Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Ila Samia hapaswi kumsema vibaya hata kama walipishana'
Mkuu mama Samia ndiye mwenye mpini sasa hivi na alikuwa msaidizi wake hivyo wacha atupatie madhaifu ya mtangilizi wake.
 
Mama anachemka sana, anaropoka ropoka tu. Hivi kweli Mwafrika yupi mwenye nidhamu ya kutoka moyoni kama siyo uoga? Kazi ya sheria ni ipi kama siyo kuwafanya watu waogope kutenda makosa wakijua sheria itawahukumu? Tumepata Rais boya kabisa na asubiri hiyo nidhamu ya kutoka moyoni ya watumishi wa umma kama ataiona
Wacha tuujue udhaifu wa jiwe kama mbwai wacha iwe mbwaaiiii
 
At the end of the day, huyu mama alikuwa anafanya kazi na Meko so anajua kila kitu kuhusu ukweli wa mambo yalivyokuwa, soon tutajua aliyewaua akina Azory na Ben Saanane.

Mama hataki kubeba dhambi za mtu, kila mtu auchukue mzigo wake mwenyewe na atoe habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Ila Meko alijua kuwafool wajinga wajinga yani dah , he was such a jerk.
Hakika Mungu hamfichi mnafiki
 
Mama kakata tamaa ya kura za kanda ya ziwa iwapo akigombea 2025!!Labda kama hatogombea na anajua hatogombea!!!
 
Kwa kweli tukisema muacheni Mh Hayati Magufuli apumzike mahali aliko tunashambuliwa eti sisi ni sukuma geg! Jaman marehemu kwa heshima za Afrika huwa tunamwacha apumzike aliko kuliko kumsemea vibaya vibaya.

Leo nimesikia Mh Raisi akisema utawala wa awamu ya Tano ulitengeneza nidhamu ya uwoga kwa watumishi, kwa sababu ulikuwa ni Simba, alikuwa ukizingua anakungata ngwadu!

Sasa kwa Nini ustekeleze unavyotaka. Paspo kumsem mwenda zake?
Kwa nini hamtaki kusikia ukweli??
 
Ni heshima hiyohiyo ya uoga ndiyo inamfanya hata CAG aatamie madudu ya awamu hii.

Muda ukifika na yeye atanangwa hivihivi.
 
"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Kama ile ilikuwa nidhamu ya uoga kwa sababu ya simba wa yuda basi tutamkumbuka sana tena sana. Yeye anayetaka nidhamu ya moyoni atuonyeshe achievements...
Nakubali the end justifies the means.
Akituletea nidhamu kubwa zaidi with different approach she will be my hero
 
Sawa boss
 
Sikupingi,hakuna mwanadam mkamilifu,pamoja na kuwa na mabaya yake bwana yule ila amekua na mazuri pia hilo siwezi kulisahau....japo wanadam tunasahau mazuri 100 kwa baya moja...
Wengi wanaomchukia bwana yule,ni wale waliozibiwa mianya yao ya janjajanja.
Hakika Mkuu kama kumchafua mzee wameshamchafua sana,hakuna jipya tena ni mipasho inaendelea
 
Nidhamu ya woga afadhali kuliko uhuru wa kuiba.

Sitetei wizi wa mali za Umma la hasha!

Lakini wacha nikuulize Mpendwa ;

Kwani wakati ule hakukuwa na wizi?

Kumbe sababu ya kumsakama CAG ilikuwa ni nini?
 
"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Hajui maana ya uongozi alio nao, hataki kumsimamia mtu yeyote ila anataka kila kitu kiende vizuri. Kuongoza bila kusimamia ni kuweka maji kwenye dema. Kikwete aliongoza bila kusimamia wakati Magufuli aliongoza kwa kusimamia: tufauti zinajulikana. Hakuna binadamu aliye malaika kiasi kuwa ukimteua tu basi atatekeleza mambo yote perfectly, lazima asimamiwe.

Serikali siyo chombo cha kubembeleza kinachotegemea hiari ya mtu, bali serikali ni chombo cha mabavu kichoendeshwa kwa kufuata sheria kikiwa kinatoa adhabu kwa kila asiyefuata sheria hizo. Inabidi rais asimamie wateule wake, ambao pia watawasimamia walioko chini yao, na msululu unaendelea hadi ngazi ya chini kabsa ya serikali.
 
Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma
Ina maana hivi vyuo kabla ya awamu hii vilikuwa vinafundisha madudu gani?

Sasa baada ya hivi vyuo kufanya marekebisho hayo, mitaala yao itakuwa pia ikionyesha "kula kwa urefu wa kamba za wahitimu wa vyuo hivyo?

Na je, makaratasi watakayokuwa wanapewa (mavyeti), sasa yatakuwa na thamani na kuwawezesha kufanya kazi?

Maswali yangu kwa sasa ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom