Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Tatizo inaonekana zoezi liliendeshwa bila haki, sina hata uhakika kama walioachishwa walipewa nafasi ya kujitetea, nina uhakika kuna watu wengi walionewa tuu maana records zetu ni za kuunga unga tu,

kama imegundulika kuna walioonewa na hakuna namna ya kufanya verifications 100%, rudisha wote kazini zoezi lianze upya, na hata kama walifoji kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza dereva au tarishi kwa kufoji cheti cha form four (ubinadamu kidogo), tuanze kujenga mifumo yetu vizuri kuzuia haya matatizo
 
Huu ni utumbo kabisa basi na afute sitisho la ajira kwa wahitimu wa Ualimu na wote wapewe ajira kuanzia mwaka 2015 alipositsha Jiwe na pia iwe kama zamani wakitoka chuoni mojamoja wapangiwe vituo vya kazi.
 
Wadau Hayati RAIS MAGUFULI Aliwaondoa Makazini WATUMISHI wote WalioGHUSHI Vyeti na Nyaraka mbalimbali.
Kitendo cha Kughushi CHETI au NYARAKA yoyote ni KOSA la JINAI
Inakuwaje SERIKALI inawarudisha Makazini WATUMISHI waliotenda huo UHARIFU?
Nilitarajia kama WAHARIFU WENGINE Wangeshtakiwa na Kuwafikisha MAHAKAMAMI sio MAKAZINI
 
Naamini tasisi imeona utendaji wao
 
Kuna uhalifu mzuri na wenye faida wa kulisaidia Taifa lako mkuu. Kuna kipindi inatakiwa mtu auwae ili Taifa Kama Taifa lipone ama lijiokoe.
Wameshakata uzoefu wa kazi acha wafanye kazi. Atakuja raisi mwingine watarudi majumbani tena atakuja mwingine atawarudisha. Nchi yetu inaendeshwa kwa utashi mtu alivyopata raha ama hasira tokea kwa mwenza wake.
 
Tanzania ni Nchi Ngumu Sana

Tanzania ni Tajiri

Ndugu Zangu Tuchape Kazi Tukimtanguliza Mungu Mbele
 
Kuna familia ya mbunge mmoja wa kanda ya ziwa waliliwa vichwa wana ndugu 5 kwa kutumia cheti kimoja watu 6! Ngoja nijifanye kuwatembelea nione kama wote wamerudi kazini!

Mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho ata kile kidogo atanyanganywa na kupewa aliyenacho.
Korosho zimekosa wanunuzi, hakika tutamkumbuka!
 
Hapo ni mkakati unasukwa wa kuwatengeneza watumishi hewa ili pesa ipigwe.
 
HONGERA na SHUKRANI nyingi kwa rais Samia kwa huruma ya kiuzazi. Kughushi vyeti ni kosa kisheria lakini katika mazingira ambapo waliofukuzwa walifanyiwa kibaguzi inatosha kuharamisha zoezi. Kwa mfano MAJESHI yote, Makonda Bashite , Mwigulu, Kingwangala nk hawakufukuzwa. Lakini pia hilo kosa lilifanyika kati ya waajiriwa na waajiri kwa maana ya shared responsibilities. Kisha mtu amekufanyia kazi vizuri kwa miaka 30, 20, 10 nk leo unamkanaje?

The best solution ilikuwa kuwastaafisha na kuwalipa, au kuwaacha wastaafu kwa hiari au wastaafu umri ukifika. Muhimu zaidi KUZUIA walioghushi kuajiriwa kwa maana ya kuwa makini wakati wa kuajiri.

Kisiasa, zoezi hili linapunguza negative effects za kufukuzwa wamachinga. Ni siasa nzuri mama Samia. Ukimwachia huru na Mbowe na wale wengine wote mnaowaonea kwa kuwa tu ni wapinzani , (tena upinzani ulioko kisheria)utapata kura nyingi pamoja na yangu.

Diffuse political temperature isiyokuwa ya lazima wala tija. Nyie mnaorudishwa kazini mshukuruni MUNGU kwa kumng'oa JPM , kwa kuleta SSH kama Rais na mzidi kumwombea ili aukatae UOVU, uonevu, ubaguzi, ubadhirifu ili nchi ipate maendeleo na baraka. Mwombeeni afuate na aheshimu Katiba na sheria za nchi moyoni na kimatendo. Mchape kazi msahau yaliyopita huku mkiganga madhara mliyopata. Maisha ni safari ndefu.
 
Kazi na iendelee!
 
Hawa watalipwa mishahara yote pamoja na posho za usumbufu kwa kipindi chote walichokuwa mtaani. Hongera CCM mna tengeneza tatizo then mnalitubu afu mnaomba credit kwa wananchi.
 
Hii itakuwa ni hela ya mtu mkubwa tu inaingiziwa mkwanja wa hao wote wanaojiita vyeti fake wamerudishwa ama wamejiendeleza
 
Kama nimemuelewa vzr Waziri ni kwamba wanaorudishwa kazini niwale walioondolewa kazini kwa kutokuwa na elimu ya kidato cha nne na sasa wameshajiendeleza na sio wale 12,000 waliogushi vyeti.
 
Kwani Mungu aliumba kuku au yai?
 

Kwahiyo sheria hazifuatwi kwenye haya mambo bali ni utashi wa rais.
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi hawakughushi kabisa, kosa lao walikuwa wamefika darasa la saba na baadae wakaendelea kupata vyeti vya (mfano) udereva kwa madaraja tafauti. Hivi vyeti vya udereva vilikuwa sahihi siyo feki, sasa hapo unawaondoa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…