Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Salaam

Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Isdor Mpango, amesmea kuwa, Rais Samia kaagiza fedha zilizotengwa kugharamia Sherehe za Muungano, amezibadilishia matumizi na kuagiza zigawanywe sawa kwa bara na Visiwani.

Pia kasema kila upande utajiamulia matumizi ya fedha hizo.
Kugawana ni sawa, je pande zote za muungano zilichangia sawa kwa sawa hadi zigawanishwe nusu kwa nusu?
 
Mil1 haiwez kuwa sawa na mil 60?
Sikatai hili, Lakini kwa huu ubaguzi mnaouanzisha mwisho mtasema mapato yanayopatikana Dar yasigawiwe kwa mikoa mingine, wakati serikali kwenye kukusanya inakusanya na kwenye kugawa inagawa kulingana na stahiki bila kuangalia ni mkoa gani umetoa mapato mengi.
 
Hela yote inayokusanywa na TRA Zanzibar uwa haivuki bahari wakati ile inayokusanywa na TRA Bara inavuka bahari. Huu muungano una mambo ambayo tukiyachokonoa, nadhani tunaweza kuona umauti wa muungano huu.
Unaelewa nini kuhusu mgawanyo wa mapato ya muungano? Na je unajuaje kuwa hiyo ambayo haivuki bahari kuwa ndio kiasi kinachotakiwa kwa ajili ya watumishi wa serikali ya Muungano waliopo Zanzibar?
Screenshot_20210426-153005.jpg

Soma hapo kuanzia kipengele namba 10.
 
Siyo sawa kugawa sawa, Zanzibar ni ndogo sana inabidi ipate kutokana na ukubwa wake.
Kwa mfano wewe hapo mkaungana na rafiki yako kwenye biashara,lkn bahati mbaya au nzuri yeye familia yake ikawa na watu wengi zaidi wakati wewe familia yako ni ndogo,kwenye mgawo wa faida ya biashara yenu utasema we upewe mgawo kidogo kwa vile familia yako ni ndogo? Au utasema mgawane sawa kwa sawa?
 
Una mfano wa kipumbavu sana

Chukua mfano huu: unabiashara ambayo unamiliki shares 95% Na partner mwenye 5% mnagawanaje 50% ?
 
Ni mambo ya ajabu ajabu tu
Ila kama Serikali haina mpango wa kuadhimisha Sherehe za Muungano, kwanini wanatenga bajeti yake kila mwaka?

Kwanini fedha hizo in a first place zisipangiwe shughuli za maendeleo badala ya kuja kuzibadilishia gia angani ilhali kuna vifungu vingi tu vya muhimu vinakosa bajeti katika wakati wa kupanga.
 
Ndio ndio ndioooooo.......................................
Nchi 2 huru ziliungana, hiyo theory yenu haileti mantik yoyote kama muliungana kwa bahati mbaya na nchi ndogo vunjeni muungano, hatamu za muungano zote ziko Tanganyika, Wazanzibar wataenda kuungana ata na Comoro ikibidi au watajitegemea
 
Zanzibar inaidai Tanganyika hela zake nyingi sana
Hilo halina shaka. Lakini ingekuwa vizuri kama ingewekwa wazi Zanzibar wanachangia kiasi gani kwenye bajeti ya Muungano? Kiasi gani cha kodi kinatoka Zanzibar n.k.

Amandla...
 
Nchi mbili zimeungana, sio suala la idadi ya watu.
Kuna mambo mengi sana vizazi vyetu vitakuja kuhoji hapo baadae.
Watu milioni 2 na watu milioni 55 uwape sawa mgao
 
Mheshimiwa Rais Samia Hassan kwa kupitia msaidizi wake Makamo wa Rais ameagiza pesa ambazo zilotengwa kwa ajili ya sherehe za muungano na hazikufanyilka zigaiwe mafungu mawaili moja la Tanganyika na fungu la pili la Zanzibar.

Yaani fifti fifti kila mmoja atatumia kivyake. Angelikuwepo mbabe yule angesema acha zitumike kwa ajili ya maendeleo (ya Tanganyika).

Asante mama damu ni nzito kuliko maji.
 
Mnaitaka Tanganyika??
Mgao wa fedha kwa ajili ya Zanzibar tunajua zitaenda wapi... Je, mgawo wa fedha za Tanganyika zitaendelea kuingizwa kwenye accounts za ccm??
 
Back
Top Bottom