Mariwand
Member
- Jun 14, 2022
- 86
- 77
Jecha hadi nae akagombea kule Zanzibar na bado akaliwa kichwa😂😂😂Nilimsikia Chebukati anasema huu ndo uchaguzi wake wa mwisho, ingekuwa poa tungemwomba aje hapa bongolala apambane na wazee wa mabegi meusi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jecha hadi nae akagombea kule Zanzibar na bado akaliwa kichwa😂😂😂Nilimsikia Chebukati anasema huu ndo uchaguzi wake wa mwisho, ingekuwa poa tungemwomba aje hapa bongolala apambane na wazee wa mabegi meusi.
Hajapongezwaa Ruto hapo.Rais Samia Hassan Suluhu ametuma salamu za pongezi kwa William Ruto kwa ushindi wake nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya, matokeo yalitangazwa jana Agosti 15, 2022
Achana na chuki kwa Raisi leteni hojaHujui unalotetea, poor you
Hawana ujuaji. HAWAJUI.Kampongeza kama rais mteule, shida ipo wapi? muwe mnaacha ujuaji usio na maana....
Bavicha hao kila kitu wanajua wao!Wabongo bhana! Jana kuna mwezio humu alikuwa analaumu kwanini kachelewa kumpongeza Ruto, wewe leo unalalamika kwanini kawahi. SMH
Watu na nusu wenye ukabilaMnadhani Kenya ni kama Bongo kila kitu kwa maelekezo kutoka juu? wale ni watu na nusu msiwachukulie poa kabisaaaa, Tuna vitu vingi sana vya kujifunza kutokana na IEBC walivyosimamia zoezi na kutangaza matokeo, na bila aibu kabisa wala woga nikaliona Limahera la NEC na lenyewe ati limeenda Kenya kujifunza uchaguzi kule aibuuuuu.
Uko vizuri blance86,Nashukuru kwa uchambuzi,wengi tunafagia tuu!VIKWAZO VITANO VYA RUTO KABLA YA KUAPISHWA
AMESHINDA au ametangazwa, hizo ni tafsiri za wenye kuchagua upande. Team Hustlers wanafurahia ushindi. Dk William Ruto ni mshindi wa kiti cha urais.
Ametangazwa; ndivyo Timu Baba wanaamini. Msimamo wao ni kuwa Tinga Raila Odinga alishinda, ila hajatangazwa. Mgombea Mwenza, Martha Karua amesema “haijaisha", kwa hiyo mapambano yanaendelea.
Hustlers wanauliza: “Tinga kila siku anaibiwa kura yeye tu?” Wapo shereheni, wakingoja mtoto wa mkulima hohehahe aapishwe kuwa Rais wa Tano wa Kenya. Ndio, Ruto ni mwana wa kapuku, aliyeuvaa u-hustler na kupanda ngazi za kisiasa na kiuchumi hadi kuwa Don.
Agosti 30, ingekuwa ni siku ya Ruto kula kiapo. Ingekuwa kiapo cha tisa cha urais tangu Uhuru wa Kenya. Jomo Kenyatta aliapa mwaka 1964, Daniel Moi 1978, 1992 na 1997, Mwai Kibaki 2002 na 2007, Uhuru Kenyatta 2013 na 2017.
Katiba ya Kenya ibara ya 141 (2) (a), inaelekeza Rais Mteule kuapishwa siku 14 baada ya kutangazwa, kama hakutakuwa na shauri lolote lililowasilishwa mahakamani kupinga ushindi wake. Ruto alitangazwa mshindi Agosti 15. Siku 14 zinaisha Agosti 29. Hivyo, Agosti 30 ingekuwa siku ya kikatiba ya Ruto kuapishwa.
Ibara ya 140 ya Katiba ya Kenya, kupitia ibara zake ndogo tatu, imefungua milango kwa mtu yeyote kuupinga ushindi wa kiti cha rais. Sharti ni malalamiko kuwasilishwa ndani ya siku saba (7), na kesi isikilizwe na kutolewa uamuzi ndani ya siku 14. Mahakama ikibatilisha matokeo ya urais, uchaguzi mpya utaitishwa ndani ya siku 60.
Ibara ya 141 (2) (b), inaelekeza kuwa Mahakama ikishapitia shauri na kuridhika ushindi ulikuwa halali, Rais Mteule ataapishwa Jumanne ya kwanza inayoangukia baada ya siku saba tangu Mahakama ilipotoa hukumu.
Chukua maneno ya Martha kuwa “haijaisha”, rejea mwanya wa Katiba wa kuupinga ushindi wa kiti cha Rais mahakamani. Kisha tuvione vikwazo vitano ambavyo Ruto anapaswa kuvikabili na kuvishinda kabla ya kuwa Rais.
MOSI; hadi sasa ushindi wa Ruto unakabiliwa na mashitaka mawili mahakamani. Hivyo, hata Mahakama ikiridhika kuwa ushindi wake ni halali, inaweza kumfanya asubiri hadi mwezi mmoja ili aape kuwa Rais badala ya siku 14. Siku saba za mashitaka, 14 za kusikiliza na kuhukumu, saba nyingine za kusubiri kiapo.
PILI; Wanaharakati 11 waliwasilisha pingamizi mahakamani kutaka Ruto na Mgombea Mwenza wake, Rigathi Gachagua, wasiapishwe kama wangeshinda uchaguzi. Agosti 12, Mahakama ilisajili kesi na leo (Agosti 16), inaanza kusikiliza.
Wanaharakati hao wanapinga Ruto kuapishwa kwa sababu Gachagua anakabiliwa na kesi za jinai ikiwemo za ufisadi na utakatishaji fedha haramu. Hivi karibuni, Mahakama ya Juu Kenya ilitoa ruhusa Serikali kutaifisha Sh202 milioni za Kenya (Sh4 bilioni) kwenye akaunti ya Gachagua. Jaji alisema, Gachagua alipata fedha hizo kwa njia ya rushwa.
TATU; Azimio la Umoja waliingia kwenye uchaguzi wakiwa wamewasilisha pingamizi mahakamani kuwa Ruto na Gachagua wakishinda uchaguzi wasiapishwe. Hoja ni kesi mfululizo za jinai zinazomkabili Gachagua, hasa za rushwa na ufisadi wa mali za umma.
NNE; Saa chache kabla ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati, kumtangaza Ruto mshindi, Makamu Mwenyekiti, Juliana Cherera, akiwa na makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang'aya, walitangaza kutokubaliana na matokeo ambayo yangetangazwa kwa kuwa mchakato wa mwisho ulikosa uwazi.
Cherera kwa niaba ya makamishna hao, aliwataka wagombea ambao hawakuridhika na matokeo kutofanya fujo, kwani kuna mlango mwingine wa kuipata haki. Walitoa ahadi ya kushirikiana na watakaopinga matokeo.
TANO; Azimio la Umoja wameweka wazi nia ya kwenda mahakamani. Hoja ni kutotimia kwa akidi wakati wa kutangaza matokeo, hii ni kwa sababu ya Cherera na makamishna watatu kujiweka kando. Wanasema Chebukati alivunja sheria ya uchaguzi kumtangaza mshindi bila akidi kutimia.
Hoja ya pili ni kukosekana uwazi. Azimio wanalalamika kwamba wakala wao alinyimwa fursa ya kuona fomu yenye majumuisho ya mwisho ya kura za urais. Gavana wa Kitui, Charity Ngilu, amesema Raila alipata kura zaidi ya 7.3 milioni na sio 6.9 milioni zilizotangazwa na Chebukati. Hapa kuna madai ya wizi wa kura.
Hivyo ni vikwazo ambavyo Ruto anavikabili mpaka kuapishwa. Ni vikwazo juu ya vikwazo; walisema asingeteuliwa kuwa mgombea urais, akateuliwa. Akafanya kampeni kwa mapambano makali. Wakasema asingetangazwa, ametangazwa. Sasa muziki upo mahakamani. Wanasema hataapishwa!
Hii ngoma imeiva au bado mbichi?
Ndimi Luqman MALOTO
Gentaymcine huwa ni mjuaji mjuaji sana sijui anajikuta nani aiseeKampongeza kama rais mteule, shida ipo wapi? Muwe mnaacha ujuaji usio na maana....