Rais Samia awainua Mbowe na Lipumba kwenye baraza la Eid, amsifia Mbowe kupendeza kwa kanzu

Rais Samia awainua Mbowe na Lipumba kwenye baraza la Eid, amsifia Mbowe kupendeza kwa kanzu

Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitri katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonesha na kuyaishi maono yake ya kuwa na Tanzania moja isiyogawanywa kwa misingi ya kisiasa

Kabla ya kuanza kuzungumza Rais Samia aliwapa nafasi wawakilishi wa vyama vya siasa waliopo kuzungumza ambapo kwanza alimakaribisha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kisha Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba

Baada ya kumaliza kuzungumza Rais Samia akaweka utani kidogo kuwa Mbowe anapendeza sana na vazi la Kanzu, hakika hii ndio Tanzania tunayoitaka ya kuishi, kula, kucheka na hata kutaniana pamoja bila kujali utofauti wa vyama vya siasa

Eid Mubaraq
View attachment 2596431
Idd ul MUBARRAK ustadh ABOUBAKAR MBOWE[emoji1488]

#SiempreJMT
#MamaKaja
 
Tuwe kwenye vyama tofauti, dini tofauti, makabila tofauti, maeneo tofauti, UKWELI HAUBADILIKI, sisi sote tu wanadamu tulio sawa. Na kama Mungu wetu angetaka watu wa imani fulani wasiwepo, watu wa kabila fulani wasiwepo, watu wa chama fulani wasiwepo, asingeshindwa kuhakikisha hawapo.

Maadam tupo, basi Mungu ametutaka sisi sote tuwepo. Kubaguana, kuchukiana na kuendeana uovu ni ujinga wetu ulio kinyume na mpango wa Mungu.

Heri yao wanaoishi kwa kadiri ya mpango wa Mungu ambao, ni kuwa wamoja kama alivyo Mwana, Roho na Mungu Baba; kuwa na upendo kama Mungu wetu alivyoupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kusiwepo na atakayepotea.
Hakika
 
Why wewe usilete upinzani huo unaousema?,why umtegemee Mr. Mbowe akupiganie wewe?,acha uoga wa kizuzu pigana mwenyewe kudai haki yako kama unaona unaonewa
Kila mapambano Kuna kiongozi..hii Ni kanuni toka enzi za kale..
Lakini nakubaliana na wewe kwenye Jambo moja..Mbowe kapambana Sana..tumuache nae apumzike..tumuache apate kifuta jasho kutoka kwa madame president..
 
Mbowe amejitoa sana sadaka kwa Taifa hili.

Alipoharibifu shamba lake kama adhabu kwa kuwatetea watanzania, wewe ulifanya nini?

Mbowe alipowekwa mahabusu mara kadhaa kwa sababu ya kutetea haki za watanzania, wewe ulifanya nini?

Mbowe alipobambikiwa kodi kwenye biashara zake, na kisha kufungiwa bank accounts zake kwa vile tu anawapigania watanzania, wewe ulifanya nini?

Kama unadhani kazi aliyoifanya Mbowe ni nyepesi, jaribu, halafu upitie japo 10% ya yale aliyopitia, ndiyo utajua uzito wa kazi aliyoifanya.

Wapo watu waliowahi kujitoa sana nchi hii, lakini bahati mbaya walijitoa kwaajili ya watu wasiojielewa, na hivyo kufanya jitihada zao zote kuonekana si kitu.
Nakubali Mbowe aliteseka Sana.. lakini unafikiri Mbowe ameteseka kuliko Mandela madiba..?
Mbowe amekata tamaa mapema Sana..lakini tumuache apate kifuta jasho..
Tukubali tunaelekea kwenye siasa za kipuuzi Sana..yaani wapinzani wanazidiwa hata Mpina wa ccm anakomaa na kina Mwigulu.. lakini wapinzani wanapishana Ikulu kula futali !
 
Namshauri Mbowe aachane na hizi siasa za kujikomba maana anapoteza haiba ya CDM. Hii approach ya Mbowe inaifaidisha zaidi CCM kuliko CDM.
Mbowe kapoteza pambano kirahisi Sana..kawa mtu wa kwenda Ikulu kula futali..
 
Kwa kweli Kama mwana CDM Sina imani na Mbowe kabisa. Anajichoresha Sana kwa CCM. Ataje siku ya kuondoka madarakani kabisa. Mbowe must go, mbowe
 
Nakubali Mbowe aliteseka Sana.. lakini unafikiri Mbowe ameteseka kuliko Mandela madiba..?
Mbowe amekata tamaa mapema Sana..lakini tumuache apate kifuta jasho..
Tukubali tunaelekea kwenye siasa za kipuuzi Sana..yaani wapinzani wanazidiwa hata Mpina wa ccm anakomaa na kina Mwigulu.. lakini wapinzani wanapishana Ikulu kula futali !
Mandela alikuwa na watu walioleta shinikizo! Mbowe kapoteza Kila kitu na mwisho watu wakamkimbia.
Tatizo lipo kwa wabongo!
Wapole wapole na hawawezi kusimamia haki zao!!
 
C
Kwa kweli Kama mwana CDM Sina imani na Mbowe kabisa. Anajichoresha Sana kwa CCM. Ataje siku ya kuondoka madarakani kabisa. Mbowe must go, mbowe
Ccm mnahangaikaaaa..ccm mpende mdipende mbowe bado yupo sana, mpaka ukombozi upatikane.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Mbowe na mwenzake Prof. Lipumba wa CUF wamekutanishwa na Baraza la Eid na kusahau yaliyopita ili wagange yajayo.

Siku za karibuni Prof. Lipumba amekuwa akiiponda sana CHADEMA lakini leo wameanza ukurasa mpya.

Ishukuriwe BAKWATA.
 
Back
Top Bottom