Rais Samia awaapisha Wakuu wa Mikoa. Afanya mabadiliko madogo, Kafulila apelekwa Simiyu, Mongella aletwa Arusha

To me Magu was the best president ever....
afanye mambo kama Magu na pengine awe mkali zaidi yake.....
ili watu wanyooke

Hata mimi natamani tu mama awe mkali, awe na misimamo yake kama kiongozi, unajua mpaka sasa hivi hatumuelewi Mama ni mtu wa aina gani, ni kama anajificha hivi makucha, juzi alisema yeye na magu ni kitu kimoja, ila matendo yake ni vitu viwili tofauti, Mama haeleweki, mama haaminiki... magu was very strict man , alikua hapindishi maneno wala kuyumba hovyo, akisema amesema, au kwa kuwa mama ni jinsia nyingine Ndio maana she is so kind? Sitaki kuamini hivyo
 
Hapana!

Mimi naomba ijirudie tena iwe mara mbili zaidi ili kuwakomesha mataga na sukuma gang

Mkuu ile kitu haichagui, maana mateso ni kwetu sote.

Gharama za business na maisha zinabadilika sana hali ya umeme ikiwa tete mkuu.

Hili la umeme naomba maza akopi kwa Magu aisee.
 
Wewe pia ni kiongozi nyumbani kwako,yako mengi unakosea,na kuyabadilisha

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Kwenu wadau wa JF.

Leo rais wa SSH amewaapisha wakuu wapya wa mikoa pamoja na viongozi wengine. Kama ilivyo ada viongozi wakuu waliohudhuria walipata nafasi ya kutuma salamu kwa viongozi hao

Mbele ya mh Wetu mpenda Mama Samia Suruhu alie beba matumaini yetu makubwa .Hivo taifa leo lili tegemea Rais atasema jambo lolote (tunavutiwa na kauli za rais kama jana alipo kitaka jeshi la polisi usalama barabarani kuacha kubambikia makosa) la kimatumaini hasa kwetu sisi wananchi,

mbele ya viongozi hao wapya,Shahuku ilikua ni kubwa sana leo kwetu wananchi kumsikiliza Mh wetu lakini gafla shauku io iliondoka.
Tunaimani na mama.

kazi iendelee mama sisi hatutachoka na hotuba zako.
 
Pongezi nyingi sana kwa Mhe. Rais kwa kuendelea kuisuka Serikali yetu.

sasa tuchape kazi.

tunawaomba wakuu wa mikoa wachape kazi, watekeleze maagizo na wafuatile miradi ktk mikoa yao.

kipekee Mkoa au JiJi la DSM amosi makala afuatilie sana miradi iliyopo ktk wilaya zote za JiJi haswa ktk wilaya ya Ubungo

Mhe. Makala ni mfuatiliaji mzuri sana tena sana sasa DSm imepata mtu sahihi
 
Wanaccm watakuwa wamemng'ata sikio! Huyu mtu wa kuja huyu atapewaje mkoa mzuri kama Arachuga halafu mwenyeji na mwaminifu kwa chama wa miaka yote atupwe Simiyu? Hii ingeleta manung'uniko kwenye Chama! Kafulila ni nani huko Ccm mpaka apewe nafasi kubwa hivyo at the expense ya wafia chama!
 
Acha Mongella aende Arusha maana qna uzoefu sana...Tangu DC na RC ....Kafulila acha akahifunze Simiyu.....Kila la kheri
 
Je na Kunenge aliyekuwa jiji kuu la Darisalama na kupelekwa Pwani? au Pwani nayo imekuwa jiji? nashindwa kuelewa hizi sababu ,kwa hiyo kama mkuu wa mkoa alikuwa kwenye mkoa ambao ni jiji akihamishwa anaenda mkoa ambao ni jiji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…