Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Tafadhali rejea jedwalu la kwanza la katiba ya jamuhuri ya muungano wa tz item namba 10,
Income tax
Custom duty na
Exercise duty
Ni jambo la muungano isipokuwa VAT
 
Fungua macho mkuu utaona manufaa ya Zanzibar kuwepo kwenye muungano.
Fikiria ukiwa sobber kabisa bila kuwa na upande
 
Tafadhali rejea jedwalu la kwanza la katiba ya jamuhuri ya muungano wa tz item namba 10,
Income tax
Custom duty na
Exercise duty
Ni jambo la muungano isipokuwa VAT
Mimi haikua jedwali ni Civics ya form two.

Which makes sense ukizingatia mtu anaweza nunua kitu Znz kisha akafika Bara na kutakiwa kulipia kodi tena hicho kitu.

Unamaanisha taasisi inayoshughulikia kodi Bara ndiyo ile ile inayoshughulikia kodi Znz?
 
sisi ndie tunaolazimisha muungano huu uendelee kuwepo hivyo usishangae kwa hiki kinachoendelea. hata kwenye mahusiano ukilazimisha kuwa na mtu asie kupenda lazima atakupa masharti magumu lengo ni kukukomoa tu.
 
Fungua macho mkuu utaona manufaa ya Zanzibar kuwepo kwenye muungano.
Fikiria ukiwa sobber kabisa bila kuwa na upande
Wakati ule ambao Bara ilikua inahofia mapinduzi na maadui kutumia Znz kama njia ya kuanzisha mashambulizi.

Hii sababu is no longer valid kwakua tukitumia logic hiyo hiyo basi itabidi tuungane na Kenya, Uganda, Congo, Msumbiji na Malawi.

Kuna kipi Bara au Znz inafaidika na Muungano?
 
Makubaliano ya mambo ya muungano yanatakiwa kuwekwa wazi tuone kipi ni kipi kisha wananchi ndio wataamua ili kuepusha balaa. Zanzibar inachangia kitu gani kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kila upande huchangia kiasi gani?
 
Tunajadili ujinga, tunapogawana mali ambayo tuna umiliki sawa huwa hatuangalii umbo la mtu. Mfano mirathi utasema bonge apate nyingi kwa sababu ni bonge kuliko kimbaumbau?Watanzania tushafuzu nishani ya juu ya ujinga
Fedha za Tanganyika zitaingia kwenye akaunti gani??
 
Budget ya sherehe ya muungano inachangiwa na nani?
Mara nyingine tusiwe tunalalamika tu. Tuende mbele zaidi na kujikumbusha kuwa tunatakiwa tupambane na kufanya kazi kweli kweli ili tupate maendeleo.
Siasa hizi zinadumaza sana. Unaweza kufikiri meli zina lolote la maana kumbe ni zile zile siasa.
 
Kwa mantiki hii CCM hawatakaa wakubali katiba mpya.
 
Mtu anachaguliwa na watu elfu 6 anapokea pesa ya bure bungeni
 
Sio vijana wanaccm wenyewe hawaujui huu muungano mtu kama polepole anachoamini ni tofauti nq msimamo wa chama chake
 
tulia sindano ikuingie, ilikua Chattle, sasa ni Kizimkazi
 


Na nyie mlivyowanyonya tangu 1964!!!😜
 
Serikali ya muungano ndiyo inayogharamia muungano kwa kodi yetu, wengine wanashiriki tu na ndio maana suala la muungano lipo kwa makamu wa rais, iweje hiyo hela igawanywe nusu kwa nusu wakati ni ya Bara?
Wewe juha tu, serikali ya muungano unaijua? hao wanaoshikiri wanashirikishwa vipi katika muungano usiowahusu? huyo makamu wa rais unaesema anashughulikia suala la muungano ni wa Serikali ya Jamhuru ya Tanzania au Tanganyika ... mmevimba mabichwa lakini hamna akili.
 
Ndio muungane sasa na hao wakenya sijui kwanini mnachelewa na kuwakumbatia wazenj ambao hamnufaiki nao kwa kitu chochote.
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.

Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?

Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda.
Yani kwa sababu tu Zanzibar inapata pesa ya muungano kama mdau namba moja wewe inakuuma sana hadi unaona sherehe ifutwe duh! mko na roho mbaya... sijui ilikuwaje yule mzee tukafika kuungana na wakatili.
 
Labda niulize kuwa pesa za gharama za Muungano huwa zinatoka wapi au kwa utaratibu gani.

Pili, je Zanzibar kuna pesa ambayo wanachangia kwenye Muungano kusema sasa warudishiwe sehemu?...
Hilo nalo neno. Nijuavyo mimi mambo ya Muungano yanaendeshwa kwa fedha zinazopatikana Tanzania bara ukiacha mikopo toka nje ya nchi. Mathalan, Zanzibar wana mamlaka ya kodi wakati mamlaka ya kodi ya Muungano, yaani TRA huwa haikusanyi kodi huko Zanzibar.

Wazanzibar lazima waelewe kuwa kama hawajadai kuchangia katika Muungano basi wakae kimya kuhusu mgawo wa kitu ambacho hawajachangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…