#COVID19 Rais Samia azindua Chanjo ya COVID-19 na kuchanjwa. Asema hawezi kujipeleka kwenye Kifo
Wataalamu watusaidie kwa nini chanjo ya corona ukichanjwa unasambaza virusi tofauti mfano delta variant wakati hizi nyengine tulizochanjwa haikuwa hivyo?
 
Njia mbadala ni kuwalazimisha wananchi wachanje, ambayo ni 'risky, kwa sababu hakuna anayetaka kuweka dhamana ya matokeo ya chanjo si tu Tanzania, bali kila taifa duniani.

Kwa sasa, bado Serikali haijaamua kuwapa wananchi sababu ya msingi ya kuchanja.

Huoni hapo viongozi wavchini yake wamelazimika kuchwa kulinda vitumbua vyao na wasionekane wasaliti. Very unfair practice.
 
Uwezo wetu mdogo sana, yani tumeshindwa hata kutuma watalamu watuletee report kwa nini nchi zilizoanza kuchanja tangu mwaka 2020 mfano Rwanda bado maambukizi ya corona ni makubwa kuliko Tanzania?
Una uhakika no makubwa kuliko hapa?
 
Kila mtu na imani yake je kama hao madaktari na wengineo hawamuamini Mungu wa gwajima hio laana itawapataje?

Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo na kusikilizwa
Kumbe Gwajima ana Mungu wake ambaye sisi wengine Mungu wetu Yehova Yahweh anahubiriwa Makanisani na Misikitini......ok nimekupata

#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Watu wanahofia kukosa ulaji mkuu;
Kwani nani anataka kuwa na PHD halafu ni unemployed au anashika chaki maisha yake yote??

Lazima wamplease mtawala Ili mambo yao yaende jambo ambalo ni baya sana kwani maamuzi mengi yatakuwa yanafanyika kumplease mtu badala ya National Interest.
Naanza kuona umuhimu wa katiba, Cdm wako sahihi, kungekuwa na baadhi ya post anazoteua Rais zinatokana na kuinterviews na mtu apate kwa competency haya mambo ya kuhama na upepo yasingekuwepo
 
Wewe mwenye akili za KICCM ndio ufukuzwe Tanzania kabisa. Kila kitu unawaza KICCM waza kwa kutumia akili zako.
HAKUNA wa kunifukuza nchini mwangu....mimi ni raia wa vizazi vingi nyuma.....

Ila CCM ni chama chenye kanuni zake....wameshawahi kufukuzwa WENGI wenye kaliba kubwa ya kisiasa zaidi yake mbunge Gwajima.....

HASHTAG Gwajima afukuzwe ndani ya CCM

#GwajimaAfukuzweCCM
#JMTMilele
#NchiKwanza
 
Mzee wa upako, Athony Lusekelo ameitwa kufungua kwa sala na kabla anatoa maneno machache ikiwemo kutaka watanzania kuiamini chanjo kwani Serikali imejiridhisha.

Pia ameongelea kauli ya Magufuli na kusema hakukataa bali alitaka tahadhari, Mwisho amesema wakristo kuna mambo wanakubaliana wote kwa pamoja.

WAZIRI WA AFYA, GWAJIMA
=>
Leo ni siku ya kihistoria ambayo tunachukua silaha za kisasa kwenda kupambana na Uviko

= > Hayati Magufuli alisema wizara ya Afya isikimbilie machanjo bila kujiridhisha, leo kuna watu wanapotosha.

=>Huko, Vifo vilikuwa vinafika 3000 mpaka 4000 kwa siku sasa hali imebadilika

=> Eti chanjo inavuruga utu wa mtu, ni uongongo, tutalieleza. Wa HIV ndio angeenda kupangua huo utu.

=> Maabara tunazo, wataalam tunao. Watanzania wasiwe na hofu. Vitu vyote hakuna visivyo na madhara lakini tunaoutways faida kuliko madhara. Mbona ukinywa Quinene kichwa kinauma, fragile ambae ni malkia wa maumivu ya tumbo pia ina madhara.

=> Mie ndio waziri wa Afya nimeapa, siwezi kumshauri Rais vibaya, naomba wanahabari mzingatie maadili yenu, wale mnaokata ujumbe usiojitosheleza kuongeza followers Mungu anawaona


WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA
=>Nikiwa mwenyekiti wa kamati inayoratibu ugonjwa wa Covid, tukuhakikishie tunaendelea kukaa pamoja, kuratibu na kushauri pia tumeendelea kupokea miongozo ya kitaalam kutoka kwa wataalam wetu.

=> Hatua mbalimbali zimechukuliwa duniani kote, tumepata uzoefu ikiwemo uchanjaji na leo tumeanza kuhamasisha watu kuchanja kudhibiti ugonjwa huu. Wataalam wamepata elimu ya kutosha ndani na nje ya nchi.

=> Mie nimekubali kuungana nawe kuchanja kuonyesha Serikali haina nia mbaya kwa wananchi wake, Mheshimiwa Rais ameapa kulitumikia Taifa hili, tunachokileta kwenu kimetokana na utafiti, sisi tuko pamoja nawe na maamuzi haya tunakupongeza sana.

=> Huku tumefanya mambo mengi, Mheshimiwa Rais leo ni siku yako.

RAIS SAMIA SULUHU
=> Juzi kupitia ubalozi wa Marekani tumepokea chanjo hizi, leo baada kuthibitishwa na wizara ya Afya tunaanza kuzitumia. Niwashukuru wote mlioko hapa kuniunga mkono kuonyesha chanjo sio balaa

Kuna ambao wanalikataa lakini wengi wanalikubali, jana nilikuwa na mazungumzo na CDC na alinieleza jinsi umoja wa Afrika tulivyojipanga kukabiliana na jambo hili na jana alitaka tuweke oda yetu ya chanjo, tumetengeza fungu la fedha na jana tumeweza kuweka oda yetu

=> Jitahada zitafanywa kwa wale wote ambao wako tayari kuchanjwa kuhakikisha inapatikana. Kwenye mwili wangu nina chanjo tano na leo ya sita, madhara yalikuwepo wakati ule lakini tulipona na tupo tunaendelea, chanjo ni imeni na kwa wale wenye imani potofu wizara mfanye kazi

=> Pamoja na chanjo nirudie wananchi kuchukua tahadhari, wasanii wamesema vizuri.

=> Kama haujaguswa na maradhi unaweza sema unavyoweza, ila walioguswa na wanatamani kupata chanjo hata sasa hivi

=> Johnson & Johnson ni chanjo moja tu, zile nyingine ndio unachoma mbili. Mtakaochoma leo, msiache kujilinda kwa kuwa wengine hawajachanja bado.


FUATILIA LIVE:



Je Haya hapa chini Samia watalamu wako wameyafanya? I guess huna wataalamu wa kufanya hayo. Twende kazini, hopefully walioitengeneza wamehakikisha hayo yote yako sawa. Tukachanje, it is safe within acceptable limits.

c&p
The critical and essential step for computational vaccinology is to design vaccine construct/s by randomly placing the epitopes and joined them with proper linkers.
The vaccine construct must be safe and effective.
To achieve this, the newly designed construct/s need to be checked for its:
antigenicity,
allergenicity,
toxicity,
solubility
and stability.
The result must show that the construct needs to be
a potential antigen,
non-allergic,
non-toxic,
soluble
and highly stable.

These outcomes make it a suitable vaccine candidate for further analysis.
 
Huoni hapo viongozi wavchini yake wamelazimika kuchwa kulinda vitumbua vyao na wasionekane wasaliti. Very unfair practice.
Nawaona VENANCE MABEYO na SIRRO hawana amani kabisa.

Sio kwamba wanaogopa chanjo ila wanajiuliza ,je watafanyiwa maigizo kama walivyokubaliana au watageukwa wadungwe kitu chenyewe.
 
We unamjua yehova au unalopoka tyu huna kaz hebu kasome Bible huko ndio utajua Yehova alisem nn na saiv kinatokea nin
 
Mguseni muone atakavyokinukisha. Gwajima ana'watu'.
Walifukuzwa akina hayati Aboud Jumbe na HAKIKUNUKA.....

Alifukuzwa hayati Maalim Seif Sharrif Hamad na HAKIKUNUKA.....

Gwajima ni nani ?!!!

Gwajima nani bwana?!!!

Watu aliokuwa nao ni wale anawaongoza "fikra zao".....

HASHTAG GWAJIMA afukuzwe CCM

#GwajimaAfukuzweCCM
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Unaweza usiamini. Yaani mageuzi ya kihistoria haya toka kunywa juisi ya “ukwaju” hadi kutiririka na molecular biology! Salute to Dorothy Gwajima. Panapostahili sifa itolewe! Bila shaka amefuta ile aibu.

Amenifurahisha alivyotanabahisha kuhusu viwango (percentages) vya ufanisi (efficacy) na madhara ya pembeni (side-effects) za madawa yote.

Wasio na uelewa wa sayansi kabisa hawatakaa wajue hili. Kwao dawa/chanjo ni ile inayofanya kazi asilimia 💯 kwa watu wote na isiyo na madhara kabisa! Kiuhalisia, hakuna kitu cha aina hiyo duniani. Wanatuwekea video kibao za anti-vaxxer conspiracy proponents zilizojaa ujinga (ignorance) kibao.

Ni kama pale unapopanda ndege au basi toka DSM kwenda Mwanza umuulize rubani/dereva UNA HAKIKA ndege hii/basi hili halitapata ajali njiani? Unategemea jibu gani?
Maadamu mtu anajaza form kabla ya kuchanjwa kwa litakalompata ni juu yake basi hilo ndio muhimu hayo mengine hayana muhimu tena hapo.
 
Nadhani hiyo sentence ya hachomwi mtu hapa imekutatiza na hujaelewa
Sihamisishi watu wasichomwe bali nimeweka video inayoonesha wakijifanya kuchoma lakini hachomwi mtu hapo
Nimeamua kukufafanulia kwa manufaa ya wengi
Nimekuelewa..Asante
 
Back
Top Bottom