Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Sitetei wizi wa mali za Umma la hasha!

Lakini wacha nikuulize Mpendwa ;

Kwani wakati ule hakukuwa na wizi?

Kumbe sababu ya kumsakama CAG ilikuwa ni nini?
Wewe unamuonaje CAG wa sasa.
 
Huyu ni ndumilakuwili,mbona aku step down

Tuseme tu ukweli umejaribu kwenda kwenye taasisi za serikali ukaona huduma zao zikoje ukifananisha na simba wa chato huduma ilikuaje.
Huduma kwa sasa ni mbovu , lakini ndo hiyo nidhamu ya uwoga . Watumishi wali comply kwa kumuogopa mr tumbua tumbua.
Katika maisha ogopa sana kuishi maisha ya wewe kuogopwa , utazungukwa na watu wanafiki kupitiliza na watafurahia anguko lako muda wowote.
Hata kwenye familia zetu , nyumba zenye wazazi wakali mara nyingi ndo huzalisha machangudoa na mateja
 
Japo mwendazake alikuwa na changamoto zake, mama angeacha the bygones be gone akapambana kutengeneza legacy yake....maana sisi binadamu wachambuzi kila leo tuna jambo letu...
 
Magufuli hajawahi na hawezi kuwa Simba wa Yuda. Ni kauli ya dhihaka sana kwa Dini ya Kikristo. Sababu kwa imani yao wao wanaamini Yesu ndiye Simba wa Yuda.

So Magufuli ni Yesu? Hii ni dhihaka kwa Wakristo ambayo sidhani kama Rais anapaswa kuwa nayo. Sometimes muwe mnawapa Elimu hawa viongozi wasiwe wanaropoka maneno ya kuudhi.

Kama ilivyokuwa kwa Job Ndugai naye aliongea kauli ya kukwaza sana enzi zake. Hizi ni kauli za kuanza kuporomoka kisiasa. Wote waliojidai kudhihaki au kikebehi dini za wengine mwisho wake Mungu alipoingilia walipata thawabu yao.

Najua huu uzi JF watautoa. Ila watu kadhaa watakuwa wamepata ujumbe. Maana JF ya sasa inategemeana na umemsema nani. Kuna watu hawatakiwi kuguswa.
 
Sidhani kama angekuwa anajua Simba wa Yuda ni nani kwa Wakristo angesema hivyo.
 
Wakristu wamedhihakiwa kivipi?Mbona unawawekea watu maneno midomoni?Aliyedhihakiwa ni aliyetajwa.Usigombanishe watu.
 
HUYU MAMA MBONA KAMA ANALETA UDINI NA UBAGUZI??? HUYU MAMA TUSIPOKAA SAWA ATALIACHA TAIFA KATIKA HALI MBAYA MNOOOO
 
Ni bora hiyo nidham ya woga iliyokuwa ikifanya kazi. Ukweli sasa hali ni mbaya kwenye mashirika ya uma, watu hawafanyi kazi, hakuna wanayemuogopa, mwendo ni wizi kwa kwenda mbele. Inasikitisha sana, kuna shirika flani watu wamefikia hatua wanatoa vitu nje wanampa mtu anawauzia tena.
 
Watu wanatafsiri vibaya sana ile kauli. Mbona iko sawa yeye alikuwa makamu wa Rais alikuwa anawaona watumishi walivyokuwa waoga badala ya kuwa na ufanisi. Uoga huondoa ufanisi na hufinya madhaifu ambayo yalipaswa kusemwa na kurekebishwa.
Tulifikia hatu ya kufunga akaunti za watu hovyo, yaani hata deni la Laki 5 mtu anafungiwa akaunti yake. Haikuwa nidhamu bali ulikuwa uoga.
 
kwakweli unafki hauna dawa, si tungeambiwa wakati ule ule ili wajue namna ya kupata suluhu. Kusema kwa sasa wakati nawe ulikuwa sehemu inaonyesha ni kujaribu kuchafua wengine ili uonekane wewe upo sahihi... hatuelewi kwakweli
 
Huyu ni ndumilakuwili,mbona aku step down

Tuseme tu ukweli umejaribu kwenda kwenye taasisi za serikali ukaona huduma zao zikoje ukifananisha na simba wa chato huduma ilikuaje.
kwani hukusikia alitaka ku-step down?
 
Hata iweje hakutakiwa kumuongelea kihivi, kwa sababu Wananchi wengi akili zimefunguka kupitia awamu ya 5. Inashangaza ila inasikitisha sana kiongozi wetu kumtamka aliyekuwa yeye msaidizi. Wanafikiri watanzania ni wale wa kabla ya JPM

Duh!!!
 
Who cares kama kuna nidhamu ?

Heri Nusu Shari kuliko Shari kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…