sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.
Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.
Nilitegemea Hawa watu wawe mfano wa onyo la kughushi vyeti lakini ndio kwanza wanarudishwa kazini, ni sawa na mtu aliefungiwa account yake benki alipokamatwa akingiza noti feki ila sasa anasamehewa na zile noti feki zinahesabiwa kuwa orijino.
Vijana kibao wapo mitaani wamesoma kwa shida ili kumaliza degree / masters, kiukweli hawatendewi haki hawa vijana, Binafsi sikuwa fan wa magufuli lakini kuna mambo machache sana aliyoyafanya nilikuwa upande wake likiwemo hili swala la kuchomoa wanao ghushi vyeti,
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora imetangaza kuwarejesha kazini Wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4000+) ambao waliondolewa kazini kutokana na kugushi vyeti katika maeneo mbalimbali lakini sasa kwa huruma ya Rais Samia watarejeshwa kazini kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mohamed Mchengerwa amesema "wale walioweza kujiendeleza ambao ni zaidi ya 4100 tayari wamerejeshwa kazini, pia tunao Watumishi 1150 ambao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kuitumikia Serikali japo walikua ni Watendaji wazuri”
Rais Samia alishatuagiza kwamba hawa 1150 kutokana na utendaji wao uliotukuka Watumishi hao wote walipwe haki zao na stahiki zao kama vile wapo kazini kwahiyo watalipwa"