Rais Samia: Bodaboda ni watoto wangu nitakwenda nao 2025

Rais Samia: Bodaboda ni watoto wangu nitakwenda nao 2025

Kwenye maisha jitahidi sana usitafute huruma za watu.

Bodaboda wapige kazi tu, ule ni mtazamo wa mtu mmoja na siyo watu wote. Nina uhakika familia zinazonufaika kupitia ajira ya bodaboda zina mtazamo chanya na tofauti.

Bodaboda waache kutafuta huruma kwa Rais maana hakuna atakachofanya kitaongeza mapato kwenye biashara yao zaidi watatumika kisiasa tu.

..kuna waendesha bodaboda na wamiliki wa bodaboda.

..vijana waendesha bodaboda wana hali ngumu ya kipato, afya zao zinaathirika, na serikali haifanyi jitihada zozote kuwakwamua.
 
..kuna waendesha bodaboda na wamiliki wa bodaboda.

..vijana waendesha bodaboda wana hali ngumu ya kipato, afya zao zinaathirika, na serikali haifanyi jitihada zozote kuwakwamua.
Bodaboda ni LAANA, Vijana wamechanganyikiwa na maisha, Ni Walevi wa Pombe kali na watumiaji wakubwa wa bangi na hao wengine ni chini ya miaka 23. kuna dogo miaka 22 ameshakatwa mguu kutokana na ajali ya pikipiki na kilichosababisha ni Double Kick na bangi na harufu ya Petroli inampagawisha, hana mguu sasa hivi kaingia kwenye bajaji na huyo ni mtoto wa Mkulima wa Dodoma huko. Je kuna Mtoto/Jamaa/Ndugu wa Kiongozi wa CCM anaendesha Bodaboda?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua kundi la vijana waliojiajiri kupitia bodaboda na yuko tayari kwenda nao mpaka 2025. Rais Samia Suluhu alizungumza hayo aliposimama kuzungumza na wakazi wa Usa River wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Vijana hao wa Bodaboda walionyesha kumuunga mkono Rais Samia na kusindikiza Msafara wake kuelekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri.

Aidha madereva bodaboda wamesisitiza kazi yao sio ya laana lakini pia wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuwapa mikopo inayowawezesha kuwekeza kwenye shughuli nyingine kama kilimo na biashara.

FqdPZRCXgAEBpec

Image
Msiojua ni kuwa hawa kina Lema tayari wako kwenye payroll ya kodi zetu wanalamba asali.

Bi mkubwa anajua mtaani hakubaliki. Hivyo nia ya kuweza kuchaguliwa ni kuhakikisha chadema anaigawa na kuwapa pesa wenye nguvu ndani ya chadema na matamshi kama ya kina Lema ni Well calculated ili waharibu yeye atengeneze.

Ndio maana kila siku wanamsema mwendazake na sio kueleza sera zao na mikakati.

Na tayari wameshaahidiwa kupewa majimbo wanayotaka.
 
Bodaboda huwa hawanaga upande ukiwapa ten ya mafuta wanakua chawa wako chap tu, hapo kesho lema akiwapa 10 ya mafuta wanasema Ni kweli hii kazi ni ya laana
Bodaboda tupendekeze Jina la Chama Chetu Cha Siasa,

Tukisajili Ili kitutoe hapa tulipo kuelekea kuongoza Nchi kisiasa.

Ndani ya Bodaboda Kuna DEGREE holders, Advanced Diploma, Certificate, la Saba na wasosoma etc.

Tuna Uchumi tayari, sababu tuna vyama vyenye usajili ktk financial institutions,

Vyama vya mikoa vikiungana, tunaweza PATA uongozi wa kitaifa strong,

Matching guys na makundi mengine yaunganishwe kupata nguvu kubwa zaidi ya uungwaji mkono.

Chama Chetu kutakuwa na nguvu kuliko kile chama Cha kishamba kinachotumia Jina la Jembe Magu.
 
Msiojua ni kuwa hawa kina Lema tayari wako kwenye payroll ya kodi zetu wanalamba asali.

Bi mkubwa anajua mtaani hakubaliki. Hivyo nia ya kuweza kuchaguliwa ni kuhakikisha chadema anaigawa na kuwapa pesa wenye nguvu ndani ya chadema na matamshi kama ya kina Lema ni Well calculated ili waharibu yeye atengeneze.

Ndio maana kila siku wanamsema mwendazake na sio kueleza sera zao na mikakati.

Na tayari wameshaahidiwa kupewa majimbo wanayotaka.

..nakupongeza kwa elimu hii uliyotoa.

..tatizo liko kwa Ccm na linasambaa kwenye vyama vya upinzani.
 
Humu mnawakejeli boda ila ndo wa kwanza kusema, ngoja nichukue boda chap iniwahishe mahali flani, si mngekua mnakimbia kwa miguu. Na bado hapo tukiwakagua simu zenu mna namba za boda zaidi ya 20
 
Hamna anae penda mtoto wake awe dereva wa boda boda, achani kumanipulate hao watu kwasbb ya political capital.....mtafutie wstoto wa wenzetu ajira za maana.
Na ndio maana nchi hii kuwafanya bodaboda kufuata sheria ni ngumu sana kwani wanasiasa ndio mtaji wao huo!!polisi wakiwabana sana kwenye kufuata sheria utasikia kiongozi wa chama anaibuka kuwa wasionewe!!
 
..nakupongeza kwa elimu hii uliyotoa.

..tatizo liko kwa Ccm na linasambaa kwenye vyama vya upinzani.
Yaani watu hawajui kusoma na hata picha hawaoni. Style ya Bi. Mkubwa ni ile ya JK. Anakula nao na wao wanazibwa mdomo hawamsumbui ili waendelee kula wote.

Hata vitendo vingi vya ufisadi hawavisemei. Siku wanapewa ruksa kuanza kuzunguka kufanya mikutano wametii maelekezo yake yote kuwa wasiende kumbagaza kuhusu mikopo. Na hakuna mpinzani sasa anayeona kopakopa isiyo na tija kama ni shida. Wanagawana pesa wananchi tunaonekana wajinga.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua kundi la vijana waliojiajiri kupitia bodaboda na yuko tayari kwenda nao mpaka 2025. Rais Samia Suluhu alizungumza hayo aliposimama kuzungumza na wakazi wa Usa River wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Vijana hao wa Bodaboda walionyesha kumuunga mkono Rais Samia na kusindikiza Msafara wake kuelekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri.

Aidha madereva bodaboda wamesisitiza kazi yao sio ya laana lakini pia wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuwapa mikopo inayowawezesha kuwekeza kwenye shughuli nyingine kama kilimo na biashara.

FqdPZRCXgAEBpec

Image
Mahaba ya muda mfupi yameshaanza kuyageukia makundi ya vijana yenye kujihusisha na ajira ambazo ni "extra-legal". Sasa hivi utasikia machinga wakiruhusiwa kufanya biashara zao sehemu yoyote ile, wale wa rangi za upinde wa mvua hutasikia tamko lolote kali likotolewa kama walivyofanya Mseveni na Rutto hivi karibuni.

Watoa uroda kwa buku mbili nao hawatabughudhiwa tena, na biashara nyingine holela zotaachwa zitamalaki kwa kuwa ni ajira kwa vijana kwa lugha ya ki CCM. Wanatumika kwa ajili ya kiki za kisiasa, na pia kama mtaji wa kura kwa watawala.

Ni ukweli kuwa serikali imekosa suluhu ya kudumu katika kukabiliana na suala la ajira ya vijana. Ijapokuwa suala hili ni changamoto ya kiuchumi ya kidunia, lakini pia isiwe sababu ya serikali yetu kujificha kwenye kivuli cha kuhalalisha uholela wa mambo.

Hoja ya Lema nafikiri ingepaswa kujibiwa na viongozi walio ngazi za chini za chama na serikali, lakini siyo Rais mwenyewe kama kiongozi wa nchi. Hivi sheria za nchi yetu zinahalalisha pikipiki kutumika kama chombo cha usafirishaji wa abiria, na tena kwa kubeba mishikaki!?
 
Ukishakuwa masikini na akili uchakaa, bodaboda sio ajira
Mkuu boda boda hazijaanzia huku mzee baba zipo mpaka ulaya yoote,china wana maendeleo na wako juu kuliko sisi ila wanatumia boda boda tena ya baiskeli na wala sio wnafanya mazoezi hapana ni ukosefu wa ajira na family zao zinakwenda MSALANI.
Wewe kama umebahatika kupata hiyo ajira hacha kudharau wenzio wanaume tunapambana huku mtaani na maisha yanaenda tu.
Vijana wa chadema mjifunze namna ya kuwa mnawakilisha hoja zenu vinginevyo mtaishiwa kudanganywa na ccm na nyie mtanasa mitegoni kwao
(Angalia hii LEMA anayeishi nje ya nchi analipwa pesa ya ukimbizi kaja anasema Boda boda ni Laana..mwenye nchi anasema boda boda ni kazi na atawakumbatia mpaka 2025,na kinachofata hapo watapewa mikopo)2025 mnapoteza kura kwa hao maboda boda then mnarudi mtaani kusema hamtambui uchaguzi na mama hamumtambui pia.
 
Back
Top Bottom