Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe? yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe?

Inashangaza sana.
Ripoti kaandikiwa yeye.
Kwenye ripoti maafisa masuhuli / makatibu wakuu,ma ras. Na ceos wengi ndio wanatajwa kuboronga.
Mama unatakiwa uanze na hao makatibu wakuu , hapo ni sawa na kesi ya nyani unampa ngedere
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.
Katibu mkuu/mtendaji mkuu wa taasisi,idara na wakala wa serikali ndio maafisa masuuli na ndio wajibu hoja wakuu wa taarifa ya CAG
 
Safi sana mh.rais hii ndio watanzania wengi walikuwa wanaisubili kwa hamu na nina imani wezi wote watafikishwa mahakamani,pia tunahitaji katiba mpya itayoweka bayana kuwa mwizi wa mali za umma atashughulikiwa vilivyo.
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.
Katika serikali makatibu wakuu ndio watendaji wakuu wa wizara, in short mawazir wao ni walezi au wasimamizi lakin sio wataalam kitaaluma katika wizara zao, mikataba yote kabla haijasainiwa na wizara husik lazm ipite kwanza, kwanza kwanza kwa hao makatibu wakuu, , hivo wawajibishwe kwanza na kama kuna namn walishirikiana na mawaziri wao bhas nao pia watafata
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

View attachment 2582469
Ni hatua ya kutia moyo.

CORRUPT COUNTRY NEVER DEVELOP!
 
Mbuzi wa Kafala wamechacha . Ametafutwa sungura wa kafala Haaa.

Akina Mashimba Ndaki mbuzi wa kafala, Kabudi mbuzi wa Kafala, Lukuvi mbuzi wa kafala. Haaa.
January Makamba Mbuzi wa kufugwa hawezi chinjwa, Makame Mbarawa mbuzi wa kufugwa UDIhaitaiweje hawezi kuchinjwa, Napee je Vp kuhusu Ummy Mwalimu,

je kuna inawezekana MKRISTO akawa mbuzi wa kufugwa? haaa, et nani......... mataje
Ni mjinga tu anaewaza mambo kwa mgongo wa UDINI...
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.

Tulishawaambia kuwa alikuwa anabweka tu kuwaita watu "STUPID" kwani hana ubavu wa kuwachukulia hatua stahiki!! Kuna fedha chungu nzima zimeibwa kwenye malipo ya bwawa la Nyerere lakini mama yuko kimyaa kwasababu ya mbuzi wake wa kufugwa!! Hizo hizo fedha ndio wamenunulia nyumba huko DUBAI lakini TISS wamefumba macho.
 
Wale ndugu almaarufu "stupid people" mambo iko huku:

mil.jpg

Kwa aliyetajwa na CAG sasa ni suala la muda tu.

Aungurumapo simba mcheza nani?
 
Back
Top Bottom