Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Huyu mama huyu !!!! ??????

Nimeishi UK, kule kila kitu gharama nguo, viatu kodi ya pango n.k. , Ila kipato changu nilichokuwa napata kule kwa wiki kwa kazi hio huku hata kwa mwaka huenda nisingepata..., (yaani hapo naongelea unskilled labor bado sijaongelea professional jobs)

Hivi haya anayasema kama siasa, kukosa uelewa au anatudharau (insulting our intelligence)

Vyote ni sawa tu mkuu..

Kalamu ya kuandikia UK ni pound tatu hio ni shilingi elfu 9 sasa mtanzania hio bei ndio ya kula siku tatu…wapi na wapi…jamani tukubali tu tumepigwa na kitu kizito chenye ncha kali….

Na watanzania tulivyo wapole sasa…
 
Nilikwambia huna akili utabisha?

Ufute Kodi harafu yakipanda tena utafuta nini?

Pili ukifuta Kodi kwa hiyo tuache kujenga barabara(Tarura na Tanroads via Road Fund),tuache kujenga mashule na tuache kujenga vituo vya afya Ili wewe ununue mafuta Kwa bei rahisi? 😁😁😁😁..

Hiyo bulk purchase umekuta haifanyiki? Kwani sasa hivi yananunuliwa kwa utaratibu upi? Eti kutunza kwenye maghala kwani saizi yanatunzwa wapi? Na kama hayatoshi kwani kujenga maghala unadhani ni sawa na kujenga madarasa ya covid 19?

Kwa hiyo mitambo ya kusafisha mafuta ni kama vile mitambo ya kutengenezea boflo na slace sio? Unatumia akili au?

Viongozi kumiliki vituo vya mafuta inahusianaje na kupanda bei Kwa mafuta? Wameanza kumiliki vituo vya mafuta awamu ya 6? Sheria inakataza viongozi kumiliki biashara na mali?

Huo ujinga ulioujaza huko Kichwani ni mzigo tosha,kwamba kwenye Nchi zenye Katiba mpya na Bora bei za mafuta ziko chini sio? Mburula hamtakaa muishe Tzn hii.

Na hizo mbinu zako ni za kutatua kupanda bei Kwa mda mfupi au mda mrefu? Kama ni za mda mrefu utakuwa huna akili na hujajubu swali la unataka nini kifanyike at this moment Ili bei zishuke.
Hapo kwa viongozi kufanya biashara katiba yetu hairuhusu
 
Wastani wa kipato cha Mtanzania mmoja kwa mwezi 500K na litre ya mafuta ni Tzs 3,184 wakati wastani wa kipato cha Mmarekani wa hali ya chini ni 11M kwa mwezi wakati gallon ya mafuta ambayo ni sawa na litre 3.4 ni USD 5.

Sasa hapo nani mwenye nafuu?
Hangaya halijui hilo.
 
Huyu mama huyu !!!! ??????

Nimeishi UK, kule kila kitu gharama nguo, viatu kodi ya pango n.k. , Ila kipato changu nilichokuwa napata kule kwa wiki kwa kazi hio huku hata kwa mwaka huenda nisingepata..., (yaani hapo naongelea unskilled labor bado sijaongelea professional jobs)

Hivi haya anayasema kama siasa, kukosa uelewa au anatudharau (insulting our intelligence)
Anaupiga mwingi anafungua nchi mama yuko vizuri ....hayo mengine hajui anajua bei US ni juu kuliko hapa full stop.
 
Labda hawakumwambia kuwa Marekani mafuta yanauzwa kwa galoni na siyo lita. Na galoni moja ni dola 4.20 kwa sasa. Galoni moja ina lita karibia 4. Apige mahesabu sasa aone kama anachokiongea ni sahihi ama la!
20220501_085419.jpg
 
Wastani wa kipato cha Mtanzania mmoja kwa mwezi 500K na litre ya mafuta ni Tzs 3,184 wakati wastani wa kipato cha Mmarekani wa hali ya chini ni 11M kwa mwezi wakati gallon ya mafuta ambayo ni sawa na litre 3.4 ni USD 5.

Sasa hapo nani mwenye nafuu?
Screenshot_20220504-103044_Chrome.jpg
 
Sasa Uwezo wetu wa kununua ni Sawa na Marekani?? Mama mm sisemi unashauriwa vibaya mana mengine wewe mwenyewe unatakiwa uelewe...Marekani Tujiringanishe nae kwa kipi hasa hata Ukiona Barabara zao ni kama zetu??? Huduma zao za afya ni kama hapa??
Haya ndio tungejilinganisha nao sio kwenye maumivu kama haya ya mafuta..Kule marekani Mlinzi analipwa kwa masaa 8 hapa mtu ni siku 30 na Tucta ndio hiyo ni zero plus.
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Kule wanauza kwa galoni na sio kwa lita wajameni
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Rais Samia Bei ya mafuta itamfanya akimbie nchi​

Per litter bei iko hivi.

Tanzania - $1.354
Kenya - $1.245
US - $1.210
 
Back
Top Bottom