Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Hii nchi KWA Sasa inapoelekea ni shimoni kabisa, hata hyo elimu ambayo ni nguzo ya nchi KWA Sasa inadharaulika na itaendelea kudharaulika Zaidi. Hivi mtu akifoji kitu official si ni mualifu na adhabu yake inaweza kua kifungo mpaka miaka7?


Nilitegemea Hawa watu kua jela Kwa Sasa, lakini ndo kwanza wanarudishwa kihuni huni tu.


Yaani nchi KWA Sasa haina Dira
 
Mambieni ahalalishe na fedha bandia tu,hata risit bandia tu poa maana wahalifu KWA Sasa wanaachiwa KWA hoja nyepesi sana;

Walianza watuhumiwa wa ufisadi tena wengine wa wazi wazi kama kina papa Musofe, Manji, Seth na wengine.

Now wameachia wahalifu wa kufoji vyeti na wapo watu wanashangilia, Si tuanze kuwafojisha watoto wetu tu vyeti maana elimu haina maana sasa
 
Sijaelewa vizuri ,waliofukuzwa vyeti feki walikuwa zaidi ya elfu 10 ,criteria gani iliyotumika kurudisha 4100? Kama ni kweli basi Mama SSH anazidi kuupiga mwingi ,vipi hao elfu 6 waliobaki stahili/stahiki zao watapata?
 
hamna kitu kinasikitisha kama uhangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote hizi za dunia, halafu uje kukutana na mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ili apate ajira kwa kufoji vyeti, hii haiko sawa Magufuli alisema shukuruni mmeachwa ilibidi mfunguliwe na mashtaka kabisa

hata kama nia ni kupata wapiga kura wa baadae atambue kuwa sio sahihi kuruhusu watu ambao hata kwenye tangazo la kazi ilisema wazi kabisa udanganyifu hautoruhusiwa

aim for the stars
 
Taarifa za ndani nikwamba hao waliorudishwa ni wale CCM kindakindaki..inagwa magufuri yeye hakujali ushauri mwanzoni wa kuwaacha wanaccm akafukuza wote sasa mama SSH ameamua kuwarusahia wafanyakai waliokuwa wanachama wa CCM tu ila wengine wote wameliwa
 
Hiyo ni pandora's box amefungua.
 
Hivyo ndiyo ilikuwa suluhishi bora. Hata JPM alipowaondoa binafsi niliona ingekuwa vyema wangelipwa mafao yao kwa muda waliotumikia. Hata sasa ingefaa ifanyike hivyo kuliko kuwarudisha tena kazini.
 
Labda wamedushwa wale waliotolewa kimakosa na drs la 7

Maan mimi bado sijamuona alie rud kzn hadi sasa.
 
Hakuna alosema walofoji vyeti warudi kazini bali wale darasa la saba na baadae wakajiendeleza ndo wanarudi kazini.

Acha kuwatia viongozi maneno mdomoni
 
Sijaelewa vizuri ,waliofukuzwa vyeti feki walikuwa zaidi ya elfu 10 ,criteria gani iliyotumika kurudisha 4100? Kama ni kweli basi Mama SSH anazidi kuupiga mwingi ,vipi hao elfu 6 waliobaki stahili/stahiki zao watapata?
4100 hawakufiji vyeti bali waliingia bila kukidhi vigezo vya ajira mfano mtu darasa la saba aliajiriwa na baadae kujiendeleza hadi kufika form four, huyu anastahili kurudishwa kwa kua hakufoji vyeti na hakuna jinai kwake
 
Aisseee....

HAPA MAMA KAUPIGA MWINGI AISEE
 
Kati ya 4000+ waliojiendeleza kielimu watakuwa wangapi?waliofika mda wa kustaafu niwangapi?na zile stress mtu atajiendeleza kweli?
Wanasiasa wana udanganyifu sana
At least watalipwa mafao yao mkuu..
Magufuli ktk hili alifanya ukatili mkubwa mnooo...

Maana ni maCCM haohao ndo waliwaajiri.
 
Kama hukuwa na ndugu, jirani, rafiki aliyekutana na hayo masaibu hakika huwezi elewa maumivu waliyopitia.. Huwezi.
 
Anyway, awalipe fidia na wale waliobomolewa nyumba zao maeneo ya Kimara wakati wa Mwendazake.

Halafu walijiendeleza lini na wapi ? sikupenda watu wafukuzwe kazi kama awamu ya 5 ilivyofanya , lakini porojo kwamba walijiendeleza ni uzushi .
Ulitaka na kujiendeleza serikali iwaambiee!??? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡
 
Wapo waliokuwa na vyeti visivyo na sifa.. Hao ndo wanahusika kujiendeleza.
 
Wengi waliopo mitaani bila ajira na wengine walio bahatika kupata ajira walifundishwa na walimu waliodaiwa kufoji vyeti!!!
 
Nimeipenda, mtu hawezi kufanya kazi miaka 10 halafu unamtoa kirahisi tu...
Muhimu wangepewa stahiki zao waondoke lakini sio kufanya walichofanya, kwanza itakuwa walipewa kazi kwa kubebana/kujuana wakawaacha wenye sifa waliostahili kazi hiyo hii ni dhambi hata kwa Mungu.

Hao jamaa ni wahalifu na walistahili kufikishwa mahakamani kwa uhalifu wao lakini sio kupewa nafasi wakasome wakati wapo waliokwisha soma na hawana ajira wanahangaika mitaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…