Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Hii nchi KWA Sasa inapoelekea ni shimoni kabisa, hata hyo elimu ambayo ni nguzo ya nchi KWA Sasa inadharaulika na itaendelea kudharaulika Zaidi. Hivi mtu akifoji kitu official si ni mualifu na adhabu yake inaweza kua kifungo mpaka miaka7?


Nilitegemea Hawa watu kua jela Kwa Sasa, lakini ndo kwanza wanarudishwa kihuni huni tu.


Yaani nchi KWA Sasa haina Dira
Wamerejeshwa wale waliojiendeleza kielimu.
 
Utadhani hakuwa kwenye hiyo serikali.

Ipo siku Rais mwingine anaetokana na CCM, atakuja kumuomba radhi Mbowe kwa kesi ya kusingiziwa, na pengine kumlipa fidia, na CCM hawa hawa wanafurahia Mbowe kuwekwa ndani, watampongeza huyo Rais.

Kuwaelewa CCM na akili zao, ni vigumu kama ilivyo vigumu kujua Mungu alitoka wapi au kati ya yai na kuku, kipi kilianza.

Anyway, awalipe fidia na wale waliobomolewa nyumba zao maeneo ya Kimara wakati wa Mwendazake.
Wale watu walionewa pure and simple, huwezi fukuza mtu kazi amefanya kazi miaka 20 eti umwambie huna elimu, sijui ulirudia darasa la saba kwa jina jingine, kilichotakiwa na kuweka mfumo wa kufanya hayo makosa yasijirudie, sio kufukuza kazi mtu kabakiza miaka 2 kustaafu,
Tatizo wabongo ni wanafiki hatuna jema, hili nalo mtakosoa utafikiri hizo nafasi 4000 ndo zimechukua nafasi zote za graduates,
Juzi tu zimetoka nafasi lukuki, polisi, pccb, Tra,, Mbona enzi za zamani ajira zilisita kabisa na midomo watu walifunga yaani, [emoji16][emoji16]
 
Nadhan ni wakat muafaka kwa sasa kuwalipa fidia wavuvi waliochomewa nyavu zao za mamilioni na kusukumizwa kwenye umaskini na hata wengine kupoteza maisha kwa stress. Hawa ni wale waliokuwa wamenunua nyavu zao kutoka maduka ya hapa nchini na kupewa rist halali za malipo,lkn ghafla nyavu hizo hizo kuonekana ni haramu na watu kuanza kusakwa kila kona,kuchomwa moto na kupigwa faini kubwakubwa....eti "uvuvi haramu".
Mama ukimalzana na hao feki,wageukiye na hao ndg zetu
 
Iwarudishe wote waliofukuzwa ule ni uonevu
Ndio walio karibia kustafuu wapewe haki zao huo ni uonevu mama au baba maisha yake yote kafanya kazi serikarin leo unamtoa hata shi 10 hakuna du dhambi kati ya dhambi magu kafanya ni hiyo uonevu sana
 
Taarifa za ndani nikwamba hao waliorudishwa ni wale CCM kindakindaki..inagwa magufuri yeye hakujali ushauri mwanzoni wa kuwaacha wanaccm akafukuza wote sasa mama SSH ameamua kuwarusahia wafanyakai waliokuwa wanachama wa CCM tu ila wengine wote wameliwa
Makonda nae karudishwa nasikia
 
Ye mwenyewe angekuwa na vyeti halisi ben asingepotea
 
Kama nimemuelewa vzr Waziri ni kwamba wanaorudishwa kazini niwale walioondolewa kazini kwa kutokuwa na elimu ya kidato cha nne na sasa wameshajiendeleza na sio wale 12,000 waliogushi vyeti.
Na ndo ilivyo Sasa sijui nani anaeneza huu uongo? Itabidi serikali iwaeleshe watu, walioruhusiwa kurudi ni wale darasa la Saba tena wengi walikuwa madereva na kweli walikuwa wanajiendeleza na walianza kurudishwa tangu JPM yupo na siyo vyeti feki.
 
Nanyie muelewe , waliorudhishwa ni wale ndugu au wapenzi wa CCM kindkindaki..Magufuri aliambiwa hao awaache akawambishi..Sasa ili kutoshambuliwa na wananchi..ndo wamekuja na gear yakiwa hao wamejiendeleza.
Thanks
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.

Nilitegemea Hawa watu wawe mfano wa onyo la kughushi vyeti lakini ndio kwanza wanarudishwa kazini, ni sawa na mtu aliefungiwa account yake benki alipokamatwa akingiza noti feki ila sasa anasamehewa na zile noti feki zinahesabiwa kuwa orijino.

Vijana kibao wapo mitaani wamesoma kwa shida ili kumaliza degree / masters, kiukweli hawatendewi haki hawa vijana, Binafsi sikuwa fan wa magufuli lakini kuna mambo machache sana aliyoyafanya nilikuwa upande wake likiwemo hili swala la kuchomoa wanao ghushi vyeti,

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora imetangaza kuwarejesha kazini Wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4000+) ambao waliondolewa kazini kutokana na kugushi vyeti katika maeneo mbalimbali lakini sasa kwa huruma ya Rais Samia watarejeshwa kazini kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mohamed Mchengerwa amesema "wale walioweza kujiendeleza ambao ni zaidi ya 4100 tayari wamerejeshwa kazini, pia tunao Watumishi 1150 ambao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kuitumikia Serikali japo walikua ni Watendaji wazuri”

Rais Samia alishatuagiza kwamba hawa 1150 kutokana na utendaji wao uliotukuka Watumishi hao wote walipwe haki zao na stahiki zao kama vile wapo kazini kwahiyo watalipwa"
Tunaomba Machinga pia waachwe maana nchi yetu hatutaki kufuata sheria
 
Hawa watalipwa mishahara yote pamoja na posho za usumbufu kwa kipindi chote walichokuwa mtaani. Hongera CCM mna tengeneza tatizo then mnalitubu afu mnaomba credit kwa wananchi.
Upuuuzi mtupu hawa ccm wafe wote itakuwa afadhali kuliko kuwa nao waliopo ssa
 
Duu ina maana wamejiendeleza kuanzia march mwaka huu hadi leo November? ina maana walifanya mitihani wapi na lini? hahahahahaha
 
Back
Top Bottom