Rais Samia: Bodaboda ni watoto wangu nitakwenda nao 2025

Kwahiyo Rais Samia yuko pamoja na Bodaboda wanaokufa kama inzi kila siku?
Kwanini wasikopeshwe daladala kwa vikundi?
 
Acha wajichanganye kuhangaika na wanasiasa!!
 
Mnatumika na ccm Ili mzidi kuwa masikini
 
Asisahau na kuhudhuria misiba yao isiyopangiliwa (untimely deaths) kwa ajali na matatizo ya kifua kwa kuvuta vumbi na hewa yenye moshi wa magari.
 
Kuna bodaboda wengi tu wanalima pia,, hao vijana wana akili usiwachukulie poa
 
..kuna waendesha bodaboda na wamiliki wa bodaboda.

..vijana waendesha bodaboda wana hali ngumu ya kipato, afya zao zinaathirika, na serikali haifanyi jitihada zozote kuwakwamua.
Serikali unataka iwabebe mgongoni ndo ujue inajitahidi kuwakwamua?,, Mikopo inatoka kila siku,, hivi mababu zetu wangekua wanakaa tu mapangoni na kulaumu watawala wao hii dunia ingeendelea kweli?,
Kuna kazi nyingi tu hazihitaji hata mtaji,,
Kulima, kupalilia, kukusanya mchanga na kuuza, kufyatua tofali na kuchoma kisha kuuza, kuponda kokoto, kukusanya chupa za plastic na kuuza viwandani, kufua nguo, kufyagia, kujenga, etc🤷🏼‍♂️
 
Mtoto gani wa Samia ni dereva wa bodaboda? Bodaboda ni mtaji wa wanasiasa
 

..kwani nchi ambazo hawana hili tatizo wanafanyaje?
 
..nazungumzia wanaotumia v-8 sasa hivi, lini wataziachia na kuanza kutumia bodaboda?

..kuthibitisha yuko na bodaboda Maza alitakiwa ashuke kwenye v-8 na kupanda bodaboda.
Ahsante mkuu, huo ndio uzalendo wa kweli kwamba anafanya anachoona kwa wengne kinafaa
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…