Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Kwa nini Watanganyika hawakusaidia kuunda jeshi la Zanzibar halafu waondoke wawaachie nchi yao?
Usipindishe historia.

Karume mwenyewe ndiye aliyeomba ulinzi kwa Nyerere tangu Mapinduzi ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar haikuwa na jeshi na Karume aliogopa Mapinduzi yatahujumiwa.
 
Bado gia nyingine itabadilishwa chini au ndani ya bahari. Hiyo hamna atakayejua wala kuhisi.
 
Una mfano wa kipumbavu sana


Chukua mfano huu: unabiashara ambayo unamiliki shares 95% Na partner mwenye 5% mnagawanaje 50% ?
Kama ni Milion unampa elfu 15[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii ndio tafsiri halisi ya Jamhuri ya Muungano,kazi iendelee.
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.

Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?

Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda.
Wacha upuuzi, hujui hii ni awamu ya sita?
 
Labda niulize kuwa pesa za gharama za Muungano huwa zinatoka wapi au kwa utaratibu gani.

Pili, je Zanzibar kuna pesa ambayo wanachangia kwenye Muungano kusema sasa warudishiwe sehemu?...
Nafuu umeliona hili Mkuu
 
Mabango, T-shirts, vikofia na Scarf.
 
Bado kidogo itatengwa bajeti ya kuwalisha Masheikh wa Uamsho
 
Hela yote inayokusanywa na TRA Zanzibar uwa haivuki bahari wakati ile inayokusanywa na TRA Bara inavuka bahari. Huu muungano una mambo ambayo tukiyachokonoa, nadhani tunaweza kuona umauti wa muungano huu.
Ya TRA inavuka bahari. Labda kama unasemea ZRB.

Na kuna wafanyabiashara wanalambwa kodi na TRA na ZRB kwa mpigo
 
ni sahihi kwa mujibu wa katiba JMT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…