Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Km mkoa wa pwani na chato walikua wanagawana robo inaenda mkoa wa pwani na nusu inaenda chato sidhan km ni kosa bara na visiwan kwenda pasupasu
 
Kumbuka ni awamu ya sita na huyo hayati unayemtaja unateseka bure awezi kurudi na safari yetu sote ila yeye katangulia tu.

Jikite kwenye mada
 
Msingi wa kugawana nusu kwa nusu ni kama hiyo pesa mmeipambania wote.

Now kodi siyo swala la muungano.

Hivyo hii pesa kama imetoka Znz pekee au Bara pekee ni pesa ya aliyeitoa kwakua kaitafuta chini ya kipengele ambacho hakipo chini ya muungano.

Hivyo kushare ni sawa na kusema kuna upande umnyonye mwingine.
 
Muda ufike tuidai Tanganyika yetu
Binafsi sijawahi kuona kama Zanzibar ina tija yoyote ile kwa Tanganyika! Hivyo hata siku wakitaka kujitenga, wajitenge tu.

Wanakula tu kodi zetu kwenye bunge letu la Tanganyika! Sijui wanamuwakilisha nani!! na wakati kule kwenye bunge lao, huwezi kumkuta Mtanganyika!

Kama siyo unyonyaji ni nini huu!! Kila siku kazi yao kulia lia tu na kunung'unika! Wazanzibari sijui ni watu wa aina gani! Wanataka usawa wa mgawanyo kati ya watu takribani milioni 50 kwa watu milioni 2 tu!!
 
Mm naona tumewalea sana WAZANZIBAR kila wakideka na kulia lia kuhusu UNION NA NON UNION MATTERS wacha kazi iendelee.
 
Watu tunapigwa na ccm mchana kweupe lakini bado ajabu akili hazitii akili.

Samia ni ccm ile ile katika vazi la kike.

"Ukishangaa ya Chato utaona ya Zanzibar"
 
Serikali ya muungano ndiyo inayogharamia muungano kwa kodi yetu, wengine wanashiriki tu na ndio maana suala la muungano lipo kwa makamu wa rais, iweje hiyo hela igawanywe nusu kwa nusu wakati ni ya Bara?
 
Hii elimu ya muungano inabidi ifundishwe sana hasa ktk kizazi cha sasa ili kukwepa mkanganyiko siku za usoni.
Vijana walioko shuleni kwa sasa hakuna wanachokijua kuhusu muungano zaidi tu ya kujua kwamba tar 26 April ni siku ya mapumziko ya muungano and no more.
 
Zanzibar ni nchi kamili usisahau hilo bwashee!
 
Km mkoa wa pwani na chato walikua wanagawana robo inaenda mkoa wa pwani na nusu inaenda chato sidhan km ni kosa bara na visiwan kwenda pasupasu
Bora na Chato naweza kwenda kununua kiwanja,Zanzibar siwez mtu WA Bara hawaruhusu kununua kiwanja, ila wao wanaruhusiwa. Daaah ila sisi wabara chini ya CCM wametuzidi akili.
 
Ccm na Zanzibar ndiyo chanzo kikuu cha Tanganyika kuto kupiga hatua kubwa ya Maendeleo! Haiwezekani watu wako milioni mbili kasoro, halafu wapate haki sawa na watu milioni 60 kasoro!

Kwanza ka nchi kenyewe ni ka visiwa! Kamezungukwa na maji pande zote! Muda wowote ule kanamezwa tu na hayo maji! Halafu wanatudekea dekea hapa! Wajitenge halafu waone kama tutapungukiwa chochote.
 
Serikali ya muungano ndiyo inayogharamia muungano kwa kodi yetu, wengine wanashiriki tu na ndio maana suala la muungano lipo kwa makamu wa rais, iweje hiyo hela igawanywe nusu kwa nusu wakati ni ya Bara?
Chief naona umeandika nilichoandika.

Now hii ni gharama ya kuungana na uliyemzidi
 
Serikali ya muungano ndiyo inayogharamia muungano kwa kodi yetu, wengine wanashiriki tu na ndio maana suala la muungano lipo kwa makamu wa rais, iweje hiyo hela igawanywe nusu kwa nusu wakati ni ya Bara?
Serikali ya muungano au serikali ya Tanganyika ndio inagharamia?
 
Chato ya Zanzibar 🤣
 
Huyu mama ameanza kufeli hata kabla hajaanza na utawala wake ni huu ambao hakuchaguliwa tu, 2025 hata asijidanganye kugombea
 
Kama tunakubaliana kuwa Zanzibar ni nchi, basi na tuelewe kuwa hakuna nchi nusu. Rwanda ina raia milioni 10, Nigeria ina raia zaidi ya milioni 100, lakini zote Rwanda na Nigeria zina kura moja katika AU, UN na kwingineko ambako kura zinahusika.
Katika partnership ya huu muungano wa Tanzania, Zanzibar na Tanganyika ziliingia na one vote each, as sovereign countries. Baada ya muungano, Tanganyika ilibaki na hadhi yake yote na ikaongezewa pia hadhi ya kusimamia mambo yaliyokubaliwa yawe ya muungano, ndio kusema serikali ya jamhuri ya muungano ni extension ya ile ya Tanganyika kwa kuongezewa madaraka. Zanzibar ilibaki na serikali yake lakini ikapunguziwa nguvu kwa kukosa jeshi la ulinzi, polisi, mambo ya nje, na benki kuu, kwahiyo ni kama serikali butu hivi. Hakuna ubaya kuilea serikali ya namna hii kwa kugawana vitu kama hivyo ambavyo mmetaja kuwa vimegawanywa kwa namna hiyo, kwani inasaidia pia kuwapunguzia hisia za unyonge na pia inaimarisha maelewano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…