwa hili

Mimi nimeona Rais Samia Suluhu Hassan yuko makini kwa kufanya utenguzi huu mara moja
Kwa hiyo alivyoletewa tu akamwaga wino bila kijiridhisha hadi wanajamii forums wamepiga kelele ndo kastuka!?
 
Rais anafanya kazi na watu, anaweza kupokea na kudai taarifa muhimu kabla ya kufanya maamuzi ila hapa naona kabisa Kuna watu wanaenda kuwajibishwa na kutenguliwa kwa hili

Mimi nimeona Rais Samia Suluhu Hassan yuko makini kwa kufanya utenguzi huu mara moja
Anatakiwa awatengue fasta hao watu tena aiweke public kuwa katwngua watu fulani kwa kumpotosha ili wanaokuja chukuabhiyo nafasi wajue wanapewa kazi gani...
Ni watu gani hawa by the way?
 
hapa sawa kabisa. N vetting was done. Ni kuteua kwa ushauri wa CCM, bado remnants za jiwe zinatake influence

duuh ushakuwa mtoto

Mataragio ni wa nani??

ashakufa japo alikuumiza, pole sana

He is gone, pambana na hali yako na familia yako


Hakuna jipya, kama alikata mirija ishaondoka pia,
 
Huu ni uamuzi sahihi kufanywa katika wakati sahihi na Mhe. Rais.

Angalizo kwa Mhe Rais, awe makini sana na washauri wake hasa timu yake ya washauri na avunje kabisa kitengo cha VETTING TISS na kukiunda upya.

Hii ilikuwa ni aibu kwa Taifa. Yaani unamtoa Christiano Ronaldo unamuingiza Sapong????

Hongera Mama Samia kwa kuchukua hatua za haraka!
View attachment 1743826

Zaidi soma:

Rais Magufuli aiagiza Wizara ya Nishati kumrejesha kazini mara moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dkt. James Mataragio
 
huyu mama ana matatizo,kwanza nilihisi kitu siku ile katibu mkuu kiongozi anaapishwa,huyu mama alisema aliletewa jina na alikuwa hamfahamu??????huyu mama atatupeleka pabaya sana,mwanamke ni kiumbe dhaifu na nchi yetu hatupo tayari kwa sasa hivi kuongozwa na viumbe dhaifu,angemuuliza boss wake magu kwa nini alikaa miezi mitatu bila kuteua alikuwa na maana gani----

Dah😐😐😐 hoja yako ni dhaifu kuliko udhaifu wenyewe
 
Back
Top Bottom