Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Nyie si mlikuwa mnashibikia uvamizi wa Putin Ukraine kama mnaangalia mpira wa Yanga na Simba? Hata kura ya kuukemea uvamizi wa Putin mlikataa kupiga kule UN. Haya ndiyo matokeo yake. Mafuta bei juu, ngano adimu na maisha yanazidi kuwa magumu.
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Swali dogo tu, anafahamu maana ya neno PER CAPITA INCOME??
 
SmartSelectImage_2022-05-04-19-02-32.png
SmartSelectImage_2022-05-04-19-04-37.png

Mengine Kokotoa mwenyewe

Pato la mmarekani ni kubwa kuliko pato la mtanzania uwiano wa pato la mtu na bei za vitu linapunguza sana uwezo wa kununua tz
 
HIVI TANZANIA TUNA THINK TANKS?

Na Thadei Ole Mushi.

Bei ya mafuta imepanda sana lita moja ya Petrol kwa sasa inafika hadi Shilingi 3,000. Nimeangalia Lita moja ya Mafuta hadi inashushwa pale badarini ni shilingi 1,162.

Yakishafika tunaweka kodi na Tozo Mbalimbali hadi yanafikia zaidi ya 3,000.

Kazi ya Ewura ni kutangaza Bei Mpya tu badala ya Ku regulate na kuishauri serikali. Hawana kazi nyingine wao ni kutangaza tu.... hawawezi hata kunusa kinachoweza kutokea baadaye na kutoa Solutions. Nafikiri kwa Sasa Serikali inaweza kufanya yafuatayo.

1. Kwenye kila kipengele cha Tozo wapunguze angalau kwa Ailimia kadhaa, Mfano badala ya VAT kuwa asilimia 18 wafanye asilimia 10 katika kipindi hiki.

2. Kuna haja ya kuindoa Tozo nyingine kwa sasa zisiwepo hadi hali ya Uchumi wa Dunia utakapotengemaaa.

3. Serikali ipunguze Matumizi yake ambayo si ya lazima kwa sasa mfano kutembelea anuani za Makazi kwa Chopa.

Tusikae kimya.....kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa marahisi... tuchukue hatua angalau kidogo tu kuonyesha tunajali. Maumivu makubwa ya ongezeko hili la bei ya mafuta anaumia mwananchi wa kawaida kabisa huku chini.

Hivi tuna Think tanks za kushauri Serikali?

Pale Marekani Washington DC kuna kituo kinachoitwa "Peterson institute for International Economics" (PIIE).

Kituo hiki kazi yake kubwa ni kutafiti na kushauri masuala mbalimbali ya kiuchumi na mahusiano ya kiuchumi. Kwa Marekani ndipo "Think Tanks" wao wanapofanyia kazi. Ili uajiriwe hapa lazima kichwani pawe vizuri si suala la kushukuru kuondoka jalalani tu ila kweli uwe na independent Mind.

Hawa wajamaa wamepewa Uhuru mkubwa sana wa kutafiti na hawafichi kitu report yote wanaitangaza kama ilivyo, kule kwao top Researchers wote wapo hapa wanasugua akili na sio kitambi. Hawa wajamaa wakiitisha press kila mtu anasogelea TV, na kila Media inawasogelea.

Sio marekani tu nchi kibao kama China, India, Venezuela nk zina Pool ya Think Tanks yaani mtu au kiongozi akitaka kufanya jambo lazima awaone. Achana na Hawa unaosikia kuwa ni mshauri wa Rais masuala ya kisiasa au mshauri wa waziri mkuu. Hawa sifa yao lazima kwanza wawe Huru ndio maana kituo hiki cha Marekani ni private institute...

Mfano pale India wao wamegawanya Think Tanks wao kutokana na maeneo mbalimbali, wana vituo 48 vya Think Tanks kama ACDR hawa wanashughulika na Siasa tu, CICR hawa ni Kilimo tu nk.

Pale uarabuni kituo cha Bookings Doha Center January 30 mwaka 2019 waliitisha panel ya Think Tanks wote katika Zone yao. Waliohudhuria ni pamoja na Nader Kabbani, MKUU wa kituo cha utafiti cha (BDC), Ezzeddine Abdelmoula, manager wa utafiti wa Al Jazeera, Mahjoob Zweiri, mkuu wa Gulf Studies Center ya Qatar University, Sari Hanafi, professor wa American University wengine walikuwa Mohammad Almasri mkuu wa Arab Center kituo cha utafiti na undaji wa Sera, Osman Ayfarah, mtangazaji wa Al Jazeera na aliyesimamia majadiliano. Hawa wajamaa wanaiongelea miaka 50 ijayo, mojawapo ya recommendations walizotoa ni Viongozi wao wote kuchukua mawazo kabla ya kufanya chochote kwenye taasisi hizi za Think Tanks.

Nadhani hata hapa kwetu tuna watu wanaoweza kuunda tume ya wachumi wakafanya kazi na mwananchi wa chini akasaidika.

Ole Mushi
0712702602.
 
Vita Ni miaka ya 70 mwishon
Vyama Ni miaka ya 90 mwanzon (~10years)
Hapo unazungumizia zaidi ya miaka kumi, kwa hiyo ktk miaka hiyo 10 uchumi wa Tz hauku tengemaa ?, moja wa viongozi ambao walikuwa hawaamini ktk misaada ni Nyerere na hata awamu yake alivyo vifanya vilionekana,moja ya awamu iliyokuwa na viwanda vyingi ilikuwa ya Nyerere mpaka anaondoka aliviacha vina operate, kusema sababu ya misaada hiyo haikiwa akili yake,kwanza anachukia utumwa kutoka nchi za Magharibi na zilikuwa haziivi na nchi za Magharibi.

Yeye alitaka kila mtu awe free kuchagua chama atakachona ndio maana ,pamoja na vyama vingi kupingwa yy ndiye aliye force kuwepo.Na kama ingekuwa sababu ni hiyo misaada Nyerere hasinge ruhusu vyama vingi, kwani mtu anayeamini maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi na kjjitegemea, kwani katika dunia hii hamna nchi iliyo endelea na kupiga hatua kwa misaada haipo na haitakuja kutokea.
 
Kwa msiyojua haya ndiyo madhara ya kumpa mtu kiti pasipo kuchaguliwa
 
Swali dogo tu, anafahamu maana ya neno PER CAPITA INCOME??
Mafuta ni global commodity. Bei zake zinategemea na soko la dunia (oil markets). Nchi tajiri na nchi masikini zote zinanunua mafuta kwa bei ya soko la dunia. Hakuna tofauti. Labda ununue mafuta ya black market au uchimbe na kusafisha mafuta yako mwenyewe kama wanavyofanya Iran.
 
Kuna wakati naona aibu hata kumsikiliza huyu mama
Mwanaume akiropoka tunasema amelewa.
Mwanamke akisema WANAUME NI SPERM DONAR TU tena mbele ya umati na vyombo vya habari utamwitaje?
 
Yeye alitaka kila mtu awe free kuchagua chama atakachona ndio maana ,pamoja na vyama vingi kupingwa yy ndiye aliye force kuwepo.Na kama ingekuwa sababu ni hiyo misaada Nyerere hasinge ruhusu vyama vingi, kwani mtu anayeamini maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi na kjjitegemea, kwani katika dunia hii hamna nchi iliyo endelea na kupiga hatua kwa misaada haipo na haitakuja kutokea.
Hii sentesi inajipinga, kama alitaka watu wawe free kuchagua kwann aliwalazimisha kitu ambacho hawataki?(vyama vingi)

Nyerere alikuwa Na misimamo hiyo sikatai.
ila ujamaa ulimshinda ndomaana akamuachia Mzee wa ruksa afungue nchi
Kama hujui Mzee wa ruksa alikuja kuficha aibu ya Nyerere maana baada ya ujamaa kufeli Nyerere Alyona aibu kuukubali ubepari ila ikambidi tu ndomaana akàanza kufosi Hizo sera.
Mzee, ujamaa Na vyama vingi Ni paka Na panya.
Usitudanganye hapa Kuwa Nyerere alikuwa mfuasi wa vyote
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.
Mbona hasemi amekuta mishahara ya wamarekani ikoje!?
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Nadhani SSH anaongea kama mwekezaji... Ambapo inawezekana ni kweli... bei ya mafuta Tanzania ni nzuri kuliko Marekani.
 
Hii sentesi inajipinga, kama alitaka watu wawe free kuchagua kwann aliwalazimisha kitu ambacho hawataki?(vyama vingi)

Nyerere alikuwa Na misimamo hiyo sikatai.
ila ujamaa ulimshinda ndomaana akamuachia Mzee wa ruksa afungue nchi
Kama hujui Mzee wa ruksa alikuja kuficha aibu ya Nyerere maana baada ya ujamaa kufeli Nyerere Alyona aibu kuukubali ubepari ila ikambidi tu ndomaana akàanza kufosi Hizo sera.
Mzee, ujamaa Na vyama vingi Ni paka Na panya.
Usitudanganye hapa Kuwa Nyerere alikuwa mfuasi wa vyote
Kwa akili yako Nyerere angeendelea ungesema ni dikteta, huyo Mwinyi alificha aibu ipi? au ndio kila kitu ruksa?

Wewe umesema Nyerere aliruhusu vyama vingi sababu ya misaada.

Ila Nyerere mpaka anakufa pamoja na kuruhusu vyama vingi,msimamo wake ulikuwa ni ujamaa na kujitegemea na mpaka anakufa still bado aliumia watu kuliacha azimio la Arusha so Nyerere hakuamini kama misaada itakuwa soln ya maendeleo ya Tanzania.
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kuwa bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikuwa Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kuwa watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Ukuda huu
 
Back
Top Bottom