Rais Samia chagua upande wa Haki au Dhuluma, huwezi kwenda na vyote

Magufuri aka jiwe was indeed a dictator, no question about that, and kuhusu kumsema rais ili afuate katiba ni lazima na wala sio ombi, hilo hatutaacha na ndio kwanza kumekucha,
mtakuwa hamna kazi za kufanya endeleeni mwishowe atawachoka sasahivi anawasihi mtulie mwisho atawanyoosha kuliko hata mtangulizi wake si mlikoma eee?
 
Anatujumuisha tu 😂😂😂 eti tunataka!
 
Tuliwaambia JPM ni the best president, mkabishi. Haya sasa mnajinyatua kurudi taratiiiiibu
Hivi maana ya neno Best imebadilika siku hizi?

Magufuli alikuwa ni kichaa tu ambaye akina Kikwette na Mkapa walipuuza ushauri wa Mama yake mzazi. Magufuli alikuwa ni kichaa, mwongo, mwizi, muuaji na DIKTETA
 
Magufuri aka jiwe was indeed a dictator, no question about that, and kuhusu kumsema rais ili afuate katiba ni lazima na wala sio ombi, hilo hatutaacha na ndio kwanza kumekucha,
Kila la heri boss! Wacha nikoleze mkaa hapa nichome mahindi na mishkaki ya paka!
 
Muda si mrefu na yeye atakuwa kama mtangulizi wake tu. Kwa mbaali madaraka yameshaanza kumlevya.

Ukiwa Kiongozi, halafu ukashindwa kutambua mahitaji ya wale unao waongoza kwa wakati huo, maana yake umeshakuwa failure tayari
Huyu mama hamna kitu kabisa.
Ni bora angetoa sababu nyingine kuliko hii ya kusema eti tuinue uchumi kwanza. Kwani nani aliua uchumi?
 
Si ndio waliochagua CCM ikashinda law kishundu au??

Pamoja na wananchi wengine lakini wana CCM ndio walioiachagua ilani ya CCM na kupenda sera zao na ndio maana ikashinda na sasa mama ndio anafanyia kazi ilani hiyo

Hakukuwa na uchaguzi boss, bali kulikuwa na maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Kwa kuwa mama alisema tumkosoe na tumuoneshe njia,
Katiba ni muhimu na huna budi kuifanya kipaumbele kwa taifa letu pia waache watu wafanye siasa freely na uchumi utapanda.

Tengeneza marafiki na washauri wazuri mama utanishukuru baadae.
 
Tatizo ninaloliona kwa sasa ni kuwa SSH anashindwa kujipambanua kama mtenda haki moja kwa moja,
kuna maslahi ya ccm wenzake,wananchi wa kawaida na wapinzani,SSH hajajua au kuamua asimame wapi,
Tatizo katika nchi hii kitu cha kwanza kinacholindwa ni maslahi ya wana ccm,sio wananchi(wanasiasa wa chama tawala)
 
Kwa kuwa SSH = JPM; mbegu ya wazo lako imetua mwambani. Kwa hiyo ninapayuka tena na tena: KATIBA MPYA!!!?
 
Mama SASHA kawakata mdomo jana.

CCM ni ile ile ..

Ooohhhh ni ile ile.
 
Kuruhusu michakato ya katiba mpya ambayo kwa kiasi kikubwa ni ile yenye mashiko ya tume ya Warioba kwa CCM ni sawa na mtu anayejipa sumu huku akijua kuwa inakwenda kumuua.

Kisaikolojia kukubaliana na mabadiliko ya katiba kwa sasa itaifanya serikali isiwe na morali ya kutekeleza yote wanayoahidi bungeni kwa ilani ya CCM. Uwepo wa ukimya kama vile hakuna madai ya katiba mpya unaipa serikali amani ya kufanya kazi.

Ndio ugumu wa JPM na SSH kukubaliana na michakato ya katiba mpya kwamba sio tu wanajikuta wakishindwa kueleweka miongoni mwa wanachama wa chama tawala bali wanaiyona gharama ya kubadilika kulingana na ukweli wa muda kwamba kuna udhaifu mwingi wa kiutendaji unaoonekana miongoni mwa watu wanaoiangalia serikali na inaonekana suluhisho ni uwepo wa katiba mpya.

Marais wanaununua muda, ingawa mategemea ni kuona zile sababu za kuununua muda zinakuwa na mafanikio ya hicho kinachofanyika kwa maana ya utekezaji wa majukumu ya kukuza uchumi.
 
Huyo rais hana akili ya kuchuja article ya Coronavirus ajue tu hii fake news.

Kaja kuhutubia watu kawaambia wajifukize kwa article ya fake news.

Unategemea nini cha maana hapo?
 

..ccm ni chama kikubwa na kikongwe.

..siyo rahisi kuwa swept away na mabadiliko ya katiba.

..kwa upande mwingine naamini ccm ita-gain kwa kuwa mstari wa mbele ktk kuandika katiba mpya, au kuifanyia marekebisho hii iliyopo.

..pia ni vizuri kufanya mabadiliko wakati nchi ina amani, na utulivu, kuliko kufanya mabadiliko under pressure huku kukiwa na rekodi mbaya ya human rights violations.

..Watz huwa hatusubiri mambo yaharibike ndipo tufanye mabadiliko.
 
Tuliwaambia JPM ni the best president, mkabishi. Haya sasa mnajinyatua kurudi taratiiiiibu.
Hapana SSH is the best. JPM alituharibia nchi kabisa ni Mungu tu alituepushia matatizo kutoka kwake maana aliyoyapanga mbele yalikuwa balaa. Tumshukuru sana Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…