Rais Samia CCM watoe amri mfumo wa PEPMIS usimame kwanza mpaka pale mtandao wao utakapokuwa na nguvu

Rais Samia CCM watoe amri mfumo wa PEPMIS usimame kwanza mpaka pale mtandao wao utakapokuwa na nguvu

Majuzi walitoa tangazo la ku-scan vyeti vya shule, kuzaliwa, kuanza kazi, ndoa nk. Iwe imekamilika ndani ya siku 2 la sivyo hupati mshahara. Wenye stationery walipiga pesa balaa. Kila cheti huku kijijini kwetu ilikuwa buku halafu vyeti zaidi ya kumi.
🙄
 
Huu Ni uhuni mwingine Hivi MTU wa Ilagala Kigoma na Kagunga Kigoma Huu mtandao haupo Wala network Hamna, Huyu Ridhione aliona Hilo?? Hawa wanaishi mijini wanawaza kimjini mjini.kwanza Ni uwizi mtupu Huo mfumo..Mama kataza Hilo usiwe mpole Mno na Wewe mama.kuwa mkali Basi.
Mama atakuwa amesikia
 
Wanafanya kwa malengo mahususi,nchi hii inahitaji mental liberation kwa raia wake,nikupe mfano,leo Mpina Luhaga yupo nje ya system anaongea km mzalendo lkn alipokua waziri alikua akiunga mkono mambo ya ajabu alafu ni km anatafuta political sympathy,kasoma upepo 2025 hatoboi ndani,na akitoboa nje analiwa kichwa, udikteta wa mwendazake ndo ulimpa jimbo
 
CCM ni chama chama wakulima na wafanyakazi, lazima kiwasemee watu hawa. Ni wapiga kura wake.

Katika pitapita zangu mitaani, ni hofu imetanda miongoni mwa watumishi wa umma.

Watumishi wa umma wamewekewa mfumo wa kutathmini kazi zao, na wanatakiwa wajaze taarifa zao humo.

Kwa mujibu wa watumishi walio wengi, mtandao huo haupatikani kabisa, na watumishi wanatishiwa kutolipwa mishahara kwa uzembe ambao hawahusiki.

Chama cha Mapinduzi kiwasemee watumishi hawa, mfumo usimame mpaka pale serikali itakapotatua tatizo la mtandao.

Nchimbi, Katibu Mkuu, usikubali chama kilaumiwe kwa jambo ambalo walioliandaa hawakuwa makini. Toa kauli kesho nchi nzima ijae shangwe.
Shida ya huu mfumo una assume taasisi zote zina function sawa na watumishi wote wanaush dar. Hii ilikuwa big mistake
 
Kwan kwenye huo mfumo mnatakiwa kujaza watumishi wote Tz nzima kwa siku moja.?

Yn nyie watumishi wa serikali muda wote n kulalamika vitu vidogo vidogo tuu, mnachojua nyie ni kutaka kupandishwa mishahara tuu bila kupandisha uweledi wenu kazini.
 
Watakwambia Maendeleo hayana Chama. Kiufupi serikali Ina mifumo mingi isiyo na tija na isiyofanya kazi. Naonaga ni miradi ya wajanja wachache kupiga hela za kuanzisha mifumo isiyo na tija.

Watumishi hasa walimu wana ESS ambayo ndani yake una PEPMIS, wana mfumo wa TSCMIS, mifumo yote miwili naona kama ina lengo moja.

Ni Upigaji mtupu.
Hiyo mifumo inawanyanyasa sana watumishi
  1. Wapo wanaosafiri toka vijijini kuja kujazia taarifa mijini, wakijilipia nauli kuja na kurudi, gharama za chakula, gharama za cafe nk
  2. Mtandao wenyewe hauko stable mtu anatumia siku nzima kusubiri mfumo uzunguke asubuhi hadi jioni hamna kitu pengine asubiri hafpdi usiku wa manane
  3. Mtumishi anaacha kuhudumia wateja anakimbizana na mfumo usiotabirika utakuwa sawa saa ngapi matokeo yake hampi mteja huduma wala yeye hakamilishi kujaza taarifa
  4. Customer care wa huo mfumo nao ni pasua kicha, kila mtu anasema lake, na wengiine hawapokei simu na wakipokea hawana maelezo ya kuridhisha wanadhani kila mtu ni mjuzi wa mifumo
Kwa ujumla ni bora kurudi kwenye paperwork huku walikowaleta watumishi ni manyanyaso tu na kutafuta sababu za kutowwalipa mishahara
 
Watumishi wengi sana wanalalamikia huu mfumo wa PEPMIS, naamini tatizo ni mtandao, Serikali ingefaa ihakikishe mtandao uko stable na kuaminika kote nchini ili huu mfumo ufanye kazi, maana ukifungua haufunguki, au hufunguka baada ya masaa kadhaa na unagoma tena, mfumo huu bado ni tatizo kubwa
 
Kwa sasa natamani sana kustaafu, ili nifanye mambo yangu.
Nikifika 55 nastaafu.
Nataka nianze kufuga mbuzi.
Kila kazi ukimwachia mtu anaharibu.
 
Ufungueni Jumatatu hadi Jumatano
Alhamisi haufunguki kabisa.

Sijui kwakuwa watu wengi wanajaza Alhamisi au sababu ni ipi.
 
Jana siku ya Alhamis nikiwa Daresalaam, internet full of charge ilinichukua masaa manne hadi kufanikiwa kuufungua.
Ulichosema ni kweli tupu.

Ila nimegundua ukiufungua Jumatatu, Jumanne na Jumatano unafunguka kiurahisi.
Ila sio Alhamis.
Wahusika fanyieni kazi hii changamoto.
Hii ni Daresalama, sijawauliza jamaa zangu wa Mpitimbi.
Huku Mpitimbi ndio tuna miezi 2 haufanyi kazi wala haufunguki.
 
We utakuwa mwalimu tuu eti toa kauli kesho🤣. Utakuta ela ya bando huna kamshahara kameisha hata June haijaanza😭😭.
Hii nchi tatizo kuubwa kwako unaona ni pepomis sio?
Jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za watu. Ebu chukua huu ushauri utakusaidia siku moja. Leo wana JF tumeuona utupu wa kichwa chako kuwa kichwa chako ni cha kuotea nywele tu na umebeba mzigo wa fuvu usio na faida kwako.

Tafadhali bwana mdogo, chukua ushauri huu. Jitahidi kufucha uchi wa akili yako mbele ya jamii.
 
Jana siku ya Alhamis nikiwa Daresalaam, internet full of charge ilinichukua masaa manne hadi kufanikiwa kuufungua.
Ulichosema ni kweli tupu.

Ila nimegundua ukiufungua Jumatatu, Jumanne na Jumatano unafunguka kiurahisi.
Ila sio Alhamis.
Wahusika fanyieni kazi hii changamoto.
Hii ni Daresalama, sijawauliza jamaa zangu wa Mpitimbi.
Alhamisi ni siku ya masupervisor kuapprove progress reports
 
CCM ni chama chama wakulima na wafanyakazi, lazima kiwasemee watu hawa. Ni wapiga kura wake.

Katika pitapita zangu mitaani, ni hofu imetanda miongoni mwa watumishi wa umma.

Watumishi wa umma wamewekewa mfumo wa kutathmini kazi zao, na wanatakiwa wajaze taarifa zao humo.

Kwa mujibu wa watumishi walio wengi, mtandao huo haupatikani kabisa, na watumishi wanatishiwa kutolipwa mishahara kwa uzembe ambao hawahusiki.

Chama cha Mapinduzi kiwasemee watumishi hawa, mfumo usimame mpaka pale serikali itakapotatua tatizo la mtandao.

Nchimbi, Katibu Mkuu, usikubali chama kilaumiwe kwa jambo ambalo walioliandaa hawakuwa makini. Toa kauli kesho nchi nzima
Wengine hawajui kabisa hata kilichowekwa kwenye mfumo. Je, Serikali inadanganywa? Ndivyo ninavyojiuliza.
 
CCM ni chama chama wakulima na wafanyakazi, lazima kiwasemee watu hawa. Ni wapiga kura wake.

Katika pitapita zangu mitaani, ni hofu imetanda miongoni mwa watumishi wa umma.

Watumishi wa umma wamewekewa mfumo wa kutathmini kazi zao, na wanatakiwa wajaze taarifa zao humo.

Kwa mujibu wa watumishi walio wengi, mtandao huo haupatikani kabisa, na watumishi wanatishiwa kutolipwa mishahara kwa uzembe ambao hawahusiki.

Chama cha Mapinduzi kiwasemee watumishi hawa, mfumo usimame mpaka pale serikali itakapotatua tatizo la mtandao.

Nchimbi, Katibu Mkuu, usikubali chama kilaumiwe kwa jambo ambalo walioliandaa hawakuwa makini. Toa kauli kesho nchi nzima ijae shangwe.
Vile vishikwambi haviwezi kutumika ?
 
Inaonekana hawakujipanga vizuri, Wametengeneza mfumo unaotumia Server resources kubwa kuliko walizo nazo ,
 
Back
Top Bottom