Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Kachemka wakati akiwa na mamlaka kamili ya kuwajibisha ila kawapa wakajikague na kujitolea hukumu.

Ukiona rais anakwepa majukumu yake basi waziri wa fedha alikuwa sahihi kutoa ile kauli kule bungeni.

Wana buy time, wameona mijadala imepamba moto, kwaiyo njia ya kupunguza mijadala ndio huo aliokuja nao.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

View attachment 2582469
 
Daaah kuna maamzi yanafanyika unajiuliza hivi kweli kuna kiongozi wa nchi hii?
Yaani honestly hapa report ya TAKUKURU ukiisikia ni ujinga ujinga tu lakini bado kiongozi anaisifia!
Inasikitisha sana,labda hawa viongozi wetu,tuna wa-overrate sana,ukute upeo wao baadhi yao ni mdogo.
Waache ujinga,hawajitolei kufanya kazi,tunawalipa kwa kodi zetu.
 
Kachemka wakati akiwa na mamlaka kamili ya kuwajibisha ila kawapa wakajikague na kujitolea hukumu.

Ukiona rais anakwepa majukumu yake basi waziri wa fedha alikuwa sahihi kutoa ile kauli kule bungeni.

Wana buy time, wameona mijadala imepamba moto, kwaiyo njia ya kupunguza mijadala ndio huo aliokuja nao.
Nchi hii ni kichwa cha mwenda wa zimu! Mtuhumiwa wa wizi ajichunguze na kujipa adhabu!
 
Wana buy time, wameona mijadala imepamba moto, kwaiyo njia ya kupunguza mijadala ndio huo aliokuja nao.
Hapa si ndiyo wamevuruga kabisa.!!!
===
Wanunue muda kwa staili ya Zumalidi na Simba Bob!
 
Waungwana,
Naomba mwenye taarifa nzima ya CAG aliyoitoa kwa kiswahili mara baada ya kuwasilisha Bungeni.
 
Nchi inachekesha sana
Kwa hayo Madudu ilipaswa kwamza Mawaziri Mbarawa, Mwigulu, January,Nape,Ummy na Diblo Dibala wapigwe chini maana ndiyo wasimazi Wakuu wa sera bila kuwasahau Makatibu Wakuu wao.Sasa kuvunja Bodi ya Shirika kunasaidia nini?inamaana Wizara zao hazihusiki?
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri? Kama yupo serious angetakiwa kuwaita mawaziri awaulize, wakati huo wizi ukitokea kwenye wizara zao walikuwa wapi? asiporidhishwa na majibu fukuza.

Haiingii akilini, hawa ambao inawezekana wameshirikiana kwenye wizi, unaagiza wachunguzane, huku ni kudanganyana tu, ndio maana kuna wakati Rais nae anatiliwa shaka.

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, kuhangaika na dagaa huku mapapa wapo tu ofisini, mimi sioni jipya, kapanua magoli tu hao jamaa wapate visingizio.

kama nimeelewa vibaya utanisahihisha
Ina Maana Makatibu wakuu+Wakurugenzi waisome report na kuifanyia kazi!
Ina Maana Kama kuna Makosa/Mapungufu ambayo yanefanya say na Afisa A,Au Meneja fulani,Afisa fulani,Mkuu wa Idara,Mhasibu,Engineer,Afisa ugavi,Mwanasheria,nk nk
hao wakuu waliotajwa wamepewa Rungu wamuwajibishe!
Kwani Kuna Makosa hapo?
Nisahihishe kama Nitakuwa nimekosea kiutendaji!(Protocol)
Instead ya Kuwawajibisha Mawaziri/Makatibu wakuu au wakurugenzi.
Wewe Una mawazo gani na Kwa nini?
 
Kwa hayo Madudu ilipaswa kwamza Mawaziri Mbarawa, Mwigulu, January,Nape,Ummy na Diblo Dibala wapigwe chini maana ndiyo wasimazi Wakuu wa sera bila kuwasahau Makatibu Wakuu wao.Sasa kuvunja Bodi ya Shirika kunasaidia nini?inamaana Wizara zao hazihusiki?
Kwa uhalisia ni kama twachezewa tusahau
 
Mkuu hiyo nayo ni hatua pia huwezi.mchukulia mtu hatua bila kuwa n evidences za kutosha. Tukae tusubiri makatibu wakuu ni wataalam kwenye wizara zao so wao wanajua vizuri zaidi kuliko raisi
Kwaiyo anawaagiza Makatibu Wakuu gani,kwani wao hawahusiki na huo uwizi?
 
kama nimeelewa vibaya utanisahihisha
Ina Maana Makatibu wakuu+Wakurugenzi waisome report na kuifanyia kazi!
Ina Maana Kama kuna Makosa/Mapungufu ambayo yanefanya say na Afisa A,Au Meneja fulani,Afisa fulani,Mkuu wa Idara,Mhasibu,Engineer,Afisa ugavi,Mwanasheria,nk nk
hao wakuu waliotajwa wamepewa Rungu wamuwajibishe!
Kwani Kuna Makosa hapo?
Nisahihishe kama Nitakuwa nimekosea kiutendaji!(Protocol)
Instead ya Kuwawajibisha Mawaziri/Makatibu wakuu au wakurugenzi.
Wewe Una mawazo gani na Kwa nini?
Kwa mazingira yaliyopo hao waliotajwa kuisoma report na kuchukua hatua kwa wabadhirifu wengi wao ni wahusika! ndo maana kuna matukio polisi hawezi kujichunguza inaundwa tume!
Huyu mama Kashindwa hata kuielekeza TAJUKURU na taasisi yake ya Urais kulifanyia kazi?
 
Huu usanii Mkuu,hamna kitu hapo,wanatuhadaa!
Nikwambie tu nchi hii kwa sasa haina Rais kuna mtu tu tunamwita Rais lakini kwa anayoshauriwa na kushindwa kupembua pumba na mchele matokea ndo haya tunayoyaona kwenye barua ya Ikulu!!
 
Tangu ripoti ya CAG ilivyo toka na Rais

kuonyeaha kukerwa ilitakiwa tuone baadhi ya

Viongozi wakijiuzulu lakini wapi wamejilausha

kama vile sio wao!!!!

Wanasubiri hadi wafukuzwe
Wakati wa Magufuli nani alichukuliwa hatua? Kuna ripoti safi imewahi kutoka nchi hii?
 
Hallo hapo kidogo samia umeonesha umuimu wa CAG mana aiwezekani sasa mireport inatoka kila leo watu wanakula kodi za wananchi kuanzia wao wakaguzi wanalipwa pesa kufanya ukaguzi pia na wale wanaokaguliwa pia nao ukaguzi waonesha wanapiga pesa alafu hyo output ya ukaguzi isifanyiwe kazi hapo wa tz tulikua tunakuona na wewe raisi ni mwizi tu
Hi ofisi ilishaanza kudharaulika
 
Safi sana mh.rais hii ndio watanzania wengi walikuwa wanaisubili kwa hamu na nina imani wezi wote watafikishwa mahakamani,pia tunahitaji katiba mpya itayoweka bayana kuwa mwizi wa mali za umma atashughulikiwa vilivyo.
Ni kweli kama mama anasitasita jibu ni Katiba mpya tu kila mtu atawajibika kivyake.
 
Back
Top Bottom