Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Siasa za kubagazana ndio propaganda inayowaumiza watu wengi kisaiklojia, ni wengi tu waliumizwa na kubagazwa na siasa za namna hiyo awamu ya tano.
Wengi tumereact kwa Mh. Rais kuhusu Simba wa Yuda wakati ndivyo ilivyokuwa.
Na hili ni funzo kubwa hasa kwa viongozi Vijana kuacha kutumika pasipo kutumia weledi zao.
Lakini lingine ni kuwa sisi huku mtaani hajui yaliyokuwa yakitendeka in-house kiasi kilichopelekea leo "Dhana ya Simba wa Yuda " kuibuka.
Tafsiri rahisi ni kuwa kuna baadhi ya clarified info inabidi zitoke ili kuondoa mentally ya Uungu mtu katika mifumo ya Utawala na kurejesha nidhamu yenye utii usio na woga.
Huwezi kuondoa dhana ya umungu mtu kwenye nchii hii bila kuunda mifumo inayojiendesha kama katiba, sheria na taratibu za kuongoza nchi na taasisi zake. Hata yeye hapo alipo kimadarak/kikatiba ni Mungu mtu kwa mujibu wa katiba yetu ni kwamba tu hajaguswa vizuri na vitu vizito. Magufuli hakuwa mungu mtu kwa sababu ya mapenzi yake bali katiba letu bovu ndilo linamfanya kiongozi hasa rais awe mungu mtu. Kama kweli huyu mama anamaanisha anayoyasema na si chuki kwa Magufuli aruhusu mchakato wa kupata katiba mpya na moja wapo ya kuondoa huo umungu mtu mnaousema ni kuondoa kinga ya rais kutokushtakiwa (katiba iruhusu rais aliyoko madaraka/mstaafu ashitakiwe/aondolewe madarakani itakapobainika amekwenda kinyume na katiba ya nchi au maslahi mapana ya nchi). REMEMBER THAT... GREAT MINDS DISCUSS IDEAS WHILE WEAK MINDS DICSCUSS PERSONALITY/PEOPLE.
 
Inasikitisha sana kuona kiongozi wa serikali anatamka maneno yenye kuleta mgawanyiko na mpasuko miongoni mwa watanzania. Mbaya zaidi kiongozi huyo huyo anasahau kwamba yeye ana madhaifu makubwa zaidi yanayotosha kabisa kumfanya akae pembeni akiwa muungwana.

Tazama hali ya upatikanaji umeme nchini, Tazama bei ya bidhaa mbalimbali, Tazama nidhamu katika utumishi wa umma,rushwa ufisadi n.k

Pamoja na yote hayo badala kiongozi mkuu awe mtetezi wa wananchi yeye amekuwa mtetezi wa kiti chake pamoja na wale aliowachagua Kula pamoja katika meza yenye urefu size ya kamba tofauti.

Waungwana husema Mtu mzima ukivuliwa nguo, Chutama.
Samia ni Rais Bora,huwezi kumfananisha na yule shetani muuaji
 
Mkuu Mmawia , asante kwa hoja hii ya nidhamu ya woga.

Kuna watu humu hili la nidhamu ya woga ndio wamelijua Leo baada ya kusemwa na Mama Samia.

If you have time, angalia tarehe ya bandiko hili na hoja yake muone sisi wengine tulilisema lini.


Kwa wavivu wa kufollow links, hapo niliuliza

Hatukuishia Kwa Number 1 tuu,
ila pia niliendesha somo humu namna ya kutofautisha kuongea Kwa ukali na kufoka foka

hata number 3, yule Kiranja Mkuu wa viranja pia tuliwahi kumshauri

Hata baadhi ya Mawaziri walipokosa utu, akina sisi tuliwasema...

Na hatukuishia viongozi wakuu na Mawaziri pekee, hata ma RC tuliwamulika

Huyu pia

Hivyo hili la nidhamu ya woga lilikuwepo sana kwa JPM, lakini twende nyuma na kurudi mbele,
Kwa hali hii, mfano Mama naye ni binadamu, anaweza kukosea, jee akikosea kibinaadamu, kuna kiongozi yoyote ndani ya serikali anaweza kum correct, au kuna any main stream media that would dare criticize or correct her, or the epitome of cowardice inaendelea?!.

Nasisitiza Mama naye she is a human being, anahitaji kusapotiwa, kusaidiwa, kushauriwa, na akikosea akosolewe kistaarabu kwa lugha ya heshima na staha huku akishauriwa the right thing to do, ushauri wangu wa kwanza, ni Tanzania tunaweza kabisa kusonga mbele na kufanya mazuri bila kunyoosheana vidole and calling names kama "Simba wa Yuda".
Nashauri tufanye tuu mambo tofauti bila kumtaja taja Kwa ubaya!
Aachwe Apumzike!.

Jumapili Njema

Paskali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mungu mtu by virtue of the Consititution of URT. Hatuwezi karne hii kutegemea utashi wa mtu kuongoza nchi ndiyo maana akija huyu tunasifu akija mwingine tunalaumu ni kwa sababu nchi hii inaongozwa kwa utashi wa rais aliyoko madarakani (mungu mtu) na si mifumo ambayo hata raisi anawajibika kuifuata. Wanatofautiana tu style za kuongoza ila rais yoyote wa JMT ni mungu mtu. Haya mengine ni mbwembwe tu. Tunahitaji katiba itakayoondoa uungu mtu wa urais wa JMT na viongozi wengine waliyovalishwa madaraka kupita kiasi na katiba letu bovu.
 
Wewe unamuonaje CAG wa sasa.


Bado naendelea kumsoma, sijajua kama msimamo wake kiweledi , kimaadili na kiuwajibikaji na kiutendaji ukoje kwa kiasi gani iwapo ni wa kuridhisha au namna gani?
 

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.
na
Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Nae si alikuwa humo humo kwenye awamu ya 5 na yeyeyndiemnufaika namba 1 wa hiyo awamu, dada anaupiga mwingi hadi anasahau mpira kaucha wapi
 
S

Vyote ulivyosema sio ukweli. Kwani sukari imepanda kipindi Cha Nani?.

Halafu kuhusu ajali mbona zilikiwepo nyingi?. Umesahau ajali ya meli ya ukerewe, ajali ya city boys , ajali ya morogoro waliokufa watu 100.

Kwangu Mimi Magufuli alikuwa mpenda sifa na Wala hakufanya Mambo kwa upendo .
Kuhamisha serikali kutoka magogoni kwenda Dodoma vipi?
Wilaya zilizokuwa sugu hazikuwa na ofisi, vipi na hao?
 
Simba wa Yuda aliikuta hiyo nidhamu ya kweli ya kutoka moyoni? Alikuta watu wanafanya kazi kwa kufuata sheria?

Na unaamini huu utawala wake huyu mama kwa msaada wa Jk ndio kutakuwa na nidhamu ya kweli na kufuata sheria kazini?

Au unaongea tu kisa una hasira na Magufuli? Mimi sijawahi kukosa amani ya moyo wakati wa Jiwe na wala hata sasa huyo Samia hanikoseshi amani ya moyo, tatizo ni ninyi ndio mna mna matatizo ya kisaikolojia mkiona katajwa Jiwe tu mnachefukwa, sasa hilo ni tatizo mnahitaji msaada.

Dhalimu hakukuta nidhamu ya woga, bali akapandikiza nidhamu ya woga, nidhamu hiyo ilipelekea watu aliokuwa na chuki nao kunyanyaswa, na kufanyiwa ukatili wa wazi. Sisi huku mitandaoni tulikuwa tunampa ukweli wake toka akiwa hai, na hata baada ya kufariki tunaweka ukweli wake wazi, ili kuepusha upotoshaji na sifa za kinafiki. Yaani hatupati tabu since hatujawahi kumkubali alivyokuwa mzima, au akiwa huko ahera madukani. Hatuhitaji msaada wowote maana hii kwetu ndio inatufanya tuwe na nguvu za kiume za kutosha.
 
Shida ni kwamba waliopo sasa wapo kwa ajili ya kulinda interest zao tu.

Wanaoumia ni wengi kuliko wanaonufaika.

That is wrong.
Kwani wale wa awamu ya 5:
1. Hawakuumiza watu?
2. Hawakuwa na interest zao?
 
Hakuna sehemu mtu wa kitaifa alishawahi kusema Yesu Kristo au Simba wa Yuda, hao wa mitaani hawana impact. Usilete utetezi ambao haupo. We unadhani kwanini basi wame react this time? Na kama kuna sababu basi hiyo hiyo a deal nayo...Otherwise tuache kuwa defensive, haisaidii. Kama kuna sababu basi hiyo sababu aiondoe ili aongeze kura zake kwakua kila kura ina thamani kwa mwanasiasa.

Amekuambia anategemea kura kupata madaraka? Dhalimu alitangazwa na tume isiyo huru ya uchaguzi kuwa alipata kura 12.5m, je alipata hizo kura Kweli?
 
Nimepitia comments humu kujaribu kuangalia kama Kuna aliye mshauri Huyu mama afanye nini ili kuleta nidhamu kwenye utumishi wa ummma lakiki wapi!!

Magufuli sawa alitishia, Ila nidhamu tuliona,. Je, huyu mama yeye anafanya nini ili kuleta nidhamu hyo. Au yupo haunted na fact kwamba nidhamu kwa Sasa ime dwindle.

Halafu eti anataka nidhamu ya kutoka moyoni eh! Kwa wabongo aliokwisha waruhusu wale kwa urefu wa kamba zao, eh! Jamani,!!

Kwa hapa namheshim tu Kiti Cha urais.

Sema akili pia za wabongo ni mtihani kung'amua hizi twists of words.

Mimi naomba nisamehewe tu. Huyu mama najitahidi kweli kweli kumuelewa lakini wapi?! Naishia kupata 'F'

Nilifurahi alipozungumzia mabadiriko ya elimu, Ila Sasa mengine haya, napata taaabu kwelikweli.

Emwenyezi Mungu nijalie hekima.
 
Nae si alikuwa humo humo kwenye awamu ya 5 na yeyeyndiemnufaika namba 1 wa hiyo awamu, dada anaupiga mwingi hadi anasahau mpira kaucha wapi
Yetu macho na masikio
 
Dhalimu hakukuta nidhamu ya woga, bali akapandikiza nidhamu ya woga, nidhamu hiyo ilipelekea watu aliokuwa na chuki nao kunyanyaswa, na kufanyiwa ukatili wa wazi. Sisi huku mitandaoni tulikuwa tunampa ukweli wake toka akiwa hai, na hata baada ya kufariki tunaweka ukweli wake wazi, ili kuepusha upotoshaji na sifa za kinafiki. Yaani hatupati tabu since hatujawahi kumkubali alivyokuwa mzima, au akiwa huko ahera madukani. Hatuhitaji msaada wowote maana hii kwetu ndio inatufanya tuwe na nguvu za kiume za kutosha.
Umenena ukweli
 
Back
Top Bottom