Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Kwa hiyo tutembee kifua mbele kwa kuishi maisha mazuri kuliko wa marekani🤓🤓!
Mama Anaupiga mwingi.
😓😓Petrol itafika 5000 kwa Lita moja
KAZI IENDELEE.
 
Nimeweka kikubwa nomesema kuna kodi nyingi katika mafuta takribani shilling 2000 ni kodi katika Lita mmoja ya mafuta-wewe huoni hapo kuna tatizo??
Kwa taarifa Kodi ni 572 tu wala sio hizo mnazojazana ujinga..

Na hizo Kodi kwa pamoja ziko Kodi muhimu za Mfuko wa barabara Road fund kwa ajili ya Tanroads na Tarura..

Wakifuta hizo Kodi kwa hiyo mwaka huu tusijenge barabara? Na mbaya zaidi ukifuta wala bei ya mafuta Kwa Lita haitapungua zaidi ya 2500 na bado inaweza panda huko tunakoenda kwa hiyo serikali itatoa nini sasa?
 
Nyerere alifosi vyama vingi ila vinakuwa kama kivuli Tu....alifanya hivo ili apate misaada ya mabeberu baada ya kuumia vita vya uganda
Kwani vita vya Uganda viliisha lini na vyama vya siasa vilianzishwa lini.
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.



Huyu mama bwana! Kwani uchumi wetu sawa na marekani!!!! Yaani mi naona tuache tu kutembelea magari wote tupande daladala
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.



(1) New York umeme haukatikikatiki eti kwa sababu ya matengenezo; ukikatika kwa sababu ya storm hutengamaa baada ya muda usiofika hata robo saa. Kuna subways zinatumia umeme, utawakatia umee treni ikiwa shimoni kwa saa moja si utauwa watu wengi sana? Il sasa mama alikuwa Marekani atakauwa anatoa mfano wa kila siku kutoka Marekani kama vile anajua maisha yote ya marekani

(2) Bei ya mafuta Marekani sasa hivi ni wastani wa dola 4 kwa galoni, sawa na dola 1.06 kwa lita au shilling 2,463.65 kwa lita ambayo ni chini ya bei ya Tanzania, kwa hiyo mama hajasema ukweli. Bei hiyo ya marekani pia inachukulia kuwa mshahara wa dereva wa roli la mafuta ni dola 10,000 (Tsh milioni 23) kwa mwezi na mshahara wa mfanyakazi wa kituo cha mafuta ni dola 15 (Tsh 34,862.9) kwa saa. Ni ulinganishaji usiokuwa na mantiki yoyote. Mama aliwahi kusema kuwa waziri fulani alizungumza nonsense!
 
Kwa sasa benchmark ya kila kitu ni Marekani.
 
Bibie ashikilie hapo hapo.
Ili kufikia 2025 tuwe tumeona Kila aina ya rangi na tutaongea lugha moja..
 
Ila kwa kweli kama nchi tumepoteana. Hakuna upinzani wa kuwa mbadala. Na CCM wamepoteana kwa kurudisha makapi ambayo ni kama wakati na jamii walishawachoka.
CCM haina mvuto kabisa na hakuna kiongozi mwenye mvuto ndani ya CCM.

We must be at standby mode!
 
Asee!

Kwa mara ya kwanza ndio nimeamini kuwa tumepigwa
 
Anajilinganisha yeye na marekani hatari?, ajue ni mbingu na ardhi hapo. Atoe makodi yake ili anusuru nchi huyu bibi
 
Hapa ndio Huwa nawadharau waandishi wa Habari wa Kibongo. Anapewa Jibu kama Hilo Naye anacheka cheka na Kulidhia Kweli kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Poor Poor, Wanahabari wetu kudadisi na Kuhoji hawawezi kabisaaaa, Huenda hata Maswali alipangiwa Ya Kuuliza.
 
Screenshot_20220504-202252~2.png

😳😳😳
 
Back
Top Bottom