Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,160
Na Ukiwatazama hapo waliposhika mabango wana huzuni kweri-kweriDaaah hivi hawa watu wa kuwashikisha mabango namna hiyo huwa wanawaokota wapi? Hao watu huwa wako timamu kichwani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Ukiwatazama hapo waliposhika mabango wana huzuni kweri-kweriDaaah hivi hawa watu wa kuwashikisha mabango namna hiyo huwa wanawaokota wapi? Hao watu huwa wako timamu kichwani?
Akipanda watamwangusha, petrol Ina madhara makubwa kwenye UBONGO wa mwanadamu,
Tanks za mafuta kwenye boda zingerudishwa nyuma kuwanusuru boda na Mawenge.
CCM wamezoea cheap politics.
Kwa hiyo unakazia boda boda ni laana?😂😂😂 yani unaona kuendesha bodaboda ni sawa na kufanya kilimo ???
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua kundi la vijana waliojiajiri kupitia bodaboda na yuko tayari kwenda nao mpaka 2025. Rais Samia Suluhu alizungumza hayo aliposimama kuzungumza na wakazi wa Usa River wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Vijana hao wa Bodaboda walionyesha kumuunga mkono Rais Samia na kusindikiza Msafara wake kuelekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri. Aidha bodaboda .
Madereva bodaboda wamesisitiza kazi yao sio ya laana lakini pia wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuwapa mikopo inayowawezesha kuwekeza kwenye shughuli nyingine kama kilimo na biashara.
![]()
![]()
Unasomesha mtoto wako kwa matarajio aje kuwa bodaboda???Kwa hiyo unakazia boda boda ni laana?
Hamna sio watu, bodaboda wana umoja yaani chama cha bodaboda kama vile cha.cha walimu, chama cha wafanyakaziDaaah hivi hawa watu wa kuwashikisha mabango namna hiyo huwa wanawaokota wapi? Hao watu huwa wako timamu kichwani?
Nakuuliza boda ni laana? Kipato halali unaitaje laana. Siwezi kuacha kwa vile nina kazi, nisingekuwa na ajira rasmi ningefanya boda.
Huna kazi,huwezi kufanya hata siziso rasmi kwa sababu mtu mwenye kazi hafanyi?
Tupambanie KATIBA mpya Ili tuirudishe nguvu KAZI shambani ktk KILIMO Cha kisasa Cha kiviwanda na kibiashara...machinga na bodaboda sio ajira ni kujikimu.
..sera mbaya za Ccm kuhusu ajira, viwanda, na usafiri, ndio zimezalisha machinga na bodaboda.
Kwa mara ya kwwnza ndani ya miaka mingi sana hatimaye CCM tunapiga propaganda nzuriRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua kundi la vijana waliojiajiri kupitia bodaboda na yuko tayari kwenda nao mpaka 2025. Rais Samia Suluhu alizungumza hayo aliposimama kuzungumza na wakazi wa Usa River wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Vijana hao wa Bodaboda walionyesha kumuunga mkono Rais Samia na kusindikiza Msafara wake kuelekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri.
Aidha madereva bodaboda wamesisitiza kazi yao sio ya laana lakini pia wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuwapa mikopo inayowawezesha kuwekeza kwenye shughuli nyingine kama kilimo na biashara.
![]()
![]()
Kwanza hizo sura sio za bodaboda, Mboga saba wote hao yaani hawa CCM wataacha lini uongo wa kudanganya umma?Mabodaboda wako organized kihasi hiki 🤣🤣🤣🤣
What a scene
Anakoipeleka CCM kunafikirisha.CCM saivi wapo kunywa juice tu huku wakichekea tumboni, mama yao kawang'ong'a wao wanachekelea.
Mimi sio CCM ila nina akili ya kusema boda ni informal employment. Inasaidia watu kujikimu katika umasikini wao. Huwezi kuita laana.
Alitakiwa kuchunga ulimi wake akajenga hoja kwa tahadhari kubwa. Sasa yeye kasema ni laana? Laaana?!!!!
Ile midude ndani ya chama cjui Ina mipango Gani kuelekea 2025 Kwa siasa hizi za viongozi wa Yanga kuungana na Simba Fc.Labda Kisiwandui kule
Inategemea na tafsiri yako ya kazi - kwa ujumla shughuli yoyote halali inayomwingizia mtu kipato ni kazi! Umaskini siyo laana ni mtihani wake Mwenyenzi Mungu. Lazima ikumbukwe kwamba matajiri ni maskini watarajiwa. Unayesema wewe ni maskini inategemea unamlinganisha nani! Mtu huyo huyo unayesema ni maskini sehemu nyingine anaonekana ni tajiri, ukimlinganisha tajiri mkubwa Afrika na Bill Gate huyu wa Afrika kwa akili za ovyo ataoneka maskini. Kusema kuendesha Boda Boda ni laana bila kutoa mbadala wa kazi ya kufanya ni ulimbukeni uliopotiliza inabidi ujitathmini kama unatosha kuwa Kiongozi.Hapana bodoboda sio kazi, ya maana ni kupoteza tu mda.
Wangemobilize na kusajiri chama Cha siasa,Ila kila kitu kwenye siasa ni fursa, kila kauli ya mmoja inaweza badilishwa na kuwa fursa kwa mwingine. Ila mwisho wa siku mnufaikaji ni mwanasiasa.
Bado watu wa VICOBA nao kuambiwa pia ni watoto wake.
Siku raia watakapoamka na kugundua kuwa wao sio mitaji ya kura za wanasiasa nahisi hapo tutapata kiongozi mzuri. Kinyume na hapo ni mwendo wa kutumiana na kutupana tu.