Rais Samia awainua Mbowe na Lipumba kwenye baraza la Eid, amsifia Mbowe kupendeza kwa kanzu

Rais Samia awainua Mbowe na Lipumba kwenye baraza la Eid, amsifia Mbowe kupendeza kwa kanzu

Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitri katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonesha na kuyaishi maono yake ya kuwa na Tanzania moja isiyogawanywa kwa misingi ya kisiasa

Kabla ya kuanza kuzungumza Rais Samia aliwapa nafasi wawakilishi wa vyama vya siasa waliopo kuzungumza ambapo kwanza alimakaribisha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kisha Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba

Baada ya kumaliza kuzungumza Rais Samia akaweka utani kidogo kuwa Mbowe anapendeza sana na vazi la Kanzu, hakika hii ndio Tanzania tunayoitaka ya kuishi, kula, kucheka na hata kutaniana pamoja bila kujali utofauti wa vyama vya siasa

Eid Mubaraq
View attachment 2596431
Sukuma Gang wanaumia saaaana
 
Back
Top Bottom