Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Kwanza bajet ya sherehe za muungano znz walihusika....kama walihusika wachukue chao kama sio basi anawapendelea tuu
Nadhani bajeti ya sherehe za muungano hupangwa na waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano.na vyanzo vya fedha vinatoka pande zote mbili za muungano.
 
Punguza hasira boss, Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazounda muungano
Kaka nakushukuru kwa kulitambua hili. Lkn ninachoweza kusema kutokea moyoni in kwamba, Mfumo wa muungano haujawa rafiki kwa sasa kwa kuwa, kama kuna nia ya dhati kabisa ya kuungana kati ya BARA NA ZANZIBAR Nini kinachokwamisha kuwa na muungano wa nchi moja? Watawala wakubali tuwe na Taiga moja kuanzia MWANZA hadi WETE, MAKUNDUCHI - UZINI hadi RUVUMA, SONGWE,MJIMKONGWE HADI BUKOBA NA KIGOMA. Rais awe mmoja tu itakuwa poa sana.
Punguza hasira boss, Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazounda muungano
 
Dodoma!

Akizungumza Leo katika kongamano la Muungano jijini Dodoma, Makamu wa Raisi Dr . Philip Mpango amesema Raisi Samia Suluhu Hassan ameelekeza Fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zigawanywe pande hizo mbili (Tanganyika na Zanzibar) ili zikafanye shughuli za maendeleo!

Dk. Philip Mpango ametumia takribani dakika 20 kuhutubia wanakongamano na Kisha kuondoka ili aendelee na shughuli zake za Kila siku za kulijenga taifa!

Source: TBC
Bajeti ilikuwa Tsh ngapi?
 
Kila mmoja arudishiwe chake alichochangia katika sherehe hiyo maana kinajulikana halafu awamu hii hatutaki fedha za dhuluma.
 
Awamu hii Zanzibar inakumbukwa saaaaana kwny mgao.

Mtu kwaoooooooooo.
Yes, Kama chato, Tena afadhali ya Zanzibar maana ndio inakamilisha maana halisi ya jamuhuri ya muungano wa tz, kwaiyo lazima ipate mgawo aswaa wa fedha,

kuliko chato wilaya yenye watu elfu hamsini, magufuli alipeleka miradi ya mabilioni ya pesa" mzee alikuwa mbinafsi aswaa
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.
Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?
Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda
Sherehe kuifuta haitakua vyema kwakua ina wakilisha umoja na kuanza kwa kuitoa ni ishara ya mgawanyiko hivyo. Bajeti inatakiwa iwe well stated and pre-planned kwa vitu vingine. Waseme bajeti ya muungano itatumika kadha kadha kabla ya siku ya tukio apo kweli.
 
Salaam

Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Isdor Mpango, amesmea kuwa, Rais Samia kaagiza fedha zilizotengwa kugharamia Sherehe za Muungano, amezibadilishia matumizi na kuagiza zigawanywe sawa kwa bara na Visiwani.

Pia kasema kila upande utajiamulia matumizi ya fedha hizo.
Dr. Mpango si makamu mteule, ni makamu wa raisi, maana ameshaapishwa tayari
 
Rais yupo sahihi. Ni hela ya Tanzania na sio Tanganyika. Tanganyika haina Tanganyika Revenue Authority. Ni hela iliyokusanywa na Tanzania Revenue Authority ambayo baadhi ya mapato yanatokea Zanzibar.
Ni mpaka Tanganyika iwe na institutions zake ndio inaweza claim kitu flani ni chake! So far, we shut up
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.
Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?
Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda
Nadhani jiwe lengo lake ilikuwa tu ni kutaka sifa
 
Back
Top Bottom